Elections 2010 Tume ya uchaguzi Tanzania yakataa dai la upinzani.

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Tume ya uchaguzi Tanzania yakataa dai la upinzani.

DAR ES SALAAM
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania imelikataa dai la chama cha upinzani kuhesabu upya kura, kwa sababu wanadai kumekuwa na udanganyifu. Mwenyekiti wa tume hiyo Lewis Makame amesema huenda kuna hitilafu ya idadi katika kujumuishwa kwa kura, lakini hilo haliwezi kubadilisha matokeo ya mwisho. Makame ametangaza matokeo zaidi ambayo yanaonyesha rais aliye madarakani Jakaya Kikwete wa chama tawala cha Mapinduzi CCM atashinda muhula wake wa pili na wa mwisho. Dkt Wilbroad Slaa, mgombea wa urais wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA alikuwa ameitaka tume ya uchaguzi kusitisha kutangaza matokeo ya urais kwa sababu kulikuwa na makosa mengi.
Waangalizi wa Kimataifa ikiwemo wale kutoka Umoja wa Ulaya wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na utaratibu wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, wakisema walikuwa na shaka na uwazi wa shughuli nzima ya kujumuishwa kwa kura. Uchaguzi mkuu nchini Tanzania ulifanyika Jumapili iliopita na matokeo kamili ya rais yanatarajiwa kutolewa hapo kesho.]
source:http://www.dw-world.de/dw/function/0,,82228_cid_6188110,00.html
 
Waangalizi wa Kimataifa ikiwemo wale kutoka Umoja wa Ulaya wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na utaratibu wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, wakisema walikuwa na shaka na uwazi wa shughuli nzima ya kujumuishwa kwa kura.[/COLOR] Uchaguzi mkuu nchini Tanzania ulifanyika Jumapili iliopita na matokeo kamili ya rais yanatarajiwa kutolewa hapo kesho.]
source:Tume ya uchaguzi Tanzania yakataa dai la upinzani. | Matukio Duniani | Deutsche Welle | 04.11.2010

hapa haihitaji uwe na phd kuelewa kinachoendelea
 
CCm wakikataa matokeo ni sawa na hakuna anayepinga, ila upinzani wakikataa matokeo yaliyopikwa wazi wazi inakuwa ni uchochezi. Jamani nchii hii ni yetu sote, sio ya akina flani tu! Makame! Tutaonana wabaya.
 
Ni sahihi Tume kukataa dai la upinzani kuwa kura zihesabiwe tena. Ni kweli pia hata kama zitakuwepo kura za zitakazoongezeka kwa Slaa, bado hazitamuwezesha kuwa rais. Hayo si matokeo ya mtihani ambayo wanafunzi waliofaulu wote kwa ujumla wao wanasonga mbele, bali matokeo ya kura ni kumtafuta mshindi mmoja tu kuwa rais na tayari hilo liko wazi. Kama kweli Slaa hana uchu na madaraka, akapiganie maslahi ya taifa, si kuleta ukorofi.
 
ni sahihi tume kukataa dai la upinzani kuwa kura zihesabiwe tena. ni kweli pia hata kama zitakuwepo kura za zitakazoongezeka kwa slaa, bado hazitamuwezesha kuwa rais. Hayo si matokeo ya mtihani ambayo wanafunzi waliofaulu wote kwa ujumla wao wanasonga mbele, bali matokeo ya kura ni kumtafuta mshindi mmoja tu kuwa rais na tayari hilo liko wazi. kama kweli slaa hana uchu na madaraka, akapiganie maslahi ya taifa, si kuleta ukorofi.

tusipotoshane hakuna mtu aliyetaka kura zihesabiwe tena. Dr slaa anapinga matokeo yanayotangazwa na tume ya uchaguzi kuwa hayako sawa na matokeo halisi kama ilivyohesabiwa vituoni na kujazwa katika fomu za matokeo na kusainiwa na wasimamizi wa uchaguzi na mawakala wa vyama.

kama inekuwa ni kumtafuta mshindi kiholela kama unavytaka tuamini basi ingetosha watu kuonyesha vidole. Ili mradi tumeamua kuingia katika uchaguzi ni lazima kura zihesabiwe,na matokeo kujazwa katika fomu za matokeo kazi iliyofanyika kwa ufanisi mkubwa.

matokeo hayo ndio yanapaswa kutangazwa na tume ya uchaguzi na sio tume kutangaza utashi wa watu wachache.
 
Tume ya uchaguzi Tanzania yakataa dai la upinzani.

