Kwa kipindi chote cha urais wa JPM karibu mwaka mmoja na miezi nane kulikuwa na maswali mengi ni wapi anatupeleka Rais JPM. Kuanzia kisiasa, kiuchumi, kijamii na maendeleo kwa jumla watu walijiuliza mwelekeo wake. Alizuiya siasa ili afanye kazi za maendeleo na alisema anabana matumizi ili kuokoa fedha na aliahidi Tanzania ya viwanda.
Muda huo wote wachunguzi walikuwa wanatazama mwelekeo na viashiria vya azma yake. Kwa maoni yangu hakuna mpya na mwelekeo haujawekewa misingi. Anachokifanya ni kucheza na akili za watanzania na kupigiwa vifijo vya siasa za propaganda na wafuasi wake.
Kinachojidhihirisha kama taifa kuna malalamiko upande mmoja na upande wa pili kuna sifa zisizo mashiko, Bungeni kuna malalamiko ya ubaguzi wa kiitikadi, kwenye serikali kunalalamikiwa matumizi ya madaraka ya kukomowa wapinzani na kukosekana uvumilivu. Kuhusu ajira mianya imejificha bado na biashara zinadorora. Wananchi wanalilia ukata wa fedha na ugumu wa maisha.
Hali hio wenyewe wanaikataa na kusifia tu na hawataki kukosolewa kwa lolote. Misingi imekosekana ya kupigania kile alichokiamini Rais JPM huo ndio ukweli.
ANAKOTUPELEKA.
Kwa mnasaba wa maelezo hapo juu, Tanzania sasa inaelekea kwenye visasi vya ubaguzi na kukomoana, kukosa uvumilivu miongoni mwa watanzania na kukosa umoja wa dhati. Huku ndiko tunakoelekea.
Kwa bahati mbaya JPM na wasaidizi wake hawajaliona hilo na taratibu hii tabia inazoeleka miongoni mwa jamii.
Mifano iko mingi. Mara ngapi serikali imetowa kauli tata za kukatisha watu tamaa na kufanya mambo yasiyo shirikishi ? Kila kinachofanywa kina mnasaba wa kujitafutia sifa NA UMAARUFU TU NA KWA MUDA MFUPI UNAGUNDUWA DHAMIRA ZA KISIASA ZILIZOJIFICHA NYUMA YAKE. Lile la madawa ya kulevya, ufisadi, vyeti, na mekanikia yamepita na mwisho inaonekana kuwalenga watu fulani tu.
Mara ngapi kuna undumi la kuwili wa maamuzi ya serikali? mambo haya huacha mwanya wa ubaguzi na kukosesha umoja kama nilivyosema.
Kule bungeni ni ushahidi tosha wa kipimo cha Tanzania ilivyo. Kama spika imefika mahali anasikitikitia kususiwa futari UNADHANI KUNA NINI? HUO NDIO UHALISIA.
Tumetoka kwenye matatizo yaliyovumilika , sasa tunaelekea kwenye matatizo yanayolazimisha kupotea kwa uvumilivu. Huku ndiko anakotupeleka rais Magufuli.
Kishada.