Tume ya Uchaguzi ya Taifa inataka kuturudisha kwenye enzi za mgombea mmoja tu wa Urais?


MwanaHaki

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Messages
2,403
Likes
125
Points
145
MwanaHaki

MwanaHaki

R I P
Joined Oct 17, 2006
2,403 125 145
Wandugu

Hebu jioneeni wenyewe hiki kinachoandikwa kwenye Rasimu ya Katiba Mpya. Si maneno yangu.

77.-(1) Katika Uchaguzi wa Rais, kila chama cha siasa
kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha kwa
Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano, kwa mujibu wa sheria za
nchi, jina la mwanachama mmoja anayependekezwa kwa nafasi ya
madaraka ya Rais.
(2) Endapo ni Mgombea huru, kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa
katika Katiba hii, atawasilisha jina lakekwenye Tume Huru ya Uchaguzi.
(3) Mapendekezo ya majina ya wagombea katika uchaguzi wa Rais
yatawasilishwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi katika siku na kwa utaratibu
uliyoainishwa katika sheria za nchi.
(4) Endapo itafika saa na siku iliyotajwa kwa ajili ya
kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wagombea, ni mgombea mmoja tu
ambaye anapendekezwa kuwa halali, Tume Huru ya Uchaguzi itawasilisha
jina lake kwa wananchi, nao watapiga kura ya kumkubali au
kumkataa kwa mujibu wa masharti yaliyoainishwa katika sheria za
nchi.
 

Forum statistics

Threads 1,273,093
Members 490,291
Posts 30,471,138