Tumeanza kupotea Utambulisho wetu kama taifa?

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Siku hizi nimeanza kupata wasiwasi sana juu ya utambulisho wetu wa makabila. Sijui nini kinatokea kwenye jamii zetu.

Juzi nilikiwa na kijana mmoja kutoka mkoani Mara katika kujitambulisha mpaka nilishtuka sana, kwani kwenye utambulisho wake sikusikia majina niliyo yazoea kutoka mkoa huo kama Marwa, Mwita, Nyambaza, Marogo na kadhalika.

Unakuwaje Mkurya halafu unaajina yote ya kizungu? Eti Mkurya anaitwa James Michael Charles.
Kuna sehemu tunakwama sana kama taifa.

Si kwa Wakurya pekee, hata Wahaya majina kama Rwechungura, Rweikaza, Mjwahuzi, Rwegoshora yanaishia taratibu.

Waha nao majina kama Ndalichako, Bhilikundi, Bhilikunzira, Chubwa, Kalankwiye hayapo tena, kule Mbeya nako majina kama akina Mwandosya, Mwampiki, Mwakatika yanapungua sana.

Kule Tanga Lushoto akina Shebughe, Shelutete yako mwishoni sana kuishia.

Zamani kwa Wachaga ilikuwa ni kawaida sana kusikia majina kama Kileo, Munisi, Shayo nao siku hizi umkuta Mchaga anaitwa Albert Robert Bryson. Hii ni hatari sana.

Kuna haja ya kupitisha sheria kila Mtanzania kumlazimisha jina lake la tatu angalau liwe la ukoo ambalo ni UNIQUE na liwe la kibantu kabisa vinginevyo tutapoteza utambulisho wetu kama taifa na majina hayo kupotea.

Zamani mtu akijitambulisha umajua kabisa katokea upande gani wa Tanzania kwa kutaja jina kale tu.

Kwa nchi kama Rwanda na Burundi bado wanatumia sana majina yao ya asili kama ilivyo pia kwa Nigeria na Ghana kuna majina ukiyasikia moja kwa moja unajua yanatokea nchi hizo
 
Kwa E.Africa ni Kenya Burundi na Rwanda ndio wabadumiaha majina yao.
Njoo Bongo majina yetu kina Brighton, Brian, Gift n.k
Upande wa waislamu napo ndio shida kina fahyma, ukhty, yassir nk.

Mimi binafsi mtoto wangu anajina la asili SHIJA na nikiongeza mwingi mwendo huohuo.
 
Umeandika kitu muhimu, utakuta watoto majina yote ni ya kizungu au kiarabu. Maana yake huheshimu historia yako, ulipotoka. Hujitambui, wala kuwatambua wazazi wako, babu, bibi zako.

Tumeingia kwenye utamaduni wa ajabu sana.
 
Nini kifanyike mkuu?

Elimu, tujue historia yetu ya ukweli, rangi yetu, umuhimu wake, kwamba sisi tulikuwa viongozi duniani, ni watu wakarimu, wenye upendo, tulikuwa na maendeleo kwenye nyanja zote.

Tuandike vitabu vyetu, kuwafundisha watoto wetu historia sahihi. Elimu ya kumjenga, kujiamini, kufikiri.

Mzungu, Mhindi, Mwarabu,Mchina anawafundisha vijana wao historia yao, maarifa ili kufanikiwa duniani. Sisi tumekariri ujinga Livingstone, Leakey, Burton, German, British, Arabs walifanya hivi, vile sio wewe ulifanya, umefanya nini hapa duniani.

Hadi Mungu tunamwabudu ni Mweupe, Mchina ana Buddha, India Krishna, Mwarabu Mohammed, Sisi tuabudu mmoja wa hao.

Hata Malaika ni weupe, Shetani tu mweusi.
 
Back
Top Bottom