Tume yalikana jimbo jipya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume yalikana jimbo jipya

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by chibingo, Jul 26, 2010.

 1. c

  chibingo Member

  #1
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  MKURUGENZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rajab Kiravu amesema hana taarifa za tume hiyo kutangaza jimbo jipya la uchaguzi la Ushetu mkoani Shinyanga.

  Kiravu alisema hayo wakati akizungumza na gazeti hili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam (JNIA) jana akirejea nchini kutoka Namibia.

  "Alisema kwamba jimbo halitangazwi na mtu kwa kujiamulia, na kufafanua, “Mimi sina taarifa za Tume kutangaza majimbo mapya kwa siku za karibuni kwa kuwa ndio yenye dhamana ya kufanya hivyo… ila ieleweke kuwa jimbo halitangazwi na mtu kwa kujiamulia.”

  Ufafanuzi wa Kiravu unatokana na utata uliojitokeza hivi karibuni katika Jimbo la Kahama mkoani Shinyanga, baada ya watendaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo kuwatangazia wanachama wake kuchukua fomu za kuwania ubunge Jimbo la Ushetu.

  Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Sospeter Nyigoti aliwatangazia wana-CCM siku ya mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu Julai 21, mwaka huu, kuwa amepewa taarifa na Makao Makuu kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekubali kutangaza jimbo jipya la Ushetu.

  Kutokana na hali hiyo, kuliibuka mvutano kati ya mbunge wa Kahama anayemaliza muda wake, James Lembeli na viongozi hao wa CCM, na hivyo Lembeli kuchukua fomu kuwania Jimbo la Ushetu.

  Uamuzi huo wa ‘Tume’ ambao unakanushwa na Kiravu, uliifanya Kahama iwe na majimbo mawili ya uchaguzi na hivyo kuwachanganya wagombea ambao wengi walikuwa tayari wamejaza fomu za kuomba uteuzi wa CCM kwa jimbo la sasa la Kahama.

  Kwa sasa, CCM imetoa fomu kwa wanachama 7 kuwania Jimbo la Kahama akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Khamis Mgeja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Andrew Masanje. Wagombea wengine ni Joseph Chimaguli, Charles Malimi, Luhende Pius, Deogratius Bundala na Sosthenes Malale.

  Kwa Jimbo la Ushetu lililozua utata, waliochukua fomu ni Lembeli pamoja na aliyekuwa mtangulizi wake katika Jimbo la Kahama, Raphael Mlolwa. Mwingine ni Erhard Mulyansi.

  Lakini akizungumza jana kwa simu kutoka Kahama, Katibu wa CCM Wilaya, Nyigoti alisema CCM imetoa fomu kwa kuzingatia maelekezo ya chama hicho kutoka kwa Katibu Mkuu, Yusuf Makamba “Tumefanya hivyo kwa maelekezo ya chama siyo ya serikali…tumepata maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu, na kama unavyojua Ushetu ni wilaya, ingawa haijatangazwa kuwa ni Jimbo la Uchaguzi,” alieleza katibu huyo wa wilaya.

  Ushetu ni miongoni mwa wilaya mpya 18 zilizotangazwa kuundwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete, pamoja na kuundwa kwa mikoa mipya minne ya Katavi, Simiyu, Njoluma na Geita.

  Aprili 15, mwaka huu, NEC ilitangaza kugawa majimbo saba ya sasa ya uchaguzi, ambayo ni Nkasi mkoani Rukwa; Tunduru (Ruvuma); Maswa (Shinyanga); Kasulu Mashariki (Kigoma); Bukombe (Shinyanga); Singida Kusini (Singida) na Ukonga (Dar es Salaam).

  Aidha, wakati wa kikao chake cha Juni 23, mwaka huu mjini Dodoma, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), iliamua kuwa mikoa mipya iliyoundwa hivi karibuni, itafanya uteuzi wa wagombea wa Viti Maalumu, na kazi hiyo itasimamiwa na mikoa mama ya sasa


  Wana JF
  Hivi, CCM wametoa wapi mamlaka ya kujiongezea majimbo ya uchaguzi bila ridhaa ya NEC? Kweli uchaguzi huu utakuwa wa 'huru na wa haki?
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kuna mchezo mchafu hapo wa kummaliza lembeli bila yeye kujua, later watatuambia jimbo la ushetu halipo na lembeli ndo itakuwa imekula kwake mazima.
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Nakubaliana na wewe mkuu. Lembeli ameingia kucheza ngoma asiyoijua!
   
Loading...