Tumeachana, lakini kila asubuhi na jioni hunisalimia

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,432
2,892
Mimi ndo niliamua kumuacha huyu binti kutokana na sababu zangu binafsi ambazo ziko nje ya uwezo wangu.

Nilifuta na namba yake kabisa, kumbe yangu ameikariri. Kinachoendelea sasa hivi ni kila asubuhi anatuma ujumbe wa "asubuhi njema" na jioni atatuma ujumbe wa "usiku mwema".

Siipendi tabia hii maana amenifanya mpaka nimeikariri namba yake.

Ni majibu gani yanamfaa huyu?

Tumeachana lakini kila asubuhi na jioni hunitumia message.
 
Acha unafiki, hapa MMU umejikutaje humu? au ni lupango tuseme umeswekwa bila hiari yako, grow up basi🙄

Alfajiri, Asubuhi, Adhuhuri, Mchana, Alasiri, Jioni, Usiku, Usiku wa manane ni mapenzi mapenzi mapenzi, tunashindwa wapi Wanaume kushughulisha akili zetu wenyewe kimaamuzi hadi tuwe vilema namna hii kiakili lakini?
 
Acha unafiki, hapa MMU umejikutaje humu? au ni lupango tuseme umeswekwa bila hiari yako, grow up basi
Hujanielewa na ndiyo maradhi ya kukurupuka jinsi yalivyo.

Namaanisha si kila kitu kuhusu mapenzi lazima kijadiliwe JF, 7bu kupambanua mengine kwa akili za kuzaliwa si dhambi, la sivyo ni ulemavu wa juu sana.
 
Alfajiri, Asubuhi, Adhuhuri, Mchana, Alasiri, Jioni, Usiku, Usiku wa manane ni mapenzi mapenzi mapenzi, tunashindwa wapi Wanaume kushughulisha akili zetu wenyewe kimaamuzi hadi tuwe vilema namna hii kiakili lakini?
Angalia majukumu yako mengine Kama ukiona jukwaa hili huliwezi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom