Tume ya Wilson Mkama ndio ilianzisha "chokochoko" kwa JamiiForums baada ya Uchaguzi 2010

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,816
Baada ya "Chokochoko" ya 2008 ya kuhama toka JamboForums mpaka JamiiForums.Mtandao huu ulikuwa machoni pa watawala na wote wenye mamlaka.Hakuna mwanasiasa wa chama kilichokuwa madarakani angependa uendelee kama ulivyo ktk harakati za uchaguzi wa 2010.Walitishika,waliuogopa na walihamaki...

Wale "wanunuzi" wa Wahariri wa Magazeti na vyombo vingine vya mawasiliano waliumiza kichwa juu ya JF kuelekea 2010,wangetamani "wainunue" iwe upande wao lakini "haikununulika".Hii ilikuwa ni vita ya ndani kwa ndani.Walisumbuka,walihangaika na wakajibiidisha bila mafanikio.

Vyombo vingi vya habari vilichagua "upande",humu ndani kukabaki "Neutral".Watu walijimwaga na kuelezea hisia zao na kile wanachokiamini.Hatimaye October 2010 ikawadia,wakatikiswa na kutikisika.Hawakumini yaliyotokea,yaliyomo yamo na ambayo hayakuwamo yakawemo.Wakastuka,wakatafakari na kuunda tume ya kufanya tathmini ya Uchaguzi wa 2010.Wakajiuliza,kwanini tumeshindwa na kudondoka kuliko ilivyokuwa 2005?

Tume ya Chama Kikuu ya kufanya tathmini ya kupungua kwa kura za mwaka 2010 ikilinganishwa na 2005 iliwekwa chini ya Ndugu Wilson Mkama.Mkama alipewa kazi ya kuangalia na kuchunguza sababu zilizofanya kura za chama chake kupungua kwa asilimia nyingi toka mwaka 2005 hadi 2010.Na majibu pamoja na mapendekezo yake ndio yatachukuliwa kama "dira" ya kuelekea 2015.

Mambo makubwa mawili yalitawala ripoti ile;kwanza ilikuwa ni mtandao wa Jamii Forum na pili ikawa kashfa ya Ufisadi kwa baadhi ya makada wa Chama tawala.

Tume ile ilikuja na suala la "Jamii Forum";kwamba kura nyingi za chama zimepungua sababu upinzani umewekeza sana kwa vijana kwa njia ya mitandao na hasa JF,kiasi kuwa habari nyingi na "publicity" ya upinzani inapata nafasi kubwa kuliko chama tawala.Vijana wengi ambao ni watumiaji wa mitandao wanashawishika na upinzani na kupata habari chanya za upinzani na hasi za chama tawala kupitia JF.

Wakati huo ndani ya JF kulikuwa na "verified member" wenye "profile" kubwa ktk vyama vyao kama Dr Slaa,Zitto Kabwe,Freeman Mbowe,Prof Kitila Mkumbo na John John Mnyika.Hawa walitoa maandiko,ufafanuzi na mijadala mikali juu ya chama chao na kujipambanua.

Dr Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA alijibu maswali na kuahiriki mijadala,Zitto Kabwe alitoa mada na kujadili kwa mapana;JJ Mnyika hakuwa mbali na jukwaa hili,wote walipatikana hapa na kuupa upinzani nguvu za "siasa za mitandaoni".Hili lilikuwa ni "tishio" la Chama Tawala na kuifanya JF kuwa moja ya ajenda ktk tathmini yao ya kupungua kwa kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge 2010.

Siasa za mtandao ziliibeba Chadema,makada wake ni miongoni mwa member wengi waliotaradadi JF kwa hoja na mantiki.Ukawa mpambano wa ulimwengu mpya wa digitari na analojia.Hapa ndipo JF ilipotazamwa kama sehemu nyingine yenye ushawishi katika siasa za vyama vingi za Tanzania.

Maazimio ya Tume ya Mkama ilikuwa na wao kama chama kikubwa kuingia kwenye mitandao na kundesha "E-Politics".Watafutwe vijana makada watakaokuwa na wajibu wa kukisemea chama mitandaoni na hasa JF.

Vijana hawa wawezeshwe na vifaa na muda wa "bundle".Na hapa ndipo lilipoasisiwa jina la "JF Buku 7" toka Lumumba.Kwanini waliitwa "buku saba?";sababu walikuwa na bajeti ya shilingi elfu moja kwa siku kwa ajili ya bundle ambayo buku saba kwa juma.Huko Ufipa nako vijana hawakulala,hapa ndipo mnyukano wa kiitikadi ulipoanzia,na upande unaonekana kuelemewa ndio huo unaotaka kutia mpira kwapani.Sasa huwezi kuweka mpira kwapani kwa kuiadhibu JF.

