Tume zisizo na matokeo

Nikukumbushe

JF-Expert Member
Jun 4, 2013
2,602
408
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha kumekuwepo na matukio ya utesaji,mauaji,uonevu,uumizaji wa watu,mandamano(mfano mtwara) na kero mbalimbali.
Matukio amabayo kwa namna moja ama nyingine,serikali imekuwa ikihusishwa kwa mfano kuteswa kwa Dr.Ulimboka,mauaji ya Daud mwangosi,migogoro ya ardhi n.k.
serikali imekuwa ikiunda tume au kamati maalumu kupitia vyombo vya usalama au bunge,lakini tume hizi zimekuwa hazina majibu.Tumeshuhudia tume nyingi juu ya matukio haya,lakini serikali imekuwa ikiunda tume kama sehemu ya kufichia maovu na kuzuia watu kuhoji juu ya tukio husika kwa kisingizio cha jambo liko mahakamani au tume iko inaendelea na uchunguzi.
Pamoja na uvumilivu wa wananchi,tume zimekuwa hazina majibu na kuwafanya wananchi kutokuwa na imani na serikali.
Kwa mfano uchunguzi wa tume juu ya mwangosi,kibanda na ulimboka n.k. Hakuna majibu ya kuridhisha yaliyotolewa na serikali.Kwa kuongezea tukio la ulimboka,mtu aliye kamatwa,kesi yake inasuasua.Inawezekana hili limefanyika kuziba midomo ya wanaohoji juu ya tukio hili.
Kwa hiyo serikali imekuwa ikiunda tume kwa kisingizio cha kuziba watu midomo,au kufikisha mahakamani watu fulani,na kushindwa kuendesha kesi kwa wakati juu ya tukio husika.ukihoji suala liko mahakamani.maoni yangu,nawasilisha.
 
Back
Top Bottom