Tume yaahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata


U

uvivumwiko

Member
Joined
Mar 22, 2010
Messages
20
Likes
1
Points
0
U

uvivumwiko

Member
Joined Mar 22, 2010
20 1 0
Tume yaahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: KUAHIRISHA BAADHI YA CHAGUZI MBALIMBALI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa katika kikao chake cha tarehe 30/10/2010 imefanya maamuzi ya kuahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata kutokana na upungufu uliojitokeza hususan katika karatasi za kura.

Kata na Majimbo ambayo Chaguzi zake zimeahirishwa ni kama ifuatavyo:-1. Uchaguzi wa Wabunge katika majimbo ya Nkenge, Mpanda Mjini na Mpanda vijijini.Kwa upande wa anzibar (Unguja) Majimbo ya Mwanakwerekwe,Mtoni na Magogoni,na Wete (Pemba)

2. Uchaguzi wa Madiwani katika kata zifuatazo:(bofya hapa http://www.nec.go.tz/index.php?modules=news&sub&op=read&id=11)

Hata hivyo katika majimbo hayo matatu ambapo Uchaguzi wa Wabunge umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Madiwani utanaendelea kufanyika leo kama ilivyopangwa.

Vile vile, katika Kata ambazo Uchaguzi wa Madiwani umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Wabunge utaendelea kufanyika kama ilivyopangwa.

Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa tarehe za kufanyika kwa chaguzi hizo itatangazwa hapo baadaye.

(Rajabu R. Kiravu)

Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi
 

Forum statistics

Threads 1,252,142
Members 482,015
Posts 29,798,033