Haikuwa siri tena,kuwa moja ya maazimio yale ya Mkama,yalifanya sasa JF kuwa sehemu ya "mvurugano" wa pande mbili za itikadi tofauti.Na baada ya Ripoti ya Tume ile,hatimaye April 2011,Ndugu Wilson Mkama akapewa Ukatibu Mkuu wa CCM ili kuhakikisha zile sababu zilizopunguza kura za 2010 zinafanyiwa ufumbuzi.Hizi zilizkuwa ni "E-Politics" na "Vua gamba".

Buku saba na Vua gamba zikawa ndio ajenda;Nape akishadadia watu wajivue magamba kwa tuhuma za ufisadi.Hapa waliandamwa watu kama Lowassa na wale wa aina yake.Hali hii ikamfanya Mbunge wa Igunga wakati huo kuachia ngazi.Hii ndio ilikuwa kazi ya Wilson Mkama mara baada ya ripoti yake na yeye kupewa nafasi ya Ukatibu Mkuu.

Hapa ndio moto wa kuifuatilia JF kwa ajili ya ushawishi wake wa "E-Politics" ukashika hatamu.Habari motomoto na mijadala iliyosababisha serikali na chama kubabaika.Kashfa nyingi zilianzia hapa,na mambo mengi yaliyoshindakana huko,hapa yaliwezekana.JF ikawa kwenye jicho la "wakubwa" wakiwa na hofu na taharuki.

Wengine walivumilia mpaka wakatoka madarakani;japo walijitahidi kuizima na kuipoteza.Wengine walioingia tu;wakaomba malaika wao waje "waizime" mitandao.Inawezekana ilichukuliwa kama ni kauli ya "kuchomekea",lkn hakika ilitoka moyoni.

Tumesikia tena kauli nyingine,kwamba kama watu wanataka kufanya mkutano sehemu ya jumba jeupe,basi ajenda zao inabidi zihakikiwe na kuidhinishwa.Hili nalo linaweza bebwa juu juu na kupita,lkn usishangae baadae tukaambiwa vyama fulani kabla ya kuitisha vikao vyao,basi ajenda za mikutano yao inabidi zichunguzwe.Tunaweza kufika huko...na haitakuwa ajabu,sababu haya tu yanatokea yameshakuwa na ajabu.
 
Hata wakiifunga itaanzishwa ingine ambapo wata host nje nchi tuone wataenda wapi kuwaamata!! Dunia ya cloud computing mnaenda kuvamia ofisi na kuchukua ma computer eti mmekamata data zote!! Hao malaika washuke tu lakini kukosolewa lazima akosolewe yeye Mungu? Hata Mungu anakosolewa!
 
Ni hapa JF ambapo kwa mara ya kwanza sera za serikali ya awamu ya tano zinakosolewa kwa hoja nzito kiasi wanashindwa hata kuzijibu!

magazeti na Tv stations,kwa woga,walibaki wanashangilia kila wanachoambiwa
 
Ni wakati wa upinzani kuwa na mikakati mipyaa.

Ni wakati wa upinzani kujiandaa kisaijolojia kuwa, hali ya kisiasa imebadilika na wao wanapaswa kubadilikaa.

Haya yanayo tokea yataleta matokeo hasi mbeleni.
Watanzania tumekaa kimya kwa uoga tukishuhudia hayaa.
Na haya yote yanafichwa kwa kichaka cha kuwa eti anapambana na ufisadi na kuleta maendeleo.

Siasa yetu inaelekea pabaya.
 
Jf inalindwa na Malaika wenye nguvu kuliko kawaida...
Haizimwi ng'o!
 
Wanaota mapembe
Waongezee mkia
Na ukinibeep tu nakupigia
Let me make one thing clear
Bla bla sitaki kusikia .......

Maisha na muziki
Wacha maneno weka muzikii ......
Uwiiiiiiii

Tutafanyaje sasa wacha tuimbe muziki tu maana ukisema wale Mamba wa mto Ruvu watazidi kunenepa
Au upewe kisa kama cha Faru John cha kupenda mademu then ulambwe shaba
 
Duuh!!sasa nimeelewa!!Huyu ndio barafu wa JF
Kweli wanaotaka kuisakama JF watatukosesha mengi,hasa watu kama huyu jamaa


Mkuu Huyu Jamaa huwa namwelewa sana ingaweje kuna wakati sikukubaliana naye hasa hasa kile kipindi cha ununuzi wa bombardier.

Kuna siku nilimuuliza barafu ni mtu mmoja au ni kikundi cha watu wenye mtizamo na maono yanayofanana...hakunijibu ila naye aliniuliza swali

Kweli Kabisa jf ikizimwa tutakosa sana threads za huyu bwana..
 
Kuna tofauti ya kuwa kiongozi na mtawala na siku zote mtu dhaifu hapendi kukosolewa au kushauriwa kwa hofu ya madhaifu yake kuwekwa bayana.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom