Tume ya Uchaguzi Uganda yatishia kumuadhibu Museveni endapo hafuati masharti katika kampeni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda jaji Simon Mugenyi Byabakama, amesema kwamba tume hiyo haitasita kumchukulia hatua rais Yoweri Museveni ambaye ni mgombea urais kupitia chama cha National Resistance Movement – NRM, endapo hatafuta sheria za kampeni zilizowekwa na tume.

Kulingana na tume ya uchaguzi, wagombea wanastahili kuandaa mikutano ya kampeni isiyozidi watu 200, na lazima wafuate maagizo ya maafisa wa afya ya kukabiliana na janga la Virusi vya Corona.

Maagizo hayo ni pamoja na kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa na kutokaribiana.

Museveni amekuwa akifuata maagizo hayo na kuhutubia wafuasi wake kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari, lakini katika siku mbili zilizopita, amehutubia umati wa watu ambao hawakufuata maagizo ya afya, katika wilaya za Busia na Bukedi.

“Tutamwandikia barua kumkumbusha kwamba anastahili kufuata maagizo yetu ili sote tupambane na janga la Covid-19. Maagizo yetu hayana ubaguzi na usimamizi wetu wa kampeni hauna ubaguzi. Unapoidhinishwa na tume ya uchaguzi kugombea nafasi yoyote, unakuwa mgombea wetu na lazima ufuate masharti yetu,” amesema Byabakama akiongezea kwamba “mwelekeo tuliotoa unatumika kwa kila mgombea. Museveni ni mmoja wao na anastahili kufuata masharti yetu. Kila mgombea anastahili kuhakikisha kwamba wafuasi wake ama mawakala wake wa kampeni wanafuata masharti hayo.”

Byabakama alikuwa akihutubia waandishi wa habari baada ya kufanya mkutano na mgombea wa urais Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine katika makao makuu ya tume ya uchaguzi jijini Kampala.

Kyagulanyi alikutana na maafisa wa tume ya uchaguzi baada ya mikutano yake ya kampeni kuzuiwa na maafisa wa polisi wilayani Jinja na Kayunga.
Mikutano yake imekuwa ikishuhudia visa vya polisi kutumia gesi ya kutoa machozi na risasi za moto kutawanya wafuasi wake.

“Kama Byabakama ameshindwa kuandaa uchaguzi, anastahili kujiuzulu amoja na timu yake kwa sababu tunanyanyashwa na amesalia kimya.”amesema Kyagulanyi.

Hata hivyo, Byabakama amesema kwamba hawezi kujiuzulu na hajawahi kufikiria kwamba anaweza kujiuzulu.

“Mchakato wa uchaguzi ulianza mwaka 2018 na sasa tunakaribia kumaliza. Siwezi kujiuzulu kwa sababu ya mambo madogo yanayojitokeza. Tumewajibika katika kazi yetu kama tume ya uchaguzi la kuweka mwelekeo namna wagombea wanastahili kufanya kampeni lakini wagombea na wafuasi wao ndio wamekataa kufuata mwelekeo huo.”

Byabakama amewaambia waandishi wa habari kwamba tume ya uchaguzi imepanga kukutana na maafisa wa usalama Pamoja na wagombea ili kukubaliana namna ya kushirikiana kufanikisha uchaguzi mkuu wa Januari 14 2021 na uwe huru na haki.

Jua litachomoza hata mvua inyeshe kiasi gani - Nobert Mao
Hayo yakijiri, mkutano wa mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic party, DP, Nobert Mao umevuruggwa baada ya polisi kutumia gesi ya kutoa machozi na kutawanya wafuasi wake.

Mao alikuwa amepangiwa kufanya kampeni wilayani Kamuli, mashariki mwa Uganda, lakini polisi wakiongozwa na kamanda Ahmed Madiri, walifunga barabara punde tu alipowasili mjini humo na kumuamuru kurudi Kampala.

