Tumechoka na maneno yenu, tunataka kuona vitendo

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,048
Anzeni na account ya muhindi iliyopata $12 millioni na account nyingine zote zilizosambaziwa pesa toka kwenye account hiyo na pesa hizi zirudishwe kwenye mfuko wa Taifa.

TAKUKURU noma!

2007-12-04 15:43:55
Na Mwandishi Wetu, Jijini


Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuipa ruksa ya kufanya chochote kilicho ndani ya uwezo wake kughughulikia mafisadi nchini, sasa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, TAKUKURU, ni noma kweli kweli.

Chini ya mikakati yake mipya, TAKUKURU imeapa kuyakomba mapesa yote yaliyotwaliwa kwa njia za rushwa na baadhi ya vigogo Serikalini na watu wengineo nchini kabla ya kwenda kuyaficha kwenye akaunti za mabenki yaliyo nje ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa toka kwa chanzo chetu ndani ya TAKUKURU, ni kwamba chini ya mkakati huo, baadhi ya vigogo wenye tabia za ulafi wa mali za umma wataipata freshi.

Kimesema chanzo hicho kuwa hadi sasa, mkakati huo uko katika hatua muhimu inayoweza kuzaa matunda katika kipindi kisichokuwa kirefu kuanzia sasa.

Chanzo hicho kimeihabarisha Alasiri kuwa hatua hiyo, ni sehemu ya mbinu za kisasa zinazoendelea kubuniwa na TAKUKURU katika kukomesha vitendo vya rushwa kubwa kubwa (grand corruption), ambayo hurudisha nyuma nia njema ya Serikali katika kuwaletea maisha bora wananchi wake.

`Mara zote, wala rushwa kubwa kubwa hukimbizia mapesa yao katika akaunti za nje ya nchi? sasa TAKUKURU iko katika mchakato wa kuhakikisha kuwa mapesa hayo yanarejea nyumbani ili yatumike kwa maendeleo ya nchi,`kikasema chanzo chetu.

`Mkono wa TAKUKURU utafika Uingereza, Ufaransa, Italia, Uswis na kokote kule duniani? pia wahusika watachukuliwa hatua za kisheria, tena bila kujali nafasi zao katika jamii,` kikaongeza chanzo hicho.

Aidha, katika kuthibitisha kuwa sasa TAKUKURU imepania hasa kuwaletea noma wala rushwa vigogo almaarufu kama mapapa, jana Mkurugenzi wake mkuu Dk. Edward Hosea alizungumzia suala hilo la kurejeshwa kwa fedha na mali zilizosafirishwa nje ya nchi kwa njia ya rushwa jana.

Dk. Hosea alizungumzia suala hilo wakati akiwa kwenye semina ya masuala ya rushwa iliyofanyika katika hoteli moja Jijini ambapo mwezeshaji mmojawapo katika semina hiyo alikuwa Bw. Alan Bacarese.

SOURCE: Alasiri
 
Hivi BUBU, unajua kuwa ARI MPYA, KASI MPYA, NGUVU MPYA NA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA hiyo slogan ni ya miaka 20? Sasa hivi 2005-2010 ndo kipindi cha hali mpya, 2010-2015 ndo tutaingia Kasi mpya, 2015-2020 itakuwa Nguvu mpya na Maisha bora kwa kila Mtanzania ni kuanzia 2020-2025. Nadhani hapo atakuwa ameshapatikana mtu mwingine mwenye maneno ya kutia moyo zaidi. Hizo i propaganda tu, nchi ina wenyewe, na utauzwa tu hata wewe
 
Hivi BUBU, unajua kuwa ARI MPYA, KASI MPYA, NGUVU MPYA NA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA hiyo slogan ni ya miaka 20? Sasa hivi 2005-2010 ndo kipindi cha hali mpya, 2010-2015 ndo tutaingia Kasi mpya, 2015-2020 itakuwa Nguvu mpya na Maisha bora kwa kila Mtanzania ni kuanzia 2020-2025. Nadhani hapo atakuwa ameshapatikana mtu mwingine mwenye maneno ya kutia moyo zaidi. Hizo i propaganda tu, nchi ina wenyewe, na utauzwa tu hata wewe

Kiatu tafadhari,
naomba kuto kukubaliana nawewe katika hili, hii nchi ni yetu wote, si ya wachache yaani wao!

Ni dhambi kubwa sana kukata tamaa nakuona kwamba uwaachie wenye nchi!

Kwa vile ni yetu wote, ndugu nakusihi tujifunge kibwebwe kusambaza habari za kuidai nchi yetu kwenye mikono yao, ili irejee na kuwa yetu wote!

kazi ni moja tu kumtaarifu na kumueleimisha mwenzio juu ya hili naye amtaarifu mwenzake na hivo hivo bila kukoma. Tukishirikiana, wote tutaamka!

Penye nia pana njia, naamini inawezekana, tutaikomboa nchi yetu na irudi kuwa yetu wote si yao peke yao! Tena mapemaaa!! sihuko 2020 ambapo walio wengi tutakuwa tumeisha lala usingizi wa milele! Saa ya ukombozi ni sasa
 
hivi wanajambo tukiamua kuchanga pesa na kupinga maovu kinagaubaga si itakuwa poa.
wewe ulie Amerika ,london urusi na china rudini tuikomboe nchi,au mnasema je??
 
Hivi habari toka Alasiri inahitaji kweli hata kujadiliwa?

Hawa huwa wanaamua tu cha kuandika ili wauze magazeti, ukweli asilimia tano na uwongo asilimia 95, bora pesa zimeingia.
 
hivi wanajambo tukiamua kuchanga pesa na kupinga maovu kinagaubaga si itakuwa poa.
wewe ulie Amerika ,london urusi na china rudini tuikomboe nchi,au mnasema je??

Inawezekana tu, hakuna shida. Sema shida itakuwa kwa wale ambao wako huko kimazabe mazabe, wanaishi bila makaratasi.
mimi niko tayari.
 
Back
Top Bottom