Tumechoka kuongozwa na Rais wa miundombinu na uchukuzi, tunataka Rais wa nchi

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,234
Watanzania tumechoka kuongozwa na Rais aliyeathiriwa na mahaba yake kwenye wizara yake ya zamani ya uchukuzi na miundombinu.

Rais aliyefika ikulu akajigeuza Waziri wa miundombinu na uchukuzi. Rais anayependelea sekta moja tu.

Haiwezekani Rais akaelekeza miradi yote sekta moja tu yaani ya miundombinu na uchukuzi sijui ndege, flyover, mabarabara, reli, vivuko na meli, viwanja vya ndege, bandari nk haiwezekani.

Tunahitaji Rais atakayebalance kila kitu. Sasa Rais anayeegemea sector moja sekta zingine anamwachia nani?

1. Wizara ya kazi na ajira hakuna alichofanya, haajiri, hapandishi mishahara wala vyeo, vijana wapo hoi hawana matumaini.

2. Wizara ya mifugo na uvuvi ndiyo usiseme.

3. Wizara ya fedha na uchumi Hamna alichofanya, deni la taifa limepaa, wananchi wanalia, biashara zinakufa, makodi na vikwazo chungu mzima.

4. Viwanja na biashara tunaambiwa viwanda vimeongezeka hatuvioni sijui ndiyo cherehani nne kiwanda?

5. Wizara ya Kilimo usiseme hakuna kitu.

6. Wizara ya afya ukiondoa hivyo vidhahanati viwili vitatu alivyojenga, vifaa hakuna shida tupu.

7. Elimu ukiondoa elimu bure, mikopo ya elimu ya juu wanaopata hawafiki nusu, na wao mara wakatwe, na wanatishiwa wakijaribu kugoma.

8. Utalii ukiondoa ndege hamna kitu chochote alichofanya.

9. Utawala bora, haki za binadamu , katiba na Sheria hapa hata sisemi, hakuna alichofanya.

10. Nk.

Sasa tunataka Rais atakayegusa nyanja zote za maisha ya mtanzania ambaye hatapendelea sekta moja ya miundombinu na uchukuzi. Rais huyo si mwingine ni Tundu Lissu tu.
 
Kabisa, tumekuwa na mtu anayefanya anachotaka wala sio wanachotaka wananchi kwa kweli ni shida sana sasa tubadilishe mtu na chama pia.
 
Mhhh jiongeze nje ya mtandao,wale mamilioni ya wananchi wakulima,wafugaji,mamazetu mijini na vijijini waliondolewa kutwishwa ndoo ya maji,bodaboda,Elimu bure,umeme wa REA,barabara za kumwaga,utaonekana kituko.

Hao watu mara zote wanajiandikisha kupiga kura na wanampigia kura CCM.
Kumbuka uchaguzi unaishia kwenye sanduku la kura.
 
Back
Top Bottom