Mtoto Wa Mbale
JF-Expert Member
- May 15, 2011
- 457
- 300
Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC)Jaji Mkuu mstaafu Bw. Damiani Lubuva akiongea na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa mikutano wa tume hiyo jijini Dar es salaam, kuhusiana na uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru mashariki kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu uchaguzi huo, ambapo jaji lubuva amekanusha vikali tuhuma za kuongeza vituo bandia zilizotolewa na chama cha (CHADEMA) Katika picha ulia Mkurugenzi wa tume ya uchakuzi Bw. Julias Mallaba, Kushoto Jaji mkuu mstaafu Zanzibar Makamu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Bw. Hamio Mahmoud Hamio.
Jaji John Joseph Mkwawa Kamishina wa tume (NEC)akifafanu jambo katika mkutano huo.kulia jaji Mary h.C.S Longway kamishina wa tume.
Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria katika mkutano huo
Kurunzi 07:23 Today
ituo bandia
Wakati hayo yakiendelea, tuhuma kwamba kuna
vituo 55 vya bandia vilivyoandaliwa kwa lengo
la kutumika kuiba kura kwenye uchaguzi huo,
zinaonekana kugonganisha vichwa vya maofisa
wa uchaguzi.
Tuhuma hizo ni zile zilizotolewa na Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa juzi
kwamba kuna vituo 55 bandia 55 vya kupigia
kura katika uchaguzi huo mdogo madai ambayo
yalikanushwa na Msimamzi wa Uchaguzi wa
Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi.
Juzi Kagenzi alipozungumza na waandishi wa
habari alisema vituo halali ambavyo
anavitambua ni 327 tu na hakukuwa na kituo
ambacho kimeongezwa na kwamba hata kama
ikitokea hivyo, itakuwa ni baada ya majadiliano
na vyama vyote shiriki.
Vituo vilivyopo ni 327 pekee, na kama ikitokea
kituo kinakuwa na watu zaidi ya 500 ndipo
kunaweza kuongezeka, lakini historia
inajionesha kila uchaguzi mdogo unapofanyika
idadi ya wapigakura inapungua,alisema
Kagenzi.
Lakini jana Kagenzi alikiri kuwapo kwa kasoro
kwenye orodha ya vituo hivyo na kwamba
alikuwa anawasiliana na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), ili kuwezesha kufanyika kwa
marekebisho.
Maeleo ya Kagenzi yanatokana na ushahidi
ambao gazeti hili liliupata kwa kuona orodha ya
vituo hivyo, ambayo ilikuwa ikionyesha
takwimu mbili tofauti za idadi ya vituo vya
kupigia kura.
Katika orodha hiyo, safu ya idadi ya vituo vya
kupigia kura katika kata 17 za jimbo hilo ilikuwa
ikionyesha vituo 327, wakati safu ya mwisho ya
orodha hiyo hiyo ilikuwa ikionyesha kuwapo
kwa jumla ya vituo 382, likiwa ni ongezeko la
vituo 55.
Waraka wa orodha hiyo unaonyesha kuwa katika
Kata ya Akheri kutakuwa na vituo 20 idadi
ambayo inayofautiana na iliyotolewa na tume
ambavyo ni vituo 18.
Kata nyingine ambazo vituo hivyo vinaonekana
kuongezwa ni Kikatiti vituo 22 badala ya 18,
Kata ya Kikwe vituo 12 badala ya halali 11, Kata
ya Kingori vituo 29 badala ya halali 26 na Kata
ya Leguruki vituo 23 badala ya halali 20.
Kata nyingine ni Makiba vituo 21 badla ya halali
18, Majiya chai 24 badala ya 29 halali, Maroroni
vituo 21 badala ya 17 halali, Mbuguni vituo 25
badala ya halali 21,Nkoarsambu vituo 10 badala
ya 8 vinavyohitajika na Kata ya Ngarenanyuki
ambako vimeongezwa vituo sita kutoka halali
20 hadi 26.
Orodha hiyo ambayo Kagenzi alithibitisha
kwamba ilikuwa na makosa pia ina kasoro
katika Kata za Nkoaranga ambako vituo
vimeongezwa kutoka halali 17 hadi 22, Pori
kutoka vituo halali 16 hadi 20, Nkwandua
kutoka vituo 22 hadi kufikia 25 na Kata ya Seela
- Singisi vituo hivyo viliongezwa kutoka halali
12 hadi 15.
Kata nyingine ni Songoro nyumbani kwa
Mgombea wa Chadema, Joshua Nassari vipo
vituo 15 na hakuna kilichoongezeka huku Kata
ya Usa River ilikuwa na vituo 36, lakini
vimeongezeka vitano na kufikia 41.
Kagenzi alisema alipowasiliana na idara ya
teknolojia ya habari ya NEC kuhusu kasoro hizo
walimwambia kwamba orodha ya awali haikuwa
toleo la mwisho na kwamba wangefanya
marekebisho ya kuondoa kasoro hizo.
Wameniambia kwamba hiyo orodha ilikuwa ni
working draft tu (rasimu ya kufanyiwa kazi),
kwahiyo nimeomba hiyo orodha kamili ya
mwisho, wakishanitumia nitaisambaza kwa
vyama husika,alisema Kagenzi jana.
Baadaye msimamizi huyo wa uchaguzi alisema
wataalamu kutoka NEC walitarajiwa kuwasili
Arumeru jana mchana kwa ajili ya kurekebisha
kasoro hizo pamoja na kufanya maandalizi
mengine kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo.
Hata hivyo, kauli ya Kagenzi ilikuwa ikipishana
na ile iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Julius Mallaba ambaye awali alisema hakukuwa
na vituo vya nyongeza kama ilivyodaiwa na Dk
Slaa.
Baada ya kuelezwa kuhusu orodha hiyo ya
tume, Mallaba alisema: Basi kama iko hivyo
nitawasiliana na wahusika ili tuone hatua
waliyofikia katika kurekebisha kasoro hizo.
Dk Slaa alisema hali kama hii waliibaini katika
Jimbo la Igunga mara baada ya matokeo
kutangazwa na baada ya kufuatilia walikuta
vituo hewa ambapo vilikuwa na kura kati ya 160
na 280.