Tume yatangaza uchaguzi mdogo wa Madiwani;Sombetini Arusha ndani!

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwa uchaguzi mdogo wa kujaza viti vilivyo wazi vya madiwani katika kata 27 zilizoko katika halmashauri 23, utafanyika Februari 9, mwakani.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba, alisema jana kuwa viti hivyo vimekuwa katika kata hizo, kutokana na baadhi ya madiwani kufariki dunia na wengine kupoteza sifa.

Kata hizo na halmashauri zake kwenye mabano ni Segela na Mpwayungu (Chamwino),Ukumbi na Ibumu (Kilolo), Nduli (Iringa), Malindo (Rungwe), Santilya (Mbeya), Tungi (Morogoro), Mkwiti (Tandahimba) na Mkongolo (Kigoma).

Nyingine ni Sombetini (Arusha), Mrijo (Chemba), Magomeni na Kibindu (Bagamoyo), Mtae (Lushoto), Ubagwe (Ushetu), Namikago (Nachingwea), Partimbo na Loolera (Kiteto), Kiwalala (Lindi), Kilelema (Buhigwe), Kiomoni (Tanga), Kasanga (Kalambo), Rudewa (Kilosa), Kiborloni (Moshi), Njombe Mjini (Njombe) na Nyasura (Bunda).

Alisema uteuzi wa wagombea udiwani utafanyika Januari 15, wakati kampeni za uchaguzi zitaanza Januari 16 hadi Februari 8 na siku ya kupiga kura itakuwa Februari 9, mwakani.

Alisema zoezi la uwekaji wazi Daftari la Kudumu la Wapigakura litafanyika kuanzia Februari mosi, mwakani katika vituo walivyojiandikisha wapiga kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na kwamba, zoezi hilo litafanyika kwa siku saba.

Mallaba alisema wagombea wa udiwani watachukua fomu za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi kuanzia Januari 2 kabla ya saa 10,00 alasiri.

Alisema wagombea wanatakiwa kuwasilisha fomu za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi siku ya uteuzi katika muda muda usiozidi saa 10.00 alasiri.

Source:Nipashe
 
Naibu katibu mkuu wetu, uanaweza kushinda kata za Kigoma?
 
Yaani kilichokuwa kinasubiriwa ni dispute ya cdm, ndo watangaze!
Na hawaambulii kitu hata kata moja!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tatizo la hii tume ni kugoma kabisa kuborehsa daftari la wapiga kura, toka 2010 watu wamekufa, wamepoteza vipande, wamehama, wamehamia na wale waliokuwa na miaka 15 sasa wamefikia umri wa kupiga kura - mbona tunanyimana haki hivi hivi jamani?
 
1.overal cdm win 1.12
2.overal cdm lose 49.68
NEC--bet
chagua 1 or 2 na weka offer yako kuanzia 1000 kwa kutabiri matokeo
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom