Tume ya Uchaguzi yakanusha vikali kuwepo vituo hewa 55 vya kupigia kura Arumeru. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya Uchaguzi yakanusha vikali kuwepo vituo hewa 55 vya kupigia kura Arumeru.

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Molemo, Mar 22, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC)Jaji Mkuu mstaafu Bw. Damiani Lubuva akiongea na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa mikutano wa tume hiyo jijini Dar es salaam, kuhusiana na uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru mashariki kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu uchaguzi huo, ambapo jaji lubuva amekanusha vikali tuhuma za kuongeza vituo bandia zilizotolewa na chama cha (CHADEMA) Katika picha ulia Mkurugenzi wa tume ya uchakuzi Bw. Julias Mallaba, Kushoto Jaji mkuu mstaafu Zanzibar Makamu mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi Bw. Hamio Mahmoud Hamio.

  [​IMG]
  Jaji John Joseph Mkwawa Kamishina wa tume (NEC)akifafanu jambo katika mkutano huo.kulia jaji Mary h.C.S Longway kamishina wa tume.


  [​IMG]
  Baadhi ya waandishi wa habari walioudhuria katika mkutano huo

   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Leo ajabu ujaweka My Take...Chadema tumeishawazoe kwa kulalamika bila ushahidi wowote, mara nyingi uwa wanaanza kulalamika kipindi cha kampeni, kama mtakumbuka Slaa, alishawahi kusema kuna kontena la futi 20 limekamatwa Tunduma limejaa karatasi za kupigia kura, Polisi walipolifungua wakakuta vipodozi.
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu wangu nimeripoti kilichofanywa na tume leo.Sio kila kitu unaweka My take
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ameanisha jimbo la arumeru lina vituo vingapi vya kupigia kura?
   
 5. K

  Kima mdogo JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wamegundua janja yao imeshtukiwa wameamua wakane ila chadema wangezubaa tu ingekula kwao
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tayari malalamiko ya kushindwa yameshaanza.
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Si ni hao hao magamba unadhani watakubali hizo mbinu zao chafu
   
 8. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Hututaki kuona vituo zaidi ya 327, zaidi ya hapo patachimbika.
   
 9. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Ametoa maelezo yoyote kwa nini wamewanyima haki ya kupiga kura maelfu ya vijana waliofikisha umri wa miaka 18 kuanzia June 2010 na wahamiaji wa Arumeru? Kupiga kura ni haki ya hawa vijana ya kikatiba lakini inashangaza sana kwa nini Jaji mzima anasimamia huu uporaji wa haki na ubakaji wa demokrasia.
   
 10. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hawa mafisadi mbinu zao tunazo mifukoni.

  Hw tutakomaa nao mpk kieleweke!
   
 11. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ingekuwa uwongo alicho sema docta wangempuuza lakini kwa sababu ni kweli imebidi wafanye hivyo

   
 12. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Its better to be roughly right in time than to be precisely right too late. Big up CHADEMA!
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Vituo 327 mkuu
   
 14. w

  wakwetu 2 Member

  #14
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  rizt au riz1?
   
 15. M

  Molemo JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hapana mkuu
   
 16. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Vingapi waliwahi kukana na baadaye ikaonekana ni kweli? ZENJI KUJIUNGA NA OIC, LOLIONDO KUUZWA, MAFISADI etc. Hatutaki ije ionekane kuwa ni kweli wakati uchaguzi ushafanyika.
   
 17. m

  mahoza JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,241
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Naomba nieleweshwe pale Dr Slaa aliposema kuna vituo bandia zaidi ya 50 wamevigundua. Kuna mtu alikanusha na niliposoma Gazeti la Mwananchi wamethibitiisha kwa kutoa data. Huyo aliyesema nd Slaa ni muongo anaweza kutengua kauli yake hiyo? Asingesema si magamba wangefaidi? Sio kila kitu uinzani wakisema kikanushwe wanaongea kwa data. Kila la heri wanaJF.:bump2:
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Mar 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Mkuu usitie Shaka, CDM watakuwa na mawakala wa kutosha kwenye vituo vyote vya uchaguzi, hivyo vituo hewa vitakamatika mapema hata kabla ya uchaguzi. Intelijensia ya people's ina nguvu mpaka ndani ya tume ya uchaguzi
   
 19. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Vituo bandia

  Wakati hayo yakiendelea, tuhuma kwamba kuna vituo 55 vya bandia vilivyoandaliwa kwa lengo la kutumika kuiba kura kwenye uchaguzi huo, zinaonekana kugonganisha vichwa vya maofisa wa uchaguzi. Tuhuma hizo ni zile zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa juzi kwamba kuna vituo 55 bandia 55 vya kupigia kura katika uchaguzi huo mdogo madai ambayo
  yalikanushwa na Msimamzi wa Uchaguzi wa Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi. Juzi Kagenzi alipozungumza na waandishi wa
  habari alisema vituo halali ambavyo anavitambua ni 327 tu na hakukuwa na kituo ambacho kimeongezwa na kwamba hata kama
  ikitokea hivyo, itakuwa ni baada ya majadiliano na vyama vyote shiriki. "Vituo vilivyopo ni 327 pekee, na kama ikitokea kituo kinakuwa na watu zaidi ya 500 ndipo kunaweza kuongezeka, lakini historia inajionesha kila uchaguzi mdogo unapofanyika idadi ya wapigakura inapungua,"alisema Kagenzi.

