Tume ya Warioba kutofanya kazi yake Zanzibar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya Warioba kutofanya kazi yake Zanzibar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Khakha, May 22, 2012.

 1. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  wadau JF,
  Nimesoma gazeti la citizen leo kuwa kumbe ile sheria iliyounda tume ya warioba haiwezi kufanya kazi znz hadi ipitishwe na baraza la wawakilishi. hii inafuatia masharti ya ibara ya 132 ya katiba ya znz ya 1984. werema na othman wamesema itakuwa tabled kwenye baraza la june halafu ndo shein aisaini kutumika znz. kwa hiyo warioba hawezi kwenda znz kukusanya maoni hadi ipite.
  jusa kaongezea kuwa isipopitishwa na wajumbe wa baraza ina maana kuwa warioba, automatically hataenda znz kukusanya maoni.
  wadau hii imekaaje? hivi toka mwanzo hili sharti halikulikana hadi tume inaanza kazi yake?
   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Zanzibar wana katiba yao, kwa nini na sisi watanganyika tusikusanye maoni ya kuunda katiba ya tanganyika? Kwa mantiki hii ina maana wazanzibar wakikataa tutaendelea kuishi na hii katiba mbovu milele. Wazanzibar wanatuchagulia jinsi ya kuishi katika nchi yetu wakati sisi huo uwezo hatuna kuwachagulia maisha yao.
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Tulijua itatokea ndo maana tusisitiza Tanganyika iko mbioni kuzaliwa kwa mara ya pili.Werema ni bomu kwa Tanzania hasomi, bora Mnyika ashike nafasi ya AG kwa muda, vinginevyo huyu **** atupeleka polini wajameni
   
 4. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Huo ni wakati muafaka wa kuunda Katiba ya Tanganyika.Zanzibar haitapita kirahisi Sheria hiyo...
   
 5. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Mimi nadhani waheshimiwa wasifanye mzaha, katiba wanayodhani haitapatikana hiyo 2014. Suala la muungano ni lazima liamuliwe kwanza. Katiba tunayoitaka ni ya Tanganyika period.
   
 6. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Asanteni wazanzibari kwa kuonyesha ujirani mwema ama kweli fimbo ya mbali haiuwi nyoka, safari hii ulaya hawatasaidia ni wazanzibar wataokoa jahazi.Tunaomba wazanzibar mkatae kabisa na sisi tutawalipa fadhira kwa kutowafukuza wapemba Tanganyika na mtaingia Tanganyika bila PASSPORT.Go zanzibar go, go wawakilishio go JUSSA MAALIMU SEIF GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
   
 7. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nawahurumia sana mnaodhani kuwa chini ya ccm hii tutapata katiba nzuri kwa faida ya taifa hili. Serikali yenyewe imejaa vilaza ambao kipaumbele chao ni matumbo yao na chama chao...
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa bahati mbaya sana Muunguano hauruhusiwi kujadiliwa ndani ya majadiliano yaliyoanzishwa isipookuwa kujadili jinsi ya kuuimarisha. Wakati wengi wanatana uimarishwe kwa kuurekebisha, watawala wanadhani kuzungumzia kuurekebisha kunalenga kuua.
   
 9. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Mi nashauri tusitishe zoezi la kuunda katiba tukomboe kwanza nchi toka mikononi mwa mkoloni mweusi ccm
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,315
  Trophy Points: 280
  Huu ndio huo tunaouita ukilaza wa sheria kuanzia kwa mwanasheria wetu mkuu mpaka chini!. Hawamshauri vizuri rais!.

  Mpaka kesho mimi bado nalia na mawaziri ambao ni wabunge wateule!. Katiba ilipotamka rais atateua mawaziri miongoni mwa wabunge ilimaanisha ubunge ndio pre requisite ya uwaziri!. Katiba haikumaaisha wabunge wateule!.

  Sasa kitakachofuata kule Zanzibar, sheria hiyo ya tume ya kukusanya maoni haitapitishwa kwanza mpaka itakapowekwa kipengele cha Wazanzibar kutoa maoni kuhusu muungano na kwenye hili, CUF na CCM Zanzibar lao ni moja na watakuwa wamoja kama kwenye suala la mafuta!.
   
 11. norbit

  norbit JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 496
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  usiwe na wasisi mkuuu b4 2015 kitaeleweka tu, ccm ndio inafikia ukingoni tunachotakiwa wa-tangayinga tuache unazi wa uchama na tuilimishane bila ya jazba kwani ccm wanatumilia mwanya huu wa kutugawgawa, kidini, kikabila sasa wanajaribu kijeografia (hawa wanatoka mikoa ya kusini sijui mashariki ... haya tu. tuwe makini tutachukua tangayika yetu na katiba yetu very soon. hio tume yao ya katiba watatafuta kwa kuipelaka

   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  May 22, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mbona kila kukicha kunakuwa na mikanganyiko ya kisheria hapa nchini? Kama ni hivyo ilikuwaje wakamshauri Rais ateue Kamati kabla ya kuipitisha hiyo sheria? Ilikuwaje wajumbe wa tume toka Zanzibar wakateuliwa na kuapishwa wakati hiyo sheria ya kuwateua haijapitishwa huko kwao?

  Mikanganyiko mingine wala haikutakiwa kuwepo kama kuna wataalam makini wa sheria. Sheria ingepitishwa JMT na ikaenda SMZ ikapitishwa na kusainiwa kisha basi Rais akateua hao wajumbe na kuwaapisha kuliko hiki kilichofanyika.
   
 13. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Huo ndio uzalendo unatakiwa watanganyike muonyeshe sio kuungana kuwatoa kina Ngeleja & cos, watanganyika kwa umoja wetu tuungane kudai tanganyika kwa wakati huu kwa kusaidiwa na kiburi cha wazanzibari
   
 14. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Watanganyika na wazanzibari tuwe kitu kimoja kusambaratisha Tanzania.kila kila nchi na zake pambafuuuuu ccm
   
 15. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Haya maibara haya hatufiki mbali lazima tubadilike
   
 16. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  tatizo baya ni kwamba kiongozi anachagua watu huku akisema "sitaki kusikia swala la muuungano"kwa hio hata kama unataka kumshauri kuwa muzee hili haliwezekani kwa sababu hii na ile.yeye hataki ushauri huo,eti ndo kulinda muungano-sijui ni lini huu muungano wa kiajabu ajabu utakufa nifanye mambo yangu kwa amani
   
 17. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Tunashukuru kwa kuwa na Rais asiye makini na mwanasheria mkuu asiye makini hawa ndiyo watasaidia sana kurahisisha M4C ifikiwe mapema kuliko matarajio ya wengi.Hili la Zanzibar limenipa faraja kwani sasa tumepata njia ya kuwahi.Go wazanzibari
   
 18. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  mkuu kimbunga
  werema na othman wanatumia precedent ya maamuzi ya mahakama ya rufaa kwenye kesi ya maalim seif ya mwaka 1992 ili kujustify kwamba jambo likishajadiliwa na bunge la muungano basi linakuwa valid pande zote za muungano. nadhani walijisahau kuwa kuna sheria katibani znz inayoeleza jinsi ya kuziingiza sheria zilizotungwa na bunge la muungano.
  naona baraza la wawakilishi mwezi june litakuwa tamu sana. nauliza tena hivi wabobezi wa sheria serikalini hawakuliona hilo mapema?
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndo hivyo mpaka rais wanatuchagulia!
   
 20. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mi sijui sheria lakini sidhani kama tume haiwezi kukusanya maoni kule,kwani hii ni katiba ya muungano na automatic hii ni swala la muungano.sheria ya kuunda tume na kuruhusu ikusanye maoni ilitungwa na watanzania wote zanzibar wakiwemo kupitia wabunge
   
Loading...