Tumeacha kujadili 'Budget' tumepewa Chalamila tumjadili

Hii bajeti ndiyo itakayomnyonga kwelikweli mnyonge na kupandisha gharama za maisha kwa hali ya juu kama mambo yasipokuwa managed vizuri tutegemee mfumuko wa bei
 
Mwanasiasa mmoja aliwahi sema 'Watanzania wana akili kama za kuku'
kuku huwa anatabia ya kusahau haraka sana. anaposogelea ama kula nafaka ya bosi wake, huwa anafukuzwa kwa kutumia ka sauti fulani hivi ambako huwa hakana madhara kwake. Haitachukua muda atarudi tena palepale alipofukuzwa. this time atafukuzwa kwa kurushiwa ama jiwe au kipande cha ukuni. lakini hata choka, muda mfui tena anarejea ili andelee kula nafaka ya boss wake. boss safari hii anaamua kumuumiza kabisa huyo kuku. Na mara nyingi huwa ni kutenguliwa baadhi ya viungo kama miguu, shingo, au mabawa. ataruka kwa sauti yenye kuashria maumivu makali kisha atakimbia. baada ya muda mfupi tu tena, atarudi akiwa amejeruhiwa huku akijivuta kuja eneo lilelile asilotakiwa kuwapo.

'Watanzania tunaumizwa mara nyingi mno na serikali yetu kupitia viongozi wetu, lakini hatujawahi kukumbuka na kufanya maamuzi mengine magumu ili kuepukana na maumivu hayo. Hata watesi wetu wanajua hatuwezi kufanya chochote zaidi ya kulalamika kwenye mitandao' Tutaendelea kuumizwa kama kuku kila sikua kama hatutafanya maamuzi magumu sasa au hata hapo mbeleni.
 
Elimu duni ya wananchi wengi ndiyo inawapa kiburi watawala ambao wengi wao pia ufisadi umewatawala

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Sio Hii wizara inaitaji
Burudani za Mama zimezidi utamu, anazidi kuwatengua Watesi wa Wananchi, Bajeti hata tukiijadili imeshapita.

Burudani! Burrudani! bado tu ya Professa Mussa Assad aishike Wizara ya Fedha halafu Lameck Madelu akafuge Fisi Iramba.
Sio siri hii wizara inaitaji mtu mtendaji alifikia mafanikio makubwa kama Asad,Kimei,siyo huyu alie ajiriwa kwenye fani yake ya uchumi mwaka sijui tena level ya chini ,mara yuko ofisa wa siasa chamani .elimu yote alionayo ya uchumi mpaka PhD niya darasani,hiyo experience ya economy ameipatia wapi na lini !!??
 
Na ashafahamu watanzania ni wepesi sana. Wanataka burudani. Wakija shtuka miaka imekatika hamna jipya....
Ni staili ya uongozi wa JK hii!

Ilikuwa akiboronga yeye anapanda ndege huyoo ughaibuni au linatokea tukio ku cover lile la kuboronga mwishowe miaka yake 5 ikaisha
 
Mkuu budget, ya mwaka huu, inarejesha kodi ya kichwa, sijajua Kama wataalam na washauri Kama wanafanyaga study tour baadhi ya Nchi au huamua liwalo liwe ilihali wapo ndani ya V8 , wanalipiwa nyumba, vocha,suti nk ,

Leo bibi yangu niliemnunulia sim ya kitoch ili niwe namsalimia mnamlipisha lain , nikituma pesa nayo mnalamba, wakati huo kampuni ya sim inawalipa kodi itokanayo na miamala, vocha nikinunia nalipa kodi ,ila bado mnataka tena, kule kodi ya jengo kupitia luku,

Chama tawala ubunifu umefika MWISHO katika kulisogeza taifa mbele, kilichobaki ni kuumiza wananchi , huku wachache mkila mema ya Nchi
Nyie endeleeni kumjadili Chalamila ndio ana umuhimu kwenu
 
Sio Hii wizara inaitaji

Sio siri hii wizara inaitaji mtu mtendaji alifikia mafanikio makubwa kama Asad,Kimei,siyo huyu alie ajiriwa kwenye fani yake ya uchumi mwaka sijui tena level ya chini ,mara yuko ofisa wa siasa chamani .elimu yote alionayo ya uchumi mpaka PhD niya darasani,hiyo experience ya economy ameipatia wapi na lini !!??
Unajua kuna baadhi ya wanaccm wanafikiri Nchi hii ni yao peke yao kuna nafasi ambazo Mama Samia anatakiwa aweke watu wenye uwezo bila ya kujali kama ni Makada wa Chama au la.
 
