Tumeanza kutumia shuleni kitabu kimoja nchi nzima

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,684
Ama kweli baadhi ya watanzania wenzetu wamelogwa na aliyewaloga sijui kagoma kuwasamehe.

Leo katika kipindi cha kipima joto kinachorushwa na ITV, nimeshangaa na kusononeka moyoni kuna watu bado wanakomalia kuendeleza mfumo wa kutumia wachapisha mbali mbali vitabu eti viwe vingi na kuchochea ubunifu alisema ndugu Benjamin Nkonya kutoka shirika sijui la TAMONGSCO.

Jamaa kaongea upuuzi sijui ni mwehu au kaishiwa pesa? Kwanza jamaa ni MTU mzima anashindwa kukumbuka ni kitu gani kilisababisha elimu ya Tanzania kudhoofu katika ubora.

Ndugu mwana JF je ni kipi bora zaidi kutumia kitabu kimoja nchi nzima au vitabu tofauti kila shule kama ilivyokuwa hivi miaka michache iliyopita na kama madai ya huyo jamaa Benjamin Nkonya//Nkoya sijui.
 
Wamelogwa = Wamerogwa, hivi hujui bibi kifimbocheza amerudi?
 
Naona huyu Bwn. Nkonya kakuudhi kweli kweli mpaka unatoka povu tu badala ya kuweka hoja yako vizuri tukaona faida na hasara ya kutumia kitabu kimoja nchi nzima vs. vitabu tofauti. Nijuavyo mimi ni vizuri kuwa na kitabu kimoja cha msingi (core textbook) halafu kunakuwa na vingine vya kujazilizia. Hivi vya kujazilizia (kiada?) Wizara inaweza kupendekeza na shule zinaweza kuamua kuvitumia vyo vyote zipendavyo ila kuwe na core textbook moja kwa kila somo kwa nchi nzima. Am I making sense?
 
Back
Top Bottom