DAR ES SALAAM
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania imelikataa dai la chama cha upinzani kuhesabu upya kura, kwa sababu wanadai kumekuwa na udanganyifu. Mwenyekiti wa tume hiyo Lewis Makame amesema huenda kuna hitilafu ya idadi katika kujumuishwa kwa kura, lakini hilo haliwezi kubadilisha matokeo ya mwisho. Makame ametangaza matokeo zaidi ambayo yanaonyesha rais aliye madarakani Jakaya Kikwete wa chama tawala cha Mapinduzi CCM atashinda muhula wake wa pili na wa mwisho. Dkt Wilbroad Slaa, mgombea wa urais wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA alikuwa ameitaka tume ya uchaguzi kusitisha kutangaza matokeo ya urais kwa sababu kulikuwa na makosa mengi.
Waangalizi wa Kimataifa ikiwemo wale kutoka Umoja wa Ulaya wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na utaratibu wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, wakisema walikuwa na shaka na uwazi wa shughuli nzima ya kujumuishwa kwa kura. Uchaguzi mkuu nchini Tanzania ulifanyika Jumapili iliopita na matokeo kamili ya rais yanatarajiwa kutolewa hapo kesho.]
source:Tume ya uchaguzi Tanzania yakataa dai la upinzani. | Matukio Duniani | Deutsche Welle | 04.11.2010

Kwenye red sio kuhesabu upya bali kurudiwa.
 
Jamani hakuna matokeo haya zaidi ya maigizo ya familia ya JK.Tupate utaratibu wa maandamano ya amani yasiyo na mwisho hadi kieleweke.
 
Unapokataa Matokeo mheshimiwa Slaa unamaanisha kwamba wale vijana na wazee waliokuwa wanakesha kulinda kura zako wanaumwa na mbu njaa je nao walihusika kuchakachua? Au walipewa hongo?

Mheshimiwa Slaa naomba uwe muungwana kidogo!
 
Acha ujinga na kulopoka tu kama kama ujinga wenu makamba... unajua madai ya Dr Slaa na unajua wanacho kifanya NEC au imradi uumechangia kaa kimya kama hujui....
 
Tume ya uchaguzi Tanzania yakataa dai la upinzani.

DAR ES SALAAM
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania imelikataa dai la chama cha upinzani kuhesabu upya kura, kwa sababu wanadai kumekuwa na udanganyifu. Mwenyekiti wa tume hiyo Lewis Makame amesema huenda kuna hitilafu ya idadi katika kujumuishwa kwa kura, lakini hilo haliwezi kubadilisha matokeo ya mwisho. Makame ametangaza matokeo zaidi ambayo yanaonyesha rais aliye madarakani Jakaya Kikwete wa chama tawala cha Mapinduzi CCM atashinda muhula wake wa pili na wa mwisho. Dkt Wilbroad Slaa, mgombea wa urais wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA alikuwa ameitaka tume ya uchaguzi kusitisha kutangaza matokeo ya urais kwa sababu kulikuwa na makosa mengi.
Waangalizi wa Kimataifa ikiwemo wale kutoka Umoja wa Ulaya wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na utaratibu wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, wakisema walikuwa na shaka na uwazi wa shughuli nzima ya kujumuishwa kwa kura. Uchaguzi mkuu nchini Tanzania ulifanyika Jumapili iliopita na matokeo kamili ya rais yanatarajiwa kutolewa hapo kesho.]
source:Tume ya uchaguzi Tanzania yakataa dai la upinzani. | Matukio Duniani | Deutsche Welle | 04.11.2010

Yetu macho
 
Unapokataa Matokeo mheshimiwa Slaa unamaanisha kwamba wale vijana na wazee waliokuwa wanakesha kulinda kura zako wanaumwa na mbu njaa je nao walihusika kuchakachua? Au walipewa hongo?

Mheshimiwa Slaa naomba uwe muungwana kidogo!
Hivi unaelewa kinachobishaniwa? kama hujui ni bora kunyamaza sio kila kitu unataka kuchangia wakati kichwani uko mtupu.
Slaa analobishania ni jambo ambalo kama tume wangemkubalia lisingechukua hata siku nzima. Kujumlisha hesabu kama ilivyo sainiwa kutoka vituoni na mawakala maana hesabu hiyo kila chama wanayo na sii hesabu inayosomwa na Makame. Hapo la ajabu nini? Mtu kashinda n'gombe halafu mtangazaji anasema kashinda kuku halafu ndio basi yaishe? tulisimama foleni siku ile za nini kama Makame na NEC yake wanamamlaka ya kupanga idadi ya kura wao wenyewe? HATUKUBALI
 
Back
Top Bottom