Tume ya uchaguzi (NEC) kutumia Sh2.5 bilioni uchaguzi wa madiwani

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
madiwa+pic.jpg
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika Novemba 26,2017 katika kata 43 utagharimu Sh2.5 bilioni.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani amesema msingi wa bajeti ya uchaguzi unategemea idadi ya vituo vya kupigia kura na idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika kata husika.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari leo Novemba Mosi,2017 Kailima amesema idadi ya wapiga kura ndiyo inatoa bajeti ya mahitaji ya vifaa vya kuendeshea uchaguzi kama vile karatasi za kura na idadi ya vituo ambavyo vinakuwa na watumishi wasiopungua wanne.

Amesema kituo cha kupigia kura kina watendaji wanne ambao ni msimamizi na msimamizi msaidizi, karani mwongozaji na mlinzi wa kituo.

“Lakini pia kuna watu wa ziada kama wasimamizi wasaidizi wako ngazi ya kata na jimbo ambao wanahusika kusimamia uchaguzi katika maeneo husika,” amesema.

Amesema gharama nyingine za uchaguzi ziko kwenye usafirishaji wa vifaa kutoka Tume kwenda kwenye halmashauri husika na kutoka halmashauri kwenda kwenye kata ambako uchaguzi unafanyika. “Gharama hizo pia zinahusu utoaji wa elimu ya mpiga kura kupitia machapisho mbalimbali ya elimu ya mpiga kura, maelekezo kwa watendaji wa uchaguzi,” amesema.

Amesema elimu pia hutolewa kupitia vyombo vya habari na machapisho yatakayotumika kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura.

“Kwa uchaguzi huu mdogo bajeti ni Sh2.5 bilioni. Si kwamba kila kata itatumia gharama sawa za fedha hizi, bali kuna kata itatumia Sh20 milioni kutokana na idadi ya vituo vya kupigia kura kuwa vichache na kata yenye vituo vingi kwenye uchaguzi huu itatumia Sh150 milioni,” amesema Kailima.

Kailima amesema vyama vya siasa vinatakiwa kuhakikisha vinawaelimisha wafuasi, wapenzi na wanachama wao juu ya kutekeleza maadili katika kipindi chote cha kampeni.

Amesema maadili yatakiukwa, chama husika pamoja na mgombea watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Kailima amesema baadhi ya vitendo vya kuvunja maadili ya uchaguzi ni kuchana mabango ya wagombea, kutoa lugha chafu wakati wa mikutano ya kampeni na kupitisha muda wa kufanya mikutano ya kampeni.

Amesema kamati za maadili za kata na jimbo zitachukua hatua kali kwa chama au mgombea ambaye atakiuka maadili na kwamba, zinatakiwa kuchukua hatua ndani ya saa 48 baada ya chama au mgombea anapovunja maadili.

Amezitaja baadhi ya adhabu ni kuomba radhi wananchi hadharani, kutotumia vyombo vya habari kwa muda fulani wakati wa kampeni, onyo la maandishi, kusimamishwa kufanya kampeni, mgombea kutangaza mbele ya vyombo vya habari kuwa yeye ni bingwa wa kukikuka maadili ya uchaguzi au kutozwa faini ya Sh100,000.

Chanzo: Mwananchi
 
Ngoja nitamuuliza mwenyenyuma hizi zingeweza kufanyia nini katika jamii, kama vp uchaguzi uahirishwe hadi 2020.
 
Ni kwa sababu ya wale Madiwani Wapuuzi walio nunuliwa...!!

Laana kubwa iwaendee wao na familia zao.

Pesa hii ingeweza kununua hata Madawa na kuokoa Maisha ya Watanzania wenzetu..!
 
Kwa hyo na Nyalandu alaaniwe kwa kuturudisha kwenye uchaguzi?
 
Ni kwa sababu ya wale Madiwani Wapuuzi walio nunuliwa...!!

Laana kubwa iwaendee wao na familia zao.

Pesa hii ingeweza kununua hata Madawa na kuokoa Maisha ya Watanzania wenzetu..!
Hiyo laana haiwezi kuwapata labda iende kwa gambo,mnyeti na kiongozi wao alieruhusu mchezo huo wa kununua madiwani,tukutane field ndio watajua kua arusha sio chattle
 
Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika Novemba 26,2017 katika kata 43 utagharimu Sh2.5 bilioni.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Ramadhani amesema msingi wa bajeti ya uchaguzi unategemea idadi ya vituo vya kupigia kura na idadi ya wapiga kura walioandikishwa katika kata husika.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari leo Novemba Mosi,2017 Kailima amesema idadi ya wapiga kura ndiyo inatoa bajeti ya mahitaji ya vifaa vya kuendeshea uchaguzi kama vile karatasi za kura na idadi ya vituo ambavyo vinakuwa na watumishi wasiopungua wanne.