Budget imesomwa jana na Waziri wa Fedha asiye na ubunifu, mwenye akili chovu mchama na si mtanzania. Kama Uchawi upo na unafanya kazi Mganga wa Mwigulu ni wa kujengewa Sanamu katikati ya Jiji.

Nchi za watu wenye akili wangetumia muda mwingi sana kuijadili budget. Kuangalia mazuri na mabaya yake. Kupongeza na kukosoa.

Kwa nchi kama ya Tanzania ni rahisi kututoa kwenye reli. Tumepewa Chalamila Tuhangaike naye. Budgeti si issue kubwa sana. Tunamshukuru Mhe. Rais kwa kumwondoa RC Jijini Mwanza.

Binafsi nlisikitika toka siku ya kwanza alipopelekwa Mwanza. Nikasema tumemkosea nini Rais mpaka kuamua kumleta RC Mgonjwa wa akili kama Chalamila?

Leo hii ametenguliwa naona ni jambo jema. Lakini si suala la kitaifa kama la Budget. Hili ni la muhimu sana kujadiliana namna ambavyo wanaona ni bora kuwakata wananchi kodi kwenye Simcard na Kwenye Mafuta. Na tungeangalia athari zake kiuchumi.

Baada ya siku kadhaa Chalamila atakuwa si issuee tena. Lakini suala la budget tunaweza kaa nalo Mwaka Mzima au miaka na athari zake ni kubwa sana. Tusiache kutumia akili zetu.

Wacha tudemke na chalamila
Tukimaliza mjadala wa bajeti umeisha
 
Mkuu kabla hata ya taarifa ya huyo mkuu wa mkoa kuondolewa, huo uzi wa bajeti haukuwa na mvuto. Hata huku mtaani hakuna mtu alikuwa anafuatilia kwa makini huo uchafu aliokuwa anasoma Mwigulu. Na kwa taarifa yako, hata kusingekuwa na hilo tukio la kutenguliwa, watu wengi wasingejikita kujadili hiyo bajeti ya bunge kibogoyo. Hayo ndio matatizo ya kuwa na bunge lililo kisheria, lakini bila ridhaa ya umma.
Nmekwambia kwenye ule uzi mwaingine kwamba siyo kwamba ni kwa sababu bunge ni kibogoyo.

Ila shida watz ni wengi ni wajinga! Yani ishu ya kuathiri maisha yako kwa miaka 2 ijayo unaacha inapita hivi hivi ila likija suala la Chalamila na Diamond ndio watu mmekomaa hadi mishipa inawatoka.
 
Hivi hata kama mkiijadili Budget na mkaona ina makosa au mapungufu, mkiwa kama raia wa kawaida mtafanyanini kuirekebisha hiyo budget??

Hamna uwezo wa kuikataa. Kama budget ni mbovu itapitishwa tu. Hivyo kujadili au kutokujadili hakuna maana yoyote ile.
Tukikomaa kama tunavyikomalia ishu ya Diamond na Chalamila wanaweza kubadili mawazo.

Mbona ishu ya gharama za vifurushi ilibadilishwa!
 
Leo hii ametenguliwa naona ni jambo jema. Lakini si suala la kitaifa kama la Budget. Hili ni la muhimu sana kujadiliana namna ambavyo wanaona ni bora kuwakata wananchi kodi kwenye Simcard na Kwenye Mafuta. Na tungeangalia athari zake kiuchumi.
Watanzania tuna matatizo sana
Kuna mtu alikuzuia usijadili budget?
Wewe mwenyewe umeongoza kumjadili chalamila kwa kumfungulia thread kabisa
 
Back
Top Bottom