Tumechoka kuendelea kuokoa maiti kwa sababu ya uzembe wetu wenyewe - gazeti la chama

MNYOO JOGOO

Senior Member
Apr 2, 2012
195
94
Picture1.jpg

Inasikitisha kuona tunaendelea kulalamika kuhusiana kuanguka kwa majengo mbalilmbali jijini, sababu zinajulikana na inasikitisha zaidi pale ambapo tumekuwa tukitafuta mchawi kumbe vitu vipo wazi na vinajulikana, Takwimu zinaonyesha kuwa Cement ambayo ni the 2nd consumable good on earth baada ya maji. Inafurahisha zaidi kuona kuwa cement kutoka Tanzania zinaubora unaiwezesha kuwa used wherever here on earth in the construction industry. Serikali imeepuuza hili matokeo yake sasa ujenzi usiozingatia viwango umeendelea kugharimu maisha ya watanzania wenzetu kwa kuruhusu cement zisizo na ubora kuingia nchini.

Tunapoelekea kusikiliza Bajeti ya serikali, ni busara sasa serikali ikaona umuhimu wa kuiangalia hii sector kwani inaweza kutusaidia fedha za kigeni through export, zaidi iangalie ubora wa cheap cement zinazoigia nchini holela kwani zimeechangia kugharimu nafsi za watu ambao wamekuwa ni nguzo muhimu katika kusukuma gurudumu l a maendeleo nchi.
 
umeongea vizuri sana mkuu, tatizo kubwa sio serikali, ni uaminifu mdogo uliopo kwa wafanya biashara na wale wanaojenga, wanapenda vitu vizuri kwa gharama ndogo..lile ghorofa lilikuwa la ghorofa 9 huyu jamaa akapandisha 16 kiutapeli na kiwizi
 
umeongea vizuri sana mkuu, tatizo kubwa sio serikali, ni uaminifu mdogo uliopo kwa wafanya biashara na wale wanaojenga, wanapenda vitu vizuri kwa gharama ndogo..lile ghorofa lilikuwa la ghorofa 9 huyu jamaa akapandisha 16 kiutapeli na kiwizi

Babako, ni kweli uaminifu miongoni mwa wafanyabiashra nchini umekuwa mdogo sana, tumeshuhudia mengi yanayotokea pale bandari. But unadhani bila usimamizi mzuri wa serikali tunaweza waondoa vipi watu hawa wasio waaminifu? Mfano nimesoma gazeti la serikali leo- Twiga Cement imeprovide ajira kwa watazania zaidi ya 1000. Zaidi inasikitisha kuona taasisi zetu zimeendelea kuwaacha hawa importers wa njia za panya ambao achilia mbali kutotoa ajira kwa wazawa, wameendelea kuiibia serikali kwa kwa kutoa taarifa za uongo za mizigo inayoingia nchini. Serikali inapoteza zaidi ya 29Bilioni kwa hawa cement importers peke yake, achilia mbali upotevu kwa waagizaji wa bidhaa nyingine. Serikali inahitaji kuamka kuliko kuendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu namna hii.
 
Back
Top Bottom