  Lakini jana Kagenzi alikiri kuwapo kwa kasoro kwenye orodha ya vituo hivyo na kwamba alikuwa anawasiliana na Tume ya Taifa ya
  Uchaguzi (NEC), ili kuwezesha kufanyika kwa marekebisho. Maeleo ya Kagenzi yanatokana na ushahidi ambao gazeti hili liliupata kwa kuona orodha ya vituo hivyo, ambayo ilikuwa ikionyesha takwimu mbili tofauti za idadi ya vituo vya kupigia kura. Katika orodha hiyo, safu ya idadi ya vituo vya kupigia kura katika kata 17 za jimbo hilo ilikuwa ikionyesha vituo 327, wakati safu ya mwisho ya orodha hiyo hiyo ilikuwa ikionyesha kuwapo kwa jumla ya vituo 382, likiwa ni ongezeko la vituo 55. Waraka wa orodha hiyo unaonyesha kuwa katika Kata ya Akheri kutakuwa na vituo 20 idadi ambayo inayofautiana na iliyotolewa na tume ambavyo ni vituo 18.


  Kata nyingine ambazo vituo hivyo vinaonekana kuongezwa ni Kikatiti vituo 22 badala ya 18, Kata ya Kikwe vituo 12 badala ya halali 11, Kata ya Kingori vituo 29 badala ya halali 26 na Kata ya Leguruki vituo 23 badala ya halali 20. Kata nyingine ni Makiba vituo 21 badla ya halali 18, Majiya chai 24 badala ya 29 halali, Maroroni vituo 21 badala ya 17 halali, Mbuguni vituo 25 badala ya halali 21, Nkoarsambu vituo 10 badala ya 8 vinavyohitajika na Kata ya Ngarenanyuki ambako vimeongezwa vituo sita kutoka halali 20 hadi 26.
  Orodha hiyo ambayo Kagenzi alithibitisha kwamba ilikuwa na makosa pia ina kasoro katika Kata za Nkoaranga ambako vituo vimeongezwa kutoka halali 17 hadi 22, Pori kutoka vituo halali 16 hadi 20, Nkwandua kutoka vituo 22 hadi kufikia 25 na Kata ya Seela - Sing'isi, vituo hivyo viliongezwa kutoka halali 12 hadi 15.

  Kata nyingine ni Songoro nyumbani kwa Mgombea wa Chadema, Joshua Nassari vipo vituo 15 na hakuna kilichoongezeka huku Kata
  ya Usa River ilikuwa na vituo 36, lakini vimeongezeka vitano na kufikia 41. Kagenzi alisema alipowasiliana na idara ya teknolojia ya habari ya NEC kuhusu kasoro hizo walimwambia kwamba orodha ya awali haikuwa toleo la mwisho na kwamba wangefanya marekebisho ya kuondoa kasoro hizo. "Wameniambia kwamba hiyo orodha ilikuwa ni working draft tu (rasimu ya kufanyiwa kazi),
  kwahiyo nimeomba hiyo orodha kamili ya mwisho, wakishanitumia nitaisambaza kwa vyama husika,"alisema Kagenzi jana. Baadaye msimamizi huyo wa uchaguzi alisema wataalamu kutoka NEC walitarajiwa kuwasili Arumeru jana mchana kwa ajili ya kurekebisha
  kasoro hizo pamoja na kufanya maandalizi mengine kwa ajili ya uchaguzi huo mdogo.

  Hata hivyo, kauli ya Kagenzi ilikuwa ikipishana na ile iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Julius Mallaba ambaye awali alisema hakukuwa na vituo vya nyongeza kama ilivyodaiwa na Dk Slaa. Baada ya kuelezwa kuhusu orodha hiyo ya tume, Mallaba alisema: "Basi kama iko hivyo nitawasiliana na wahusika ili tuone hatua waliyofikia katika kurekebisha kasoro hizo". Dk Slaa alisema hali kama hii waliibaini katika Jimbo la Igunga mara baada ya matokeo kutangazwa na baada ya kufuatilia walikuta vituo hewa ambapo vilikuwa na kura kati ya 160 na 280.
   
 20. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapa tume ya ccm iko kazini tayari kufanya uchakachuzi. Hongera Dr. Slaa kwa kusimamia ukweli na kuwaumbua hawa wapuuzi wa tume ya uchaguzi. Wanakataa hata taarifa walizoziandaa wenyewe? What a shame.
   
Loading...