Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu Syria yasema bado hakuna usalama Syria

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Syria imetowa ripoti yake hii leo inayosema kwamba hali bado sio salama nchini Syria kwa wakimbizi kurudi,ikiwa ni muongo mmoja tangu ulipozuka mzozo nchini humo.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhalifu uliofanyika Syria wameorodhesha matukio ya vurugu mbaya na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na vikosi vya wanajeshi wa serikali ya Syria, ikiwemo watu kufungwa bila hatia.

Tume hiyo ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imesema kwa ujumla hali inazidi kuwa mbaya,ikitaja mapigano katika maeneo mengi ya nchi hiyo iliyoporomoka,pamoja na hali ngumu ya kiuchumi, na ongezeko la mashambulio ya wanamgambo wa kundi linalojiita dola la kiislamu.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imetolewa katika wakati ambapo rais Bashar al Assad jana alikutana na mwenyeji wake mjini Moscow rais Vladmir Putin na kujadiliana kuhusu ushirikiano wa wanajeshi wao na njia ya kuendeleza operesheni ya kuwania kudhibiti ngome za mwisho zinazoshikiliwa na waasi nchini Syria
 
Wazungu umbwa sanaaa,
Wameenda kuchafua inchi ya watu halafu haoooo wamekimbiaaaa, eti wanajidai kuonea huruma
 
Back
Top Bottom