Amesema kituo cha kupigia kura kina watendaji wanne ambao ni msimamizi na msimamizi msaidizi, karani mwongozaji na mlinzi wa kituo.

“Lakini pia kuna watu wa ziada kama wasimamizi wasaidizi wako ngazi ya kata na jimbo ambao wanahusika kusimamia uchaguzi katika maeneo husika,” amesema.

Amesema gharama nyingine za uchaguzi ziko kwenye usafirishaji wa vifaa kutoka Tume kwenda kwenye halmashauri husika na kutoka halmashauri kwenda kwenye kata ambako uchaguzi unafanyika. “Gharama hizo pia zinahusu utoaji wa elimu ya mpiga kura kupitia machapisho mbalimbali ya elimu ya mpiga kura, maelekezo kwa watendaji wa uchaguzi,” amesema.

Amesema elimu pia hutolewa kupitia vyombo vya habari na machapisho yatakayotumika kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura.

“Kwa uchaguzi huu mdogo bajeti ni Sh2.5 bilioni. Si kwamba kila kata itatumia gharama sawa za fedha hizi, bali kuna kata itatumia Sh20 milioni kutokana na idadi ya vituo vya kupigia kura kuwa vichache na kata yenye vituo vingi kwenye uchaguzi huu itatumia Sh150 milioni,” amesema Kailima.

Kailima amesema vyama vya siasa vinatakiwa kuhakikisha vinawaelimisha wafuasi, wapenzi na wanachama wao juu ya kutekeleza maadili katika kipindi chote cha kampeni.

Amesema maadili yatakiukwa, chama husika pamoja na mgombea watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Kailima amesema baadhi ya vitendo vya kuvunja maadili ya uchaguzi ni kuchana mabango ya wagombea, kutoa lugha chafu wakati wa mikutano ya kampeni na kupitisha muda wa kufanya mikutano ya kampeni.

Amesema kamati za maadili za kata na jimbo zitachukua hatua kali kwa chama au mgombea ambaye atakiuka maadili na kwamba, zinatakiwa kuchukua hatua ndani ya saa 48 baada ya chama au mgombea anapovunja maadili.

Amezitaja baadhi ya adhabu ni kuomba radhi wananchi hadharani, kutotumia vyombo vya habari kwa muda fulani wakati wa kampeni, onyo la maandishi, kusimamishwa kufanya kampeni, mgombea kutangaza mbele ya vyombo vya habari kuwa yeye ni bingwa wa kukikuka maadili ya uchaguzi au kutozwa faini ya Sh100,000.

Chanzo: Mwananchi

Baada tu ya kuona hizo 2.5 bilioni sikuhangaika kusoma hayo madudu mengine.
Kweli inauma sana kuona jinsi watanzania tunavyokabwa kila kona kulipa kodi halafu kuna wengine wanakaba kila kona kuhakisha zinaenda na maji!Inashangaza sana kuona viongozi waliojinadi majukwaani kufahamu shida na dhiki za watanzania wakiwa ndio wako msatari wa mbele kutapanya hela za watanzania kukidhi maslahi yao ya kisiasa kwa kuwanunua madiwani na hata kuwapambikizia wengene kesi za ajabu kura zirudiwe waone kama ccm itashinda.

Kwa mambo yaliondelea kwa nafasi hizi za madiwani kurudiwa, naamini kama wote wangekuwa ccm naamini kusingekuwa na hizo nafasi wazi labda iwe diwani amefariki.
Hizo 2.5 bilioni zingetatua matatizo mangapi ya wananchi katika hizo kata husika?
 
Binafsi naona matumizi ya sh 2.5 bil kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa madiwani ni upotezaji tu wa fedha za walipakodi. Kwa kuwa wakuu wa mikoa ya huko bara hawajaonyesha ubunifu wowote utakaohitaji fedha ya ziada, napendekeza fedha hizo apewe mkuu wa mkoa wa Dsm Makonda zikatumike katika miradi ya madarasa na miundombinu aliyoibuni. Hayo mambo ya uchaguzi yasubiri 2020, hata ule wa Nyalandu usubiri na mbunge Kingu akaimishwe hilo jimbo. Nawasilisha!!
 
Naomba unitajie kifunga cha sheria kinachoruhusu Mbunge kukaimu jimbo lingine
 
Naomba nitajie kifungu cha sheria kinachomruhusu Supika wa bunge kuwa msemaji wa chama cha siasa bungeni!!
Unajua kabisa Spika ni mbovu halafu tena unahoji.

Nilichokuuliza ndio nimekisoma kwako leo, Je sheria ya hilo jambo ipo? Hilo jambo limewahi kutokea jimbo lipi? Lini?
 
Cheti cha kidato cha nne ameshakipata hata tumpe hizo pesa za wavuja jasho atujengee miundombinu?
 
Back
Top Bottom