Tume ya uchaguzi nchini Uganda imewatahadharisha polisi nchini humo dhidi ya kuwazuia wagombea wa urais kuendesha kampeni zao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Tume hiyo imesema kuwa imepokea baadhi ya malalamiko kutoka kwa wagombea wa urais na pia kuona taarifa zavyombo vya habari kwamba polisi inazuia na kuvuruga kampeni zao .

Wakati huo huo katika taarifa ya pamoja ya mabalozi wa nchi za Muungano wa Ulaya nchini humo, wameeleza kutofurahishwa kwao na ghasia zilizotawala kampeni ya uchaguzi tarehe 18 na 19, Novemba nchini humo.

Wamesema Uganda ilishuhudia ghasia na maandamano pamoja na matumizi yasiyofaa ya vikosi vya usalama dhidi ya raia na kuvitaka vyama vyote vya kisiasa na wagombea wake kuwataka wafuasi wao kuacha ghasia na matumizi ya lugha mbaya.

Wametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kumaliza uchokozi unaolenga kuleta ghasia au kusababisha ukiukaji wa sheria.

Hii inajiri huku Kiongozi wa upinzani nchