tume ya uchaguzi yaanza rasmi mkakati wa kuchakachua daftari 2015

tanira1

JF-Expert Member
Nov 18, 2011
942
159
wakuu leo nimesikia kichwa cha habari cha gazeti moja hapa nchini likiwa na habari ya kuwa tume ya uchguzi iko taaban kifedha katika kuboresha daftari la wapiga kula kwa ajili ya uchaguzi wa 2015, kwangu mimi huu ni mkakati mpya wa watawala kuhakikisha daftari hilo hariboreshwi hili tuingie uchaguzi kwa daftari la zamani wadau tujadili nini kinachopaswa kufanywa kunusuru taifa hili zidi ya mbinu chafu
 
Wasituchezee! Tutapitisha mchango nchi nzima kwa ajili ya kuipata hiyo hela.

Hapo ndo wataitambua nini maana ya M4C!
 
Usiwe na Shaka ndugu hakuna kitu Kama hicho kuingia kwenye uchaguzi mkuu bila ya kuboresha daftari. Watabana wataachia tu,

UOTE=tanira1;5110418]wakuu leo nimesikia kichwa cha habari cha gazeti moja hapa nchini likiwa na habari ya kuwa tume ya uchguzi iko taaban kifedha katika kuboresha daftari la wapiga kula kwa ajili ya uchaguzi wa 2015, kwangu mimi huu ni mkakati mpya wa watawala kuhakikisha daftari hilo hariboreshwi hili tuingie uchaguzi kwa daftari la zamani wadau tujadili nini kinachopaswa kufanywa kunusuru taifa hili zidi ya mbinu chafu[/QUOTE]
 
kuboresha daftari la wapiga kura ina maanisha kuiondoa ccm madarakani. Hilo liko wazi, hata wao wanalijua.
 
Daftari litaboreshwa baada ya kupatikana katiba mpya, kwa sasa kuna maoni kuwa tume hii ya uchaguzi siyo huru na maoni haya yanatolewa na watanzania ktk tume ya kuksuanya maoni.Tunaamini jaji warioba na tume yake wataona umuhim wa kuwapa watanzania TUME HURU YA UCHAGUZI na tume hiyo ndiyo itakuwa na wajibu wa kusafisha daftari la wapiga kura hii tume ya uchaguzi iliyopo ni ya kikwete si ya watanzania.WATABANA MWISHO WATAACHIA
 
Ni bora wachelewe maboresho yafanywe 2014. Hiyo inamaanisha vijana wengi zaidi wataingia kwa hiyo tutaweza kushindana vyema na watakaochagua sura ya Membe kureplce sura ya sasa
 
Hawa tume ya uchaguzi ya sasa ya jaji Lubuva wanatest zarii kuona je watanzania wanasemaje.Jibu letu kwa lubuva ni kwamba tunasubiri katiba mpya ndipo tuboreshe daftari.Haraka ya nini???????????????????
 
hii haiwezekani. uchaguzi hauwezi kufanywa bila kuboresha daftari. othewise wale wote waliotimiza 18yrs mara tu baada ya mboresho uliopita, watakwenda kwa korti na uchaguzi utazuiwa na korti. ni haki yao kikatiba kuandikishwa.
 
Wasituchezee! Tutapitisha mchango nchi nzima kwa ajili ya kuipata hiyo hela.

Hapo ndo wataitambua nini maana ya M4C!

mimi nipo tayari kufanya kazi bure ili mradi kusiwe na hundi itakayoandikwa kwamba wamelipa vibarua wa kufanya kazi hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom