Tumechoshwa na CCM jimbo letu la Monduli

"Mh.Shikamoo!" Si rushwa ila ujumbe huu umetoka kwa mtu aliyemsalimia Mh. na yawezekana ni jamaa na mkubwa wake wa Huko Monduli. Lakini usingeandika comment hii kama isingekuwepo neno hili "Shikamoo" katika post!Tafadhali lete maoni makini kwa manufaa ya umma. Posts zangu ziko hewani mara kwa mara kwa sababu zinajenga uelewa kwa watu makini.Hakuna rushwa. Narika katoa salamu hiyo! Upo hapo mkuu!

Okay mkuu nilishakuambia kwamba komaeni mpaka kieleweke kwani kila kitu kinaeleweka hasa ukizingatia huyo wanaesema yupo strong kwa kuwa hamjawapa nafasi watu wengine, hivyo imani yangu ni kuwa kuna watu wengi wazuri hawapo kwenye system ila wamekosa fursa au wamenyimwa fursa kwa zengwe kupata nafasi. Mfano mzuri mtu anapokuwa anakubalika utasikia mbunge alieko madarakani anapita na kusema kuna watu wanapita kuwaadaa wananchi.
 
Mkuu Mpungati, usemayo ni kweli!, hata wa Misri wanajuta!. Wairaq nao ni majuto, Libya Mmarekani amelipa kwa damu ya balozi wake!. Mungu bariki kwa Monduli, jamaa anajifurahisha!. Kile ni kisiki cha mpingo, kamwe hakingoleki bila kukatwa katwa kwanza!. Ili Chadema kuishika Monduli, kwanza ama wamshike mwenye Monduli yake, au wamsubiri CCM imkatekate na kummaliza ndipo waje kujiokotea jimbo!.
Ni kisiki cha mpingo huko huko Monduli wanakovaa shuka mpaka leo. Sio sehemu zote watu wanavaa shuka utawaimbia Lowasa ni kisiki cha mpingo wakuelewe. Hebu uje huku Tarime utuambie Lowasa ni jembe kama hujaondoka na ngeu.
 
Ni kisiki cha mpingo huko huko Monduli wanakovaa shuka mpaka leo. Sio sehemu zote watu wanavaa shuka utawaimbia Lowasa ni kisiki cha mpingo wakuelewe. Hebu uje huku Tarime utuambie Lowasa ni jembe kama hujaondoka na ngeu.
Kwani 2015 ni mbali?!..
 
Kwani 2015 ni mbali?!..
Si mbali. Na wala usijipe matumaini makubwa. Nchi imebadilika kama hujui. Jirani zangu hapa waliochagua ccm na mwaka 2010 nilipata shida kuwashawishi kutoichagua ccm kwa mshangao wanasema hawataki kusikikia kitu ccm. Hebu tathmini tu Lowasa Keshapoteza wanachama wa ccm kiasi gani na akigombea watakaotoka zaidi ni wangapi. Hiyo haitoshi. Vyama vya upinzani wanahitaji tu kuhamasha watu kupiga kura. Watu wakihamasika hata wangekuwepo Lowasa 10 watadoda tu.
 
Back
Top Bottom