Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi, pigeni marufuku JKT kujihusisha na Mambo ya kampeni

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Tunaelewa JKT Wana miradi wanayosimamia na yawezekana wanalipwa kujenga majukwaa ya CCM kwa ajili ya kampeni. Ila huu ni uchaguzi na jeshi ni chombo neutral katika issue kama hizi, tuliona Dodoma magereza wakitumia wafungwa kufunga bendera za chama, leo Singida JKT wanaingia mtaani kutengeneza majukwaa, si sawa.

Hawa vijana wanapaswa kujitolea kulinda nchi siyo kulinda chama, wafungwa wanapaswa kuzalisha kwa ajili ya nchi siyo kwa ajili ya chama. Kuendelea kuruhusu haya yaendelee nikuhatarisha usalama wa nchi.

TUME YA UCHAGUZI MNAPWAYA SANA, MNASHINDWA KUKEMEA HATA MAMBO YA KAWAIDA KABISA, MMEDHARAULIKA NA KUENDESHWA NA SERIKALI HADI LADHA YA TUME HAKUNA. MAJAJI WETU SIJUI WANAJAJI NINI?

JAJI ANAPASWA KUSIMAMIA HAKI SIYO KUSIMAMISHWA KUSIMAMIA HAKI,
 
Wajifunze Kenya na Malawi. Lkn waogope sn nguvu ya umma
 
Suma JKT wanafanya biashara.

Hata Chadema mkihitaji Huduma zao mnakaribishwa kwa bei za kixalendo kabisa!
Iko wazi kuwa watahatarisha ajira zao, huoni Mkuu wa majeshi, Polisi, TBC (chombo cha serikali) wanavyohangaika kulinda ajira zao.
Kwa katiba yetu Mgombea wa CCM bado ni Raisi wa JMTZ
 
KWA TAARIFA YAKO NI KWAMBA JESHI LA KUJENGA TAIFA LINA KITENGO CHA BIASHARA KINAITWA SUMA JKT.

HATA CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO, CHADEMA MKIWALIPA WATAFANYA KAZI ZENU BILA SHIDA. ACHENI KULIA LIA MITANDAONI. View attachment 1555284
20200901110631_IMG_0677.JPG
 
Kama wanalipwa hakuna tatizo, ila kama wanafanya bure sio sawa. Kuna uwezekano CCM wameamua kuwatumia SUMA JKT kwa kuwalipa ili kulinda usalama wa Rais kwa kuwa vijana wanaotumika hapo wote wanawajua taarifa zao. Ila CDM na yale majukwaa yenu kama ya vigodoro mtaweza kuwalipa SUMA JKT kweli ?
 
Nijuavyo mimi hapo CCM analetewa invoice kwa services waliyotoa JKT, JKT Nni service provider mtu au taasisi yoyote wakiitaji services zao wapo huru kuzitumia.
 
Back
Top Bottom