Tume ya Uchaguzi yatoa Ufafanuzi kuhusu wabunge wa CUF walioteuliwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefafanua juu ya uteuzi wa wabunge wapya wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF).

Imesema kuwa imesikitishwa na kushangazwa na taarifa za Baraza Kuu la Taifa la chama hicho kwamba tume hiyo imekiuka kanuni zake katika uteuzi wa wabunge wanane wa chama hicho ili kujaza nafasi za wazi zilizotokea hivi karibuni. Maazimio ya baraza kuu la uongozi la Taifa la CUF kuhusiana na hujuma za dola dhidi ya chama

Aidha, imesema chama husika kilipewa fursa ya kupendekeza na kilifanya hivyo, kabla ya NEC kuanika majina ya wabunge wapya wa CUF katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yamo katika taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani aliyoitoa jana jioni, akizungumzia tuhuma dhidi ya tume hiyo, inayodaiwa kukiuka kanuni katika uteuzi wa wabunge wanane wa viti maalumu wa CUF.

Sehemu ya Taarifa ya CUF katika mitandao ya kijamii inayoituhumu NEC inasema; “Kanuni walizojiwekea wenyewe Tume katika uteuzi wa watu wa kujaza nafasi hizo zinasema uteuzi huo unafuata mpangilio wa majina, kama ulivyokuwa umewasilishwa na chama husika wakati wa uteuzi wa wagombea wa ubunge wa viti maalumu wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

“CUF ilipeleka orodha yake ambayo haihusishi majina yaliyotangazwa, hivyo ndiyo kusema hata kama hicho kinachoitwa kufukuzwa uanachama wabunge hao kingekuwa halali (jambo ambalo si halali kama ilivyokwishaelezwa hapo juu), basi kwa Kanuni za Tume yenyewe, watu wa kujaza nafasi hizo wasingekuwa hao waliotangazwa.”

Kailima, katika taarifa yake, alisema taarifa zinazotolewa katika mitandao zikihusisha NEC kukihujumu chama hicho ni za kushangaza na kwamba Baraza Kuu la Uongozi la CUF, linataka kuupotosha umma kuhusu utekelezaji wa kazi za Tume.

“Chama husika ndicho kinaweza kujua ni nani siyo mwanachama wa chama hicho kwa kipindi cha kujaza nafasi wazi inapotokea,” alieleza Kailima na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa majina manane yaliyopendekezwa na CUF kujaza nafasi wazi za wabunge wa viti maalumu ni miongoni mwa majina 55 yaliyowasilishwa na chama hicho kwa barua yenye kumbukumbu Namba CUF/AK/DSM/ KM/003/1A/2015/14 ya Septemba 28, 2015 iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.

MY TAKE

Hapa NEC wamejichanganya. Nmezoea kuona NEC wakitumia Majina yaliyopo NEC kujaza nafasi za Viti maalum. Yaani Uchaguzi mkuu unapofanyika, Vyama vinatakiwa vipeleke idadi ya majina ya wabunge wa viti maalum. NEC ikitaka kumchukua mtu huwa inachukua kwenye ile orodha iliyopelekwa. Tumekuwa tukiona CHADEMA Wakifanyiwa hivyo.

Wabunge wa CHADEMA waliotangulia mbele ya haki, nafasi za kujaza walitumia Orodha ya uchaguzi mkuu na ndivyo sheria inataka.

Yaani kama majina yalipelekwa mia moja na chama kimepata viti maalum 20, yale themanini yanabaki NEC, Kukitokea tatizo wanahesabu kuanzia walipoishia bila kuruka mtu. Kama waliishia 20 basi litakapokuja tatizo wanaanza na 21 na kuendelea. Bila kuruka namba. Mfano kama walikuwa wameishia 20 kuongeza jao wabunge 8 walitakiwa wahesabu kuanzia 21 hadi 28. Likitokea tatizo tena huko mbeleni wanaanzia 29 kuendelea hadi ifike mia. Sasa hawa nec sijui wale wabunge waliwatoa wapi. NEC nasikia pale Ofisini tangu jana wanalaumiana, muda si mrefu kitanuka.

Hapa chini kwenye hii act wameelezea. 86A(8).
IMG_20170731_011730.png
 
Sawa, lakini je tume ya Uchaguzi haifahamu kuwa chama cha wananchi CUF kinamgogoro? Je, Bunge halifahamu chochote kuhusu mgogoro huo?

Hizo ni mbwembwe, tunafahamu kuwa mnatekeleza maelekezo.

Kuna watu wakifa hawastahili hata kuliliwa kulingana na mabaya, dhuluma, unyanyasaji, na udikteta wanaoufanya.
 
Nadhani kwenye hii hali iliyo Cuf ndio pale watu tunaposema tume hii ya uchaguzi sio huru wanapaswa kutuelewa. Kweli hii tume haijui kuna mgogoro wa wazi ndani ya Cuf? Kwenye hali hiyo unawezaje kumkubalia mwenyekiti tena ambaye ndio sababu hasa ya huo mgogoro kile anachotaka? Ikumbukwe hao wabunge aliowatimua hakushiriki kuwapata wakati wa uchaguzi. Hapo huoni Tume ya uchaguzi, bunge na serekali kwa kufanya walichofanya imeacha wazi nia yao ovu?
 
Majibu ya kusikitisha kabisa haya, hivi NEC hawajui kua kuna kesi mahakamani juu ya Mgogoro wa CUF. Mahakama imeshatoa uamuzi juu ya uhalali wa Lipumba kua mwanachama wa CUF?

Jibu ni Moja tu, Ramadhani Kailima ni kada wa CCM linajulikana hilo aache kujitetea,wanambeba Lipumba kuhairibu CUF.
 
Sawa, lakini je tume ya Uchaguzi haifahamu kuwa chama cha wananchi CUF kinamgogoro? Je, Bunge halifahamu chochote kuhusu mgogoro huo?

Hizo ni mbwembwe, tunafahamu kuwa mnatekeleza maelekezo.

Kuna watu wakifa hawastahili hata kuliliwa kulingana na mabaya, dhuluma, unyanyasaji, na udikteta wanaoufanya.
Wahenga walishanena, 'vita ya panzi ni furaha kwa kunguru'. Hao panzi wa CUF wajilaumu wenyewe... Kunguru (NEC) asilaumiwe hapa...
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefafanua juu ya uteuzi wa wabunge wapya wa Viti Maalumu wa Chama cha Wananchi (CUF).

Imesema kuwa imesikitishwa na kushangazwa na taarifa za Baraza Kuu la Taifa la chama hicho kwamba tume hiyo imekiuka kanuni zake katika uteuzi wa wabunge wanane wa chama hicho ili kujaza nafasi za wazi zilizotokea hivi karibuni.

Aidha, imesema chama husika kilipewa fursa ya kupendekeza na kilifanya hivyo, kabla ya NEC kuanika majina ya wabunge wapya wa CUF katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yamo katika taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani aliyoitoa jana jioni, akizungumzia tuhuma dhidi ya tume hiyo, inayodaiwa kukiuka kanuni katika uteuzi wa wabunge wanane wa viti maalumu wa CUF.

Sehemu ya Taarifa ya CUF katika mitandao ya kijamii inayoituhumu NEC inasema; “Kanuni walizojiwekea wenyewe Tume katika uteuzi wa watu wa kujaza nafasi hizo zinasema uteuzi huo unafuata mpangilio wa majina, kama ulivyokuwa umewasilishwa na chama husika wakati wa uteuzi wa wagombea wa ubunge wa viti maalumu wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

“CUF ilipeleka orodha yake ambayo haihusishi majina yaliyotangazwa, hivyo ndiyo kusema hata kama hicho kinachoitwa kufukuzwa uanachama wabunge hao kingekuwa halali (jambo ambalo si halali kama ilivyokwishaelezwa hapo juu), basi kwa Kanuni za Tume yenyewe, watu wa kujaza nafasi hizo wasingekuwa hao waliotangazwa.”

Kailima, katika taarifa yake, alisema taarifa zinazotolewa katika mitandao zikihusisha NEC kukihujumu chama hicho ni za kushangaza na kwamba Baraza Kuu la Uongozi la CUF, linataka kuupotosha umma kuhusu utekelezaji wa kazi za Tume.

“Chama husika ndicho kinaweza kujua ni nani siyo mwanachama wa chama hicho kwa kipindi cha kujaza nafasi wazi inapotokea,” alieleza Kailima na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa majina manane yaliyopendekezwa na CUF kujaza nafasi wazi za wabunge wa viti maalumu ni miongoni mwa majina 55 yaliyowasilishwa na chama hicho kwa barua yenye kumbukumbu Namba CUF/AK/DSM/ KM/003/1A/2015/14 ya Septemba 28, 2015 iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad.
Tume ya uchaguzi ni jumuiya ya chama cha mapinduzi
 
Tume imekubali ionekane kama ya kipumbavu kabisa hadi na watoto wa chekechea!! Hivi katika maamuzi kama haya yanayotolewa na watu walioonekana kuwa eti Ndiyo wenye akili zenye nafuu ni kipi kitatufanya tusijiite wendawazimu? Yaani unafanya jambo la kipumbavu kabisa tena mbele za watu! Halafu unakomaa kabisa kutetea eti Siyo upumbavu! Na wapumbavu wengine wa kundi lako wanaunga mkono upumbavu huo!! Si upumbavu huo?
 
Back
Top Bottom