Tume ya uchaguzi, punguza majimbo ya uchaguzi


Z

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Messages
724
Likes
648
Points
180
Z

Zygot

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2016
724 648 180
Hili ni ombi langu kwenu tume, kwamba uchaguzi ujao, punguzeni majimbo ya uchaguzi. Hatuwezi kuendelea kwa kuwa na majimbo kila mtaa. Ongezeko la majimbo limeifanya siasa kuwa ni agenda ya nchi, kila siku. Kila siku! Hakuna anayezungumzia elimu au afya kila siku. Ni siasa kila siku.

Ktk kipindi cha takriban miaka 30, nchi ina wanasiasa wengi kuliko waalimu na madaktari! Ukiongeza shule tutaelewa pia kwamba ndo ajenda ya nchi na ni hivyo kama utaongeza hospitali na ukubwa wa mashamba. Kuna watu sasa hivi wnalipwa kwa kufanya siasa bila kazi nyingine ktk maisha yao. Huu ni uzembe na haitachukuwa miaka mingi kila mwanafunzi atachukia udaktari, uinjinia na kutamani siasa tuu!

Tumechoka! Pelekeni pesa ktk mambo ya msingi kitaifa acheni kujiongezea kazi kwa kuongeza majimbo. Hii haihitaji katiba ni uamuzi wenu Tume ya uchaguzi.
 
Patriot

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
2,878
Likes
1,725
Points
280
Patriot

Patriot

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
2,878 1,725 280
Baada ya uchaguzi huu naikumba msg hii. Ni halali kila siku uchaguzi? Uchaguzi wa aina hii unaongeza nini ktk jamii hii?

Wiki ijayo, wengine wataunga mkono tena na tuanze kampeni. Hakika hatuhitaji kusubili katiba mpya. TUme ina madaraka ya kutupunguzia matumizi haya mabaya.
 
Caroline Hans

Caroline Hans

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2017
Messages
723
Likes
383
Points
80
Caroline Hans

Caroline Hans

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2017
723 383 80
Hili ombi ni batili ndio maana hata wachangiaji hawaonekani
 
Caroline Hans

Caroline Hans

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2017
Messages
723
Likes
383
Points
80
Caroline Hans

Caroline Hans

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2017
723 383 80
Mtoa post naomba nikusaidie tu kukujibu hiyo hoja yako Batili kwa majibu yafuatayo ukiyasoma utaelewa kwa nini tuna majimbo na hautarudia tena kuja na hoja nyepesi kama hiii ambayo haina mashiko kwa ustawi wa nchi yetu.


UGAWAJI MAJIMBO YA UCHAGUZI
Kwa mujibu wa Ibara ya 74(5) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina jukumu la kuchunguza na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Majimbo ya Uchaguzi kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge.

Kuchunguza mgawanyo wa Mipaka ya Majimbo katika Jamhuri ya Muungano na kubadilisha Majimbo ya Uchaguzi hupaswa kufanywa angalau kila baada ya miaka kumi.

Vigezo vinavyotumika ni ;-

Wastani wa Idadi ya Watu,
Upatikanaji wa mawasiliano; na
Hali ya kijiografia.

mwaka 2010, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifanya utafiti katika Jumuiya ya nchi zilizopo Kusini mwa Bara la Afrika, ili kujua vigezo vingine vinavyoweza kutumika katika nchi hizo kwa lengo la kuchunguza mipaka na kugawa majimbo kwa ufanisi zaidi. Baada ya utafiti huo, na kwa kuzingatia mashauriano na wadau mbalimbali, Tume iliongeza vigezo vingine katika Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka huo ambavyo ni:-

Hali ya kiuchumi;

Ukubwa wa Eneo la Jimbo husika;
Mipaka ya Kiutawala;

Jimbo moja lisiwe ndani ya Wilaya/Halmashauri mbili;

Kata moja isiwe ndani ya majimbo mawili;
Mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu;
Mazingira ya Muungano;

Uwezo wa Ukumbi wa Bunge; na
Idadi ya Viti Maalum vya Wanawake.

Aidha, kwa kuzingatia Ibara ya 75(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, katika Uchaguzi wa mwaka 2015, Tume ilitumia vigezo vitatu tu ambavyo ni:

Idadi ya Watu, ambapo Tume iliamua kuyagawa Majimbo yote yaliyokuwa na idadi ya watu zaidi ya 400,000;

Ukubwa wa ukumbi wa Bunge; na
Mipaka ya kiutawala.

Kuhusu utaratibu wa kugawa majimbo ya Uchaguzi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inao utaratibu wa kuchunguza mipaka na kugawa majimbo ya Uchaguzi kama ifuatavyo:-

Kufanya mikutano na wadau kwa kujadili vigezo na utaratibu unaotumika katika kuchunguza Mipaka na kugawa Majimbo;
Kutangaza kwa Wadau mbalimbali na Wananchi kwa ujumla kuhusu nia ya kufanya zoezi la kuchunguza mipaka na kugawa Majimbo. Katika matangazo hayo vigezo na utaratibu unaotumika vinaelezwa;
Kupokea maombi na mapendekezo ya kugawa, kurekebisha mipaka au kubadili majina ya Majimbo kutoka kwa wadau mbalimbali na kuyachambua;
Kuainisha maombi ambayo yametimiza vigezo.
Kutembelea maeneo ambayo yanakusudiwa kugawanywa; kukutana na wadau wa maeneo hayo wakiwemo wa ngazi za Kata, Mitaa, Vijiji na Vitongoji ili kujadiliana na kukubaliana kuhusu namna ya kufanya ugawaji,matayarisho ya ramani na majina ya Majimbo mapya;
Kuandaa taarifa ya mapendekezo ya ugawaji wa majimbo na kuiwasilisha kwa Mhe. Rais kwa mujibu wa ibara 75(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Kutangaza Majimbo kama yalivyogawanywa/yalivyorekebishwa mipaka au kubadilishiwa majina katika Gazeti la Serikali.
 

Forum statistics

Threads 1,250,505
Members 481,371
Posts 29,735,954