Tume yaahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume yaahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ally Msangi, Oct 31, 2010.

 1. Ally Msangi

  Ally Msangi Verified User

  #1
  Oct 31, 2010
  Joined: Jun 29, 2010
  Messages: 581
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  YAH: KUAHIRISHA BAADHI YA CHAGUZI MBALIMBALI

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa katika kikao chake cha tarehe 30/10/2010 imefanya maamuzi ya kuahirisha Uchaguzi katika baadhi ya Majimbo na Kata kutokana na upungufu uliojitokeza hususan katika karatasi za kura.

  Kata na Majimbo ambayo Chaguzi zake zimeahirishwa ni kama ifuatavyo:-  1. Uchaguzi wa Wabunge katika majimbo ya Nkenge, Mpanda Mjini na Mpanda vijijini.Kwa upande wa anzibar (Unguja) Majimbo ya Mwanakwerekwe,Mtoni na Magogoni,na Wete (Pemba)

  2. Uchaguzi wa Madiwani katika kata zifuatazo:-


  Na.
  HALMASHAURI
  KATA

  1
  Newala DC
  Mtonya

  2
  Mbulu DC
  Endegikot

  3
  Manyoni DC
  Kitaraka

  4
  Same DC
  Kisiwani

  5
  Kibaha DC
  Janga

  6
  Rufiji
  (a) Kibiti

  (b) Chemchem

  (c) Ngorongo

  (d) Kipugira

  (e) Mjawa

  7
  Uyui DC
  (a)KIgwa

  (b)Ibelamilundi

  8
  Sikonge
  Kisanga

  9
  Njombe
  Mji Mwema  10
  Ulanga DC
  Msogezi

  11
  Karagwe DC
  (a) Kimuli

  (b) Kamuli

  12
  Kasulu
  Kitagata

  13
  Chato DC
  Buseresere

  14
  Mwanza (Jiji)
  (a) Mkuyuni

  (b) Mirongo

  Hata hivyo katika majimbo hayo matatu ambapo Uchaguzi wa Wabunge umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Madiwani utanaendelea kufanyika leo kama ilivyopangwa.  Vile vile, katika Kata ambazo Uchaguzi wa Madiwani umeahirishwa, Uchaguzi wa Rais na Wabunge utaendelea kufanyika kama ilivyopangwa.  Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa tarehe za kufanyika kwa chaguzi hizo itatangazwa hapo baadaye.

  (Rajabu R. Kiravu)

  Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi
   
 2. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  hivi kiravu mbona ni bogas sana?
   
 3. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndo utabiri wa Chizi Yahya huo wakuuuuuuuuuuuu.....utabiri uchwara kabisa.
   
 4. Ally Msangi

  Ally Msangi Verified User

  #4
  Oct 31, 2010
  Joined: Jun 29, 2010
  Messages: 581
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  kiravu kwani ana akili si ana waskiza ma boss wake wa ccm
   
Loading...