Tume za jaji Nyalali na jaji Kisanda ziheshimiwe.

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,450
2,000
1. Napenda kuiomba tume hii ya jaji Warioba kwanza kuchukua na kuheshimu mapendekezo yote yahusuyo muungano wa Zanzibar na Tanganyika kama ilivopendekezwa na tume za majaji NYALALI na KISANDA.
Mie naamini kama watawala wetu wangefuata mapendekezo yaliyomo humo katika kuuboresha muungano wetu, leo hii tungekuwa tunafikiria mambo mengine tu ya kuweka katika katiba mpya. Lakini KUTOJALI na DHARAU ndio kunaponza hata wengine wafikirie kuuvunja muungano. Chonde chonde mzee Warioba!
2. Jambo jingine napendelea kwenye katiba ni kuorodhesha IDADI ya wizara na mikoa, kwa mfano wizara ziwe zile zilizomo kwenye HATI YA MUUNGANO kwa serikali ya muungano na wizara nyingine (chache) ziundwe na serikali za Zanzibar/Tanganyika.
Mikoa ipunguzwe na ama isiwe chini ya nane na isizidi kumi kwa Tanganyika, kwa Zanzibar isizidi mitatu. Hii itasaidia nchi yetu KIUCHUMI zaidi.
3. Lugha na Tamaduni zetu za ASILI ziheshimiwe. Wenzetu wamefanya hivo kwa ustawi wa jamii nzima na heshima pia.
4. Majina ya sehemu yawe ya ASILI ya pale ili kuendeleza UTAMBULISHO wetu.
Kwa haya machache nawatakia heri na BUSARA zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom