Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Mwaka 2016 unaisha. Tunatarajia mwaka mpya 2017. Siku zinapita na wala hazirudi nyuma. Katika masuala makubwa makubwa yaliyotikisa taifa letu lipi limefanikiwa au tumevumisha tu kupiga kelele kwa mambo au ambayo hayakuwapo ila tumefanya vile ku-draw attention ya media bila impact kwa jamii ya watanzania kiuhalisia?
1. Tulianza na watumishi hewa, je wameisha? Waliosababisha hilo tatizo wako wapi ni akina nani?
2. Kutumbua, kumeleta tija kwa taifa au kumejenga woga?
3. Sakata la sukari kufichwa na itakayopatikana ingegawiwa bure kwa watanzania? Ilipatikana? Iligawiwa? Lini wapi na walionufaika na sukari ya bure ni akina nani? Bei elekezi ya sukari ya serikali ni 1800, je hapo ulipo wanauza kiasi gani leo?
4. Mbwembwe za Mawaziri kuwahi ofisini hadi kufunga geti ili kubaini wanaochelewa zimeisha lini? Na Waandishi walipataje taarifa kuwa waziri atawahi kufunga geti ili wampige picha
5. Ziara za kushtukiza za Mawaziri, na viongozi wengine zilizokuwa zinasheheni waandishi zimeisha kwanini? Mwakani zitajirudia?
6. Fedha zilizokuwa zimefichwa na wafanyabishara zimetolewa? Hatua gani imechukuliwa.
7. Kukatika umeme ilielezwa itakuwa ndoto, hali ikoje sasa
8. Mbwembwe za mahakama ya mafisadi zimeishia wapi? DK Mwakyembe amesema watuhumiwa hakuna.
9. Sakata la Faru John litaishaje, na kwanini lilipewa umuhimu kuliko miili 7 ya mto ruvu na kupotea Ben Saanane.
10. Wapiga dili tulioambiwa watachukuliwa hatua kuwa walitaka kutugombanisha na Dangote wamechukuliwa hatua gani, ni akina nani?
HERI YA MWAKA MPYA 2017, MUNGU ATUSAIDIE KUKOMAA SHINGONI KWENDA JUU.