“Najua mna hamu kubwa sana kumfurahisha mkubwa wenu lakini ni lazima muelewe kwamba mnavuruga demokrasia nchini humu, na kukosa kutenda yaliyo mema kwa taifa hili,” amesema Nobert Mao huku polisi wakimlazimisha kureudi Kampala.

Ameendelea kusema kwamba “nashukuru kwa msaada wenu kunifukuza mjini na kunisindikiza hadi nje ya mji lakini hii ni gharama tunayolipia katika kutaka kurejesha demokrasia nchini humu. Daima, jua litachomoza kila baada ya mvua hata iwe kubwa namna gani. Ukweli na haki vitapatikana hivi karibuni.”

Msemaji wa polisi eneo la Busoga Michale Kasadha ameambia waandishi wa habari kwamba Mao hakutaka kufuata maagizo ya tume ya uchaguzi na kwamba hakuwa ameomba kibali kufanya kampeni katika ehemu aliyokuwa anataka kuhutubia wafuasi wake.

Mgombea wa FDC adai tume ya uchaguzi inashirikiana na polisi kukandamiza wagombea wa upinzani
Mgombea wa FDC asema tume ya uchaguzi inashirikiana na polisi kukandamiza upinzani

Naye mgombea wa urais kupitia chama cha Forum for Democratic Change Patrick Amuriat, amedai kwamba maafisa wa tume ya uchaguzi wanashirikiana na maafisa wa usalama kuwapiga, kuwatesa na kuvuruga wafuasi wa upinzani.

Amuriat, ametaka Robert Kyagulanyi kuacha kutafuta msaada wa tume ya uchaguzi dhidi ya polisi, akisema kwamba hatasaidiwa kwa namna yoyote.

“Dhuluma zote ambazo maafisa wa usalama wanatufanyia kama wagombea wa upinzani ni za maksudi na tume ya uchaguzi ni sehemu ya mpango huo. Kwenda kushitaki kwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi jaji Byabakama ni sawa na kwenda kushitaki kwa rais Yoweri Museveni ambaye ndiye amepanga haya yote tunayopitia.” Amuriat ameliambia gazeti la Uganda la Daily Nation.

Museveni aendelea na kampeni mashariki mwa Uganda
Rais Yoweri Museveni ameendelea kufanya kampeni mashariki mwa Uganda, akizindua miradi mbalimbali na kueneza ujumbe kwamba analinda maslahi ya baadaye ya nchi.

Amezindua ujenzi wa barabara na kuanzisha safari ya feri katika kivuko cha Sigulu, Ziwa Victoria na kusema ni yeye pekee mwenye uwezo wa kuongoza Uganda na kwamba wapinzani wake wote hawana rekodi yoyote ya maendeleo na wanachofanya ni kuwahadhaa wapiga kura wa Uganda.

Amekuwa pia akifungua masoko ambayo ujenzi wake umekamilika na kuahidi kuwasaidia wafanyabiashara katika sehemu mbalimbali za nchi.

Museveni amekuwa akimlenga sana Bobi Wine katika kampeni zake, akisema kwamba hakuna cha maana ambacho Bobi Wine anaweza kufanyia vijana.
 
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda jaji Simon Mugenyi Byabakama, amesema kwamba tume hiyo haitasita kumchukulia hatua rais Yoweri Museveni ambaye ni mgombea urais kupitia chama cha National Resistance Movement – NRM, endapo hatafuta sheria za kampeni zilizowekwa na Tume.

Chanzo: VOA


My Opinion: Ingawa ni kinafiki, angalau tume hii ya uchaguzi imejaribu kumpiga mkwara M7! Lakini tume ya jirani yake "Mmmh!!! Thubutu!!!
 

Attachments

  • 01DEDCD2-B517-45D9-A405-AE40220AEDBB_w408_r1_st.jpg
    01DEDCD2-B517-45D9-A405-AE40220AEDBB_w408_r1_st.jpg
    6.9 KB · Views: 1
Tuseme kweli pamoja na udikteta wote wa Museven Uganda mahakama zake ziko huru sana.
 
Back
Top Bottom