Tumebuni mfumo (IT solution) kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo (agriculrural value chain) tunatafuta mdau wa kufanya naye kazi

kt the irreplaceable

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
1,107
2,000
Hi wakubwa.
moja kwa moja kwenye mada, tumedisign mfumo (it solution) kwenye mnyororo mzima wa thamani kwenye kilimo (agricultural value chain) ambao utarahisisha mahusiano na mawasiliano kwa washikadau (stakeholders) wote ambao wanaingia kwenye sekta hii ya kilimo na ufugaji. washika dau hao wanaweza kua taasisi za fedha kama banks, insurance, pia wadau muhimu kama serikali au Ng'os, wanunuzi wa mazao, wauza pembejeo na mbegu pamoja na wakulima wenyewe.

je mfumo unafanya nini zaidi? mfumo huu una pande mbili, ambazo ni android app, na web based (backend). Android app ni kwa ajili ya kuingiza taarifa na backend kwa ajili ya kutoa taarifa (reports). zifuatazo ni vipengele vilivyopo kwenye mfumo (modules)

.1 USAJILI (PROFILING MODULE)
hapa mfumo unaweza kuchukua (capture) taarifa zote muhimu za mkulima ambaye ni mdau muhimu kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo. taarifa hizo ni kama vile, majina kamili ya mkulima, namba ya simu, namba ya nida, picha ya mkulima, taarifa za shamba lake, jinsia, umri, taarifa za kidigitali mahali shamba lilipo ( geo coordinates) taaarifa za kikundi ikiwa mkulima yupo kwenye kikundi chochote pamoja na alama ya kidole ikiwa kutakua na ulazima.

.2 MAFUNZO (TRAINING & COACHING MODULE)
Pia mfumo unaweza ku capture (kuchukua) taarifa zote ikiwa mkulima atataka kupata mafunzo yoyote kutoka kwa taasisi yoyote, mafunzo hayo yanaweza kua, jinsi ya kulima kisasa ( good agricultural practice) mafunzo ya kifedha (financial education) nk

.3 TAARIFA ZA MIKATABA (CONTRACT FARMING)
Hapa mfumo unaweza pia kutunza taarifa zote za kimikataba, ikiwa mkulima au wakulima watakua na mkataba na mnunuzi wa mazao hayo.

. TAARIFA ZA MBEGU NA MAVUNO (INPUTS & YIELDS)
Mfumo una uwezo wa kurekodi taarifa zote za mbegu na mbolea ambazo mkulima alitumia mwanzoni mwa shughuli yake, pia kurekodi taarifa za mavuno mwishoni wakati wa mavuno.

. 4 TAARIFA (REPORTS)
Hii ni sehemu ambayo mtu anaweza ku access taarifa (reports) mbalimbali ambazo atazihitaji, mfano idadi ya wakulima, idadi ya waliopata mafunzo, mavuno ,historia nk . reports zinaweza kua kwenye mifumo tafauti tofauti, either excel au graphical.

. MFUMO WA MALIPO (PAYMENT SYSTEM)
NB; Mfumo ni customized (unabadilika kulingana na mahitaji ya mtu)

FAIDA ZA MFUMO
1) Utunzaji sahihi wa taarifa
2) kuaminika kwa taarifa za mkulima
3) kuvutia washika dau muhimu kama wanunuzi wa mazao ambao ni rahisi kufanya tathimini za kibiashara
4) kuaminika na benk au kampuni za bima ili upatiwe mikopo au bima.
5) kuvutia uwekezaji
6) data sahihi kwa ajili ya takwimu.

Ikiwa kutakua na mdau ana maswali, maoni, support au ushirikiano wa kibisahara, tafadhali usisite kuwasiliana nami kupitua anuani zifuatazo
email; michae@rems-africa.co.tz au andrewmichael245@gmail.com pia namba ya simu. 0715 45 56 49.

mike.
 

Cybergates

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
467
1,000
Japo sijaisoma mpaka mwisho imeona hii post yako nimekumbuka kitu. Kipindi cha nyuma kidogo nilikua naskiza bbc swahili ile ya saa 12 na nusu kwenye redio walikua wanafanya mahojiano na developer wa nigeria wame develop app ambayo mkulima anaitumia ku detect ugonjwa wa mazao yake kwa ku piga picha jani au mche wenye dalili azizozielewa mfano mm nimelima maharage yangu baada ya mda naona majani yanabadilika rangi kuliko niende kumtafuta mtaalam wa kilimo mm na piga picha app ina cheki ina nipa result kama ni ugonjwa au mmea umekosa maji, kama ni ugonjwa app ina ni recommend dawa za kutumia

Nilikua nawaza hapa kama ungeweza ku apply iyo feature kwenye system yako ingesaidia sana alfu pia nadhani github kuna source code unaweza uka zi clone japo shida itakua ni kupata data picha ku train iyo ai model

1-s2.0-S1110866520301110-gr2.jpg
 

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,986
2,000
Tuelekeze hiyo app ìnapatikana wapi tuipakue tujiridhishe ndipo maswali yaje,Hivi vitu km apps sio vya maneno matupu.
It man hana maneno mengi kama mwanasiasa.
 

kt the irreplaceable

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
1,107
2,000
Japo sijaisoma mpaka mwisho imeona hii post yako nimekumbuka kitu. Kipindi cha nyuma kidogo nilikua naskiza bbc swahili ile ya saa 12 na nusu kwenye redio walikua wanafanya mahojiano na developer wa nigeria wame develop app ambayo mkulima anaitumia ku detect ugonjwa wa mazao yake kwa ku piga picha jani au mche wenye dalili azizozielewa mfano mm nimelima maharage yangu baada ya mda naona majani yanabadilika rangi kuliko niende kumtafuta mtaalam wa kilimo mm na piga picha app ina cheki ina nipa result kama ni ugonjwa au mmea umekosa maji, kama ni ugonjwa app ina ni recommend dawa za kutumia

Nilikua nawaza hapa kama ungeweza ku apply iyo feature kwenye system yako ingesaidia sana alfu pia nadhani github kuna source code unaweza uka zi clone japo shida itakua ni kupata data picha ku train iyo ai model

1-s2.0-S1110866520301110-gr2.jpg
Ahsante sana mkuu, umetuongezea kitu.

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 

Mega Mind Nyerere

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
2,142
2,000
Habari mkuu nimepitia bandiko lako. Nimeona mmefanya kitu kikubwa cha ubunifu.

Naweza kupata website/blogu yenu ili niweze kusoma na kujifunza zaidi kuhusu project(s) zenu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom