Tume ya Wilson Mkama ndio ilianzisha "chokochoko" kwa JamiiForums baada ya Uchaguzi 2010

Upinzani, Vyombo vya Habari na Mitandao ya kijamii ndio vitu vinavyolichangamsha Taifa na lionekane lina UHAI.

Hivi vikipigwa ban basi Taifa litakuwa Kimya.
 
Mkuu Huyu Jamaa huwa namwelewa sana ingaweje kuna wakati sikukubaliana naye hasa hasa kile kipindi cha ununuzi wa bombardier.

Kuna siku nilimuuliza barafu ni mtu mmoja au ni kikundi cha watu wenye mtizamo na maono yanayofanana...hakunijibu ila naye aliniuliza swami.

Kweli Kabisa jf ikizimwa tutakosa sana threads za huyu bwana..
Mkuu hii namba nafikiri nijikampuni,maana mambo ya kanisa twende,huko kwenye bombadia ndi balaa,siasa ni kama alikuwepo sijui toka ujana wa Nyerere...Huko jukwaa la mapenzi ndio usiseme!!Sielewi ha ha ha ah ah
 
Giza nene! Mungu pekee ndiye unayejua wapi huu utawala inatupeleka
 
Mkuu barafu nimekuelewa sana kiongozi lakini mimi sidhani kama ni siasa pekee inayopelekea JF kupata misukosuko hii lipo jambo ambalo ni zaidi ya siasa na kama ingekuwa ni mambo ya siasa pekee leo JF ingekuwa imeshafungwa toka 2010 baada tu ya uchaguzi na kama unavyosema utafiti uliofanywa na Wilson mukama hakuna kipindi kigumu ambacho CCM imepitia toka kuanzishwa kwake kama uchaguzi wa 2015 na ambao kama chama tawala kingefanya vyovyote kujiokoa lakini JF ilibaki na pia tunatakiwa kujua kuwa hakuna chombo kinachoheshimika kama JF na habari zake zimekuwa ni vyanzo vya habari vya media house nyingne nying sema wamekosa uungwana wa kutambua uwepo wa JF kama chanzo makini cha habari yao. JF ndipo sehemu pekee ambapo viongozi na wanasiasa wana account hapa tena zingne ni verified accounts hii ni heshima kubwa sana kwa social forum ya hapa nyumbani tofauti na FB na twitter za nje

Kinachosumbua kwa sasa ni kujaa kwa taarifa za uongo hapa JF na hili ndo tatizo kubwa na hatari kwa uhai wa JF tena tumeshindwa kujua JF ni chombo kinachofatiliwa na kuheshimiwa na watu kuna watu hawasomi wala kuangalia TV au redio wanatumia JF kama chombo chao cha habari sasa kunapokuwa na taarifa za upotoshaji na uchochezi inakuwaje hapo??? Si mala moja kuja kwa taarifa za uongo hapa na si mala ya kwanza kuja kwa mpaka taarifa fake ya kurugenzi ya ikulu mfano ni ile barua ya kutumbuliwa kwa mkuu wa mkoa wa arusha ambayo inasemkana barua ile ilianzia hapa na kusambaa kwingine
pia tunatakiwa kujua watu wenye nia mbaya wanaitumia JF kupitishia uzushi wao kwa kujua JF ina nguvu kubwa na kuaminiwa na watu wa rika na kada tofauti na kutembelewa na watu wengi watu milion 2 ndio wanaitembelea JF kwa mwezi wakipata taarifa mbalimbali hapa JF

Duniani hakuna serikali yeyote itakayo acha taasisi au chombo chenye kuweza kuleta taarifa za kutibua amani au kuleta sintofahamu ndani ya nchi dunian bajet kubwa inakwenda kwenye ulinzi na usalama na usalama ni pamoja na kuhakiksha wananchi wanapata taarifa sahihi si za upotoshaji au uchochezi na imegundulika vyanzo vikuu vya kuleta matatizo ndani ya nchi ni vyombo vya habari mfano Rwanda na Kenya mpaka waandish wa habari nao walikuwa washitakiwa ktk mahakamani wengine mpaka ICC kwani wanasema information is power. Giving people the knowledge to understand

Kuna malalamiko ya member wenzetu wakilalamika kushuka kwa heshima ya JF leo JF ya 2010 si ya 2016 na ni ukweli usiofichika JF kuwekuwa kama genge badala ya jukwaa la GT watu wenye weledi wamekuwa wakipungua siku baada ya siku leo hata wale vyenye verified acc wamekuwa wakipungua na kuacha kuchangia au kupost kitu tofauti na zaman kwa sababu mtu wenye VA awezi kuleta habari ya uongo hapa lakini sisi wenye fake Id tunaleta na kusema chochote hata bila kujua au kpima kitu hiki kina madhala gani kwa Taifa au wananchi

Ushauri wangu kwa Max na wengne wanaohusika na JF waangalie mfumo na madhumuni ya kuanzisha JF ni yapi na je yanafatwa ?? Duniani hakuna taasisi au mtu aliyeweza kushindana na serikali na kushinda hakuna. Wanasiasa dunian wananguvu sana kuliko hata makomando au majenerali wa kijeshi neno moja tu la mwanasiasa linaweza kuleta amani au vita leo majenerali wa jeshi wanawapigia salute wanasiasa ambao hata mgambo awajapitia na maana ya salute ni heshima na utii kwa yule unayempigia hyo salute mm sipendi kuona siku JF ikiwa off kwa sababu ya watu wachache tena kwa masilai yao
 
Baada ya "Chokochoko" ya 2008 ya kuhama toka JamboForums mpaka JamiiForums.Mtandao huu ulikuwa machoni pa watawala na wote wenye mamlaka.Hakuna mwanasiasa wa chama kilichokuwa madarakani angependa uendelee kama ulivyo ktk harakati za uchaguzi wa 2010.Walitishika,waliuogopa na walihamaki...

Wale "wanunuzi" wa Wahariri wa Magazeti na vyombo vingine vya mawasiliano waliumiza kichwa juu ya JF kuelekea 2010,wangetamani "wainunue" iwe upande wao lakini "haikununulika".Hii ilikuwa ni vita ya ndani kwa ndani.Walisumbuka,walihangaika na wakajibiidisha bila mafanikio.

Vyombo vingi vya habari vilichagua "upande",humu ndani kukabaki "Neutral".Watu walijimwaga na kuelezea hisia zao na kile wanachokiamini.Hatimaye October 2010 ikawadia,wakatikiswa na kutikisika.Hawakumini yaliyotokea,yaliyomo yamo na ambayo hayakuwamo yakawemo.Wakastuka,wakatafakari na kuunda tume ya kufanya tathmini ya Uchaguzi wa 2010.Wakajiuliza,kwanini tumeshindwa na kudondoka kuliko ilivyokuwa 2005?

Tume ya Chama Kikuu ya kufanya tathmini ya kupungua kwa kura za mwaka 2010 ikilinganishwa na 2005 iliwekwa chini ya Ndugu Wilson Mkama.Mkama alipewa kazi ya kuangalia na kuchunguza sababu zilizofanya kura za chama chake kupungua kwa asilimia nyingi toka mwaka 2005 hadi 2010.Na majibu pamoja na mapendekezo yake ndio yatachukuliwa kama "dira" ya kuelekea 2015.

Mambo makubwa mawili yalitawala ripoti ile;kwanza ilikuwa ni mtandao wa Jamii Forum na pili ikawa kashfa ya Ufisadi kwa baadhi ya makada wa Chama tawala.

Tume ile ilikuja na suala la "Jamii Forum";kwamba kura nyingi za chama zimepungua sababu upinzani umewekeza sana kwa vijana kwa njia ya mitandao na hasa JF,kiasi kuwa habari nyingi na "publicity" ya upinzani inapata nafasi kubwa kuliko chama tawala.Vijana wengi ambao ni watumiaji wa mitandao wanashawishika na upinzani na kupata habari chanya za upinzani na hasi za chama tawala kupitia JF.

Wakati huo ndani ya JF kulikuwa na "verified member" wenye "profile" kubwa ktk vyama vyao kama Dr Slaa,Zitto Kabwe,Freeman Mbowe,Prof Kitila Mkumbo na John John Mnyika.Hawa walitoa maandiko,ufafanuzi na mijadala mikali juu ya chama chao na kujipambanua.

Dr Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA alijibu maswali na kuahiriki mijadala,Zitto Kabwe alitoa mada na kujadili kwa mapana;JJ Mnyika hakuwa mbali na jukwaa hili,wote walipatikana hapa na kuupa upinzani nguvu za "siasa za mitandaoni".Hili lilikuwa ni "tishio" la Chama Tawala na kuifanya JF kuwa moja ya ajenda ktk tathmini yao ya kupungua kwa kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge 2010.

Siasa za mtandao ziliibeba Chadema,makada wake ni miongoni mwa member wengi waliotaradadi JF kwa hoja na mantiki.Ukawa mpambano wa ulimwengu mpya wa digitari na analojia.Hapa ndipo JF ilipotazamwa kama sehemu nyingine yenye ushawishi katika siasa za vyama vingi za Tanzania.

Maazimio ya Tume ya Mkama ilikuwa na wao kama chama kikubwa kuingia kwenye mitandao na kundesha "E-Politics".Watafutwe vijana makada watakaokuwa na wajibu wa kukisemea chama mitandaoni na hasa JF.

Vijana hawa wawezeshwe na vifaa na muda wa "bundle".Na hapa ndipo lilipoasisiwa jina la "JF Buku 7" toka Lumumba.Kwanini waliitwa "buku saba?";sababu walikuwa na bajeti ya shilingi elfu moja kwa siku kwa ajili ya bundle ambayo buku saba kwa juma.Huko Ufipa nako vijana hawakulala,hapa ndipo mnyukano wa kiitikadi ulipoanzia,na upande unaonekana kuelemewa ndio huo unaotaka kutia mpira kwapani.Sasa huwezi kuweka mpira kwapani kwa kuiadhibu JF.

Haikuwa siri tena,kuwa moja ya maazimio yale ya Mkama,yalifanya sasa JF kuwa sehemu ya "mvurugano" wa pande mbili za itikadi tofauti.Na baada ya Ripoti ya Tume ile,hatimaye April 2011,Ndugu Wilson Mkama akapewa Ukatibu Mkuu wa CCM ili kuhakikisha zile sababu zilizopunguza kura za 2010 zinafanyiwa ufumbuzi.Hizi zilizkuwa ni "E-Politics" na "Vua gamba".

Buku saba na Vua gamba zikawa ndio ajenda;Nape akishadadia watu wajivue magamba kwa tuhuma za ufisadi.Hapa waliandamwa watu kama Lowassa na wale wa aina yake.Hali hii ikamfanya Mbunge wa Igunga wakati huo kuachia ngazi.Hii ndio ilikuwa kazi ya Wilson Mkama mara baada ya ripoti yake na yeye kupewa nafasi ya Ukatibu Mkuu.

Hapa ndio moto wa kuifuatilia JF kwa ajili ya ushawishi wake wa "E-Politics" ukashika hatamu.Habari motomoto na mijadala iliyosababisha serikali na chama kubabaika.Kashfa nyingi zilianzia hapa,na mambo mengi yaliyoshindakana huko,hapa yaliwezekana.JF ikawa kwenye jicho la "wakubwa" wakiwa na hofu na taharuki.

Wengine walivumilia mpaka wakatoka madarakani;japo walijitahidi kuizima na kuipoteza.Wengine walioingia tu;wakaomba malaika wao waje "waizime" mitandao.Inawezekana ilichukuliwa kama ni kauli ya "kuchomekea",lkn hakika ilitoka moyoni.

Tumesikia tena kauli nyingine,kwamba kama watu wanataka kufanya mkutano sehemu ya jumba jeupe,basi ajenda zao inabidi zihakikiwe na kuidhinishwa.Hili nalo linaweza bebwa juu juu na kupita,lkn usishangae baadae tukaambiwa vyama fulani kabla ya kuitisha vikao vyao,basi ajenda za mikutano yao inabidi zichunguzwe.Tunaweza kufika huko...na haitakuwa ajabu,sababu haya tu yanatokea yameshakuwa na ajabu.

Paragraph ya mwisho imeniogopesha sana kwenye huo mwelekeo, duh
 
Mkuu barafu nimekuelewa sana kiongozi lakini mimi sidhani kama ni siasa pekee inayopelekea JF kupata misukosuko hii lipo jambo ambalo ni zaidi ya siasa na kama ingekuwa ni mambo ya siasa pekee leo JF ingekuwa imeshafungwa toka 2010 baada tu ya uchaguzi na kama unavyosema utafiti uliofanywa na Wilson mukama hatuna kipindi kigumu ambacho CCM imepitia kama uchaguzi wa 2015 na ambao chama kingefanya vyovyote kujiokoa lakini JF ilibaki na pia tunatakiwa kujua kuwa hakuna chombo kinachoheshimika kama JF na habari zake zimekuwa ni vyanzo vya habari vya media house nyingne nying sema wamekosa uungwana wa kutambua uwepo wa JF kama chanzo makini cha habari yao JF ndipo sehemu pekee ambapo viongozi na wanasiasa wana account hapa tena zingne ni verified accounts hii ni heshima kubwa sana kwa social forum ya hapa nyumbani tofauti na FB na twitter za nje

Kinachosumbua kwa sasa ni kujaa kwa taarifa za uongo hapa JF na hili ndo tatizo kubwa na hatari kwa uhai wa JF tena tumeshindwa kujua JF ni chombo kinachofatiliwa na kuheshimiwa na watu kuna watu awasomi wala kuangalia TV au redio wanatumia JF kama chombo chao cha habari sasa kunapokuwa na taarifa za upotoshaji na uchochezi inakuwaje hapo??? si mala moja kuja kwa taarifa za uongo hapa na si mala ya kwanza kuja kwa mpaka taarifa fake ya kurugenzi ya ikulu hapa mfano ni ile barua ya kutumbuliwa wa mkuu wa mkoa wa arusha ambayo inasemkana ilianzia hapa na kusambaa kwingine

Duniani hakuna serikali yeyote itakayo acha taasisi au chombo chenye kuweza kuleta taarifa za kutibua amani au kuleta sintofahamu ndani ya nchi dunian bajet kubwa inakwenda kwenye ulinzi na usalama na usalama ni pamoja na kuhakiksha wananchi wanapata taarifa sahihi si za upotoshaji au uchochezi na imegundulika vyanzo vikuu vya kuleta matatizo ndani ya nchi ni vyombo vya habari mfano Rwanda na Kenya mpaka waandish wa habari nao walikuwa washitakiwa ktk mahakama

Kuna malalamiko ya member wenzetu wakilalamika kushuka kwa heshima ya JF leo JF ya 2010 si ya 2016 na ni ukweli usiofichika JF kuwekuwa kama genge badala ya jukwaa la GT watu wenye weledi wamekuwa wakipungua siku baada ya siku leo hata wale vyenye verified acc wamekuwa wakipungua na kuacha kuchangia au kupost kitu tofauti na zaman kwa sababu mtu wenye VA awezi kuleta habari ya uongo hapa lakini sisi wenye fake Id tunaleta na kusema chochote hata bila kujua au kpima kitu hiki kina madhala gani kwa Taifa au wananchi

Ushauri wangu kwa Max na wengne wanaohusika na JF waangalie mfumo na madhumuni ya kuanzisha JF ni yapi na je yanafatwa ?? Duniani hakuna taasisi au mtu aliyeweza kushindana na serikali na kushinda hakuna. Wanasiasa dunian wananguvu sana kuliko hata makomando au majenerali wa kijeshi neno moja tu la mwanasiasa linaweza kuleta amani au vita leo majenerali wa jeshi wanawapigia salute wanasiasa ambao hata mgambo awajapitia na maana ya salute ni heshima na utii kwa yule unayempigia hyo salute mm sipendi kuona siku JF ikiwa off kwa sababu ya watu wachache tena kwa masilai yao
mkuu umeongea point flaniflani kwenye bandiko lako.
 
Hata wakiifunga itaanzishwa ingine ambapo wata host nje nchi tuone wataenda wapi kuwaamata!! Dunia ya cloud computing mnaenda kuvamia ofisi na kuchukua ma computer eti mmekamata data zote!! Hao malaika washuke tu lakini kukosolewa lazima akosolewe yeye Mungu? Hata Mungu anakosolewa![/QUOTE
Hayo yote uliyoandika tupo pamoja. (Lakini) UNAAMINI UNAWEZA KUMKOSOA MUNGU ALIYEKUUMBA?. HAPANA UMEENDA MBALI. KIONGOZI YEYOTE ANAKOSOLEWA LAKINI SIO MUNGU. Lets go my brother.
 
Kulikuwa na enzi ambazo Invisible alikuwa anapiga ban wote walioanzisha uzushi na kutoa lugha ya matusi,siku hizi JF imekuwa uzushi mwingi sana unaanzishwa hapa.Kuna haja ya sisi members kubadilika kwani sisi ndio tunawaponza kina Maxi
 
Yule malaika wa JPM alikuwa aje kuzima lakini bahati nzuri tumemlipua
na sasa wametuma malaika wengine wameenda kumdhuru msimamizi wa familia hawajui hata sisi pia tunao malaika
 
Yule malaika wa JPM alikuwa aje kuzima lakini bahati nzuri tumemlipua
na sasa wametuma malaika wengine wameenda kumdhuru msimamizi wa familia hawajui hata sisi pia tunao malaika
Atakuwa kagoma huyo Malaika waliomtuma
 
JF ni sehemu ambayo hata hao watawala wanaitumia kutumbuana kwasababu huwezi jua ni nani hasa ameandika hiyo habari.

Inawezekana huyo barafu yupo ndani ya CCM.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom