Tumechagua Makamu wa rais Mgonjwa

muheza2007

JF-Expert Member
Mar 19, 2010
483
771
Makamu wetu wa rais ameondoka kwenda Ulaya kwenda kufanyiwa check up ikiwa ni kama mwezi tu tokea apate madaraka hayo.

Inaelekea tumechagua makamu mgonjwa na sasa inakula kwetu.

Inasemekana ameelekea Uingereza.

Habari ndio hiyo tujadili.
 
Suala la afya nafikiri hakuna mwenye guarantee nalo. Tungeweza kuchagua mwingine yeyote lakini akaugua ndani ya wiki moja na kufariki. Hakuna anayejua kitakachojiri dakika hata moja mbele. Unajua wewe utakuwa mgonjwa lini na utakufa lini? Kama hujui, basi tumwachie Mungu kwa kuwa wote siye ni wa kuugua.
 
Kwani binadamu haumwi? tumpe muda katika katiba yapo yanayocontrol hili kama ni mgonjwa kweli. Ila cha kushnagaza ni je Prof Pallangyo pale MUHAS amekosa Prof/Dr wa kumhudumia jamani?
 
Ukiongelea ugonjwa nini makamu wa rais, tumechagua rais mgonjwa.
 
Ukiangalia picha za siku aliyotangazwa kuwa makamu rais anaonekana choka mbaya. Nikadhani maisha ya jua kali. Sasa kama wote wagonjwa........
 
Tuwatakie afya njema tu. Sisi sote tunaugua kwa namna moja au nyingine.
 
Mbona hili la afya linajulikana wazi waulizeni wazanzibari walilizungumzia sana wakati wa makundi ya urais wa zanzibar hawakujua kwamba wanatoboa siri.



Hatari lakini salama
 
Huko kwao walimchaguwa ili asiweze kugombea Urais baada ya miaka 5 kwisha kwa sababu atakuwa mzee sana... Calculated!

Tumuombee dua kama binadamu arudi salama. Ugonjwa hauchaguwi ila wangetumia hizi hospitali za hapa kwetu.
 
Ni kwelii kuugua hakuepukiki ila nikumuomba Mungu awaepushie viongozi wetu na magonjwa.
Kikubwa ni serikali kuboresha matibabu katika hospitali zetu zilizopo nchini ili wakiugua watibiwe hapa hapa.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa biologically no one is safe as we are all subjected to death at one point in time. Ila likelihood ya kufa inatofautiana mtu na mtu. Kama wewe una virusi vya ukimwi basi likelihood yako ni kubwa kuliko yule asiye navyo japo yeye anaweza kuanza kufa kabla. Sasa katika hali ya kawaida watu huwa wanapunguza likehood hasa kwa viongozi kwa kuhakikisha wanakuwa na afya njema na mojawapo ni hii ya kumpeleka nje VP kwa check up. Ila kama akigundulika mjonjwa basi likelihood yake inakuwa kubwa zaidi. Kwa hiyo tujue kuwa nature haimguarantee yeyote kuiona kesho. Ndiyo maana kwa sisi waumini huwa tunasema mungu akipenda tutaonana.
 
Jamani waboreshe Muhimbili ili wapunguze matumizi makubwa ya kuenda ulaya kutibiwa,Tunamwombea heri aende na arudi salama hatutaki vilio sasa hivi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom