Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) chini ya Uenyekiti wa Jecha Salim Jecha imetangaza kuwa mchakato wa kuelekea kwenye uchaguzi wa marudio wa March 20, 2016 unaendelea kwa mafanikio.
Katika taarifa waliyoisambaza leo, ZEC imedai kuwa kulikuwa na kasoro ya jina la mgombea wa Urais wa Chama Cha ADA - TADEA katika karatasi ya kupigia kura ingawa kasoro hiyo imesharekebishwa.
Wamewataka watanzania na hasa wazanzibar kuwa watulivu na kuliombea Taifa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi na pia wamewahakikishia wananchi kuwa uchaguzi utakuwa huru, wa haki na uwazi.
Kumekucha Zanzibar..!!