Tumefanya kosa kubwa kupeleka siasa mashinani, Wahusika zimeni huu upepo

Midimay

JF-Expert Member
Apr 12, 2015
2,907
4,770
Mojawapo ya sababu vya nchi hii kuwa na utulivu kwa upande wa Tanganyika, ni kwa sababu ya mkakati wa viongozi wa mwanzo kuepuka kupeleka siasa kali mashinani kuanzia enzi ya TANU, UTP ya Zuberi Mtemvu, ASP,ZNP hadi enzi za TADEA na CHAUMMA. Siasa kali mashinani siyo. Kulitakiwa kufanyike mkakati kuepuka siasa kali za ushindani huku mitaani kwetu.

Kuna kosa nchi hii imefanya kuanzia washauri wa mambo ya siasa hadi TISS na hata vyama vya siasa.
Mimi nashauri huu upepo wa uchaguzi wa serikali za mitaa tunaoukomalia Kama Uchaguzi Mkuu, uzimwe kwa nguvu zote. Kitengo fanyeni kazi. Naamini mnajua na mna taarifa Kama huu upepo ni natural au man made. Na Kama ni man made, je kutoka ndani au nje? Na Kama ni nje, kwa jirani au kutoka mbali?
Huu upepo uzimwe kwa kuufutilia mbali huu uchaguzi usifanyike kabisa.
 
Hakuna maisha bila siasa au siasa bila maisha. Hao watawala wamesahau kuwa ni wananchi ndio wanaowapa mamlaka. Wafikirie hilo tu.
 
Tufunge, tuombe na kusali sana ili Mola atuepushe kwani sasa ni kama 'vita imeshushwa chini'

One of the impediment of development in Africa is religion, Kuomba na kusali sidhani kama kunafanya kazi (samahani najua nagusa wengi kwa kusema hili), we have fundamental universal laws that govern this universe and our lives in general, one of them is CAUSE and EFFECT, it states that for every effect there is definite cause, likewise for every cause there is a definite effect.

Kwa maneno mengine matatizo uliyonayo wewe leo ni matokeo ya maamuzi yako uliyoyafanya jana, kama situation uliyonayo sasa huipendi fanya maamuzi tofauti leo. Kwa bahati mbaya waafrika hizi laws either hatuzijui au tumepumbazwa sijui, yaani unafanya maamuzi ya kijinga leo ya kutaka kukandamiza watu wengine halafu unategemea outcome nzuri? Biashara ya kukimbilia nyumbaza ibada kuomba vitu ambavyo viko obvious hata mungu hapotezi muda he is very busy with most important stuff.
 
Ndicho tulichokuwa tukikitaka miaka yote wananchi wa chini wajue kinachoendea sasa ndugu na rafiki zao wamekatwa wakiona tunakoelekea ndiko pazuri zaidi kwenye wananchi wote kujitambua.
 
Hii nchi ni kubwa sana , mleta mada umetumia mifumo yako ya fahamu vema sana. Naamini umesukumwa na uzalendo kwa nchi yako. Huu upepo uzimwe.
 
Hii ndo democracy, ukisema ufutwe ina maana unataka jambo la ushirikishwaji ambalo ndo msingi wa demokrasia ufutwe. I don't agree with you. Dawa ni uwazi na ukweli, mtu ashindwe anaona wazi kwamba namba zimekataa, sasa mtu namba zinakataa anatangazwa chini ya mtutu wa bunduki halafu unakuja na hoja za ajabu.

Hatua ya chini ndo mwananchi wa kawaida anajiona kwamba naye ameshiriki katika kufanya maamuzi ya mustakabali wa nchi yake.
 
Back
Top Bottom