Tume ya uchaguzi Tanzania yakataa dai la upinzani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya uchaguzi Tanzania yakataa dai la upinzani.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Saint Ivuga, Nov 4, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,893
  Trophy Points: 280
  Tume ya uchaguzi Tanzania yakataa dai la upinzani.


  DAR ES SALAAM
  Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania imelikataa dai la chama cha upinzani kuhesabu upya kura, kwa sababu wanadai kumekuwa na udanganyifu. Mwenyekiti wa tume hiyo Lewis Makame amesema huenda kuna hitilafu ya idadi katika kujumuishwa kwa kura, lakini hilo haliwezi kubadilisha matokeo ya mwisho. Makame ametangaza matokeo zaidi ambayo yanaonyesha rais aliye madarakani Jakaya Kikwete wa chama tawala cha Mapinduzi CCM atashinda muhula wake wa pili na wa mwisho. Dkt Wilbroad Slaa, mgombea wa urais wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA alikuwa ameitaka tume ya uchaguzi kusitisha kutangaza matokeo ya urais kwa sababu kulikuwa na makosa mengi.
  Waangalizi wa Kimataifa ikiwemo wale kutoka Umoja wa Ulaya wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na utaratibu wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, wakisema walikuwa na shaka na uwazi wa shughuli nzima ya kujumuishwa kwa kura. Uchaguzi mkuu nchini Tanzania ulifanyika Jumapili iliopita na matokeo kamili ya rais yanatarajiwa kutolewa hapo kesho.]
  source:http://www.dw-world.de/dw/function/0,,82228_cid_6188110,00.html
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,496
  Likes Received: 19,893
  Trophy Points: 280


  hapa haihitaji uwe na phd kuelewa kinachoendelea
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Huyu Kivyuitu wa bongo atapaswa kujiuzuru!
   
 4. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  CCm wakikataa matokeo ni sawa na hakuna anayepinga, ila upinzani wakikataa matokeo yaliyopikwa wazi wazi inakuwa ni uchochezi. Jamani nchii hii ni yetu sote, sio ya akina flani tu! Makame! Tutaonana wabaya.
   
 5. M

  Mashakamasudi New Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni sahihi Tume kukataa dai la upinzani kuwa kura zihesabiwe tena. Ni kweli pia hata kama zitakuwepo kura za zitakazoongezeka kwa Slaa, bado hazitamuwezesha kuwa rais. Hayo si matokeo ya mtihani ambayo wanafunzi waliofaulu wote kwa ujumla wao wanasonga mbele, bali matokeo ya kura ni kumtafuta mshindi mmoja tu kuwa rais na tayari hilo liko wazi. Kama kweli Slaa hana uchu na madaraka, akapiganie maslahi ya taifa, si kuleta ukorofi.
   
 6. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  tusipotoshane hakuna mtu aliyetaka kura zihesabiwe tena. Dr slaa anapinga matokeo yanayotangazwa na tume ya uchaguzi kuwa hayako sawa na matokeo halisi kama ilivyohesabiwa vituoni na kujazwa katika fomu za matokeo na kusainiwa na wasimamizi wa uchaguzi na mawakala wa vyama.

  kama inekuwa ni kumtafuta mshindi kiholela kama unavytaka tuamini basi ingetosha watu kuonyesha vidole. Ili mradi tumeamua kuingia katika uchaguzi ni lazima kura zihesabiwe,na matokeo kujazwa katika fomu za matokeo kazi iliyofanyika kwa ufanisi mkubwa.

  matokeo hayo ndio yanapaswa kutangazwa na tume ya uchaguzi na sio tume kutangaza utashi wa watu wachache.
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Kwenye red sio kuhesabu upya bali kurudiwa.
   
 8. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Jamani hakuna matokeo haya zaidi ya maigizo ya familia ya JK.Tupate utaratibu wa maandamano ya amani yasiyo na mwisho hadi kieleweke.
   
 9. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Unapokataa Matokeo mheshimiwa Slaa unamaanisha kwamba wale vijana na wazee waliokuwa wanakesha kulinda kura zako wanaumwa na mbu njaa je nao walihusika kuchakachua? Au walipewa hongo?

  Mheshimiwa Slaa naomba uwe muungwana kidogo!
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Acha ujinga na kulopoka tu kama kama ujinga wenu makamba... unajua madai ya Dr Slaa na unajua wanacho kifanya NEC au imradi uumechangia kaa kimya kama hujui....
   
 11. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Yetu macho
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Hivi unaelewa kinachobishaniwa? kama hujui ni bora kunyamaza sio kila kitu unataka kuchangia wakati kichwani uko mtupu.
  Slaa analobishania ni jambo ambalo kama tume wangemkubalia lisingechukua hata siku nzima. Kujumlisha hesabu kama ilivyo sainiwa kutoka vituoni na mawakala maana hesabu hiyo kila chama wanayo na sii hesabu inayosomwa na Makame. Hapo la ajabu nini? Mtu kashinda n'gombe halafu mtangazaji anasema kashinda kuku halafu ndio basi yaishe? tulisimama foleni siku ile za nini kama Makame na NEC yake wanamamlaka ya kupanga idadi ya kura wao wenyewe? HATUKUBALI
   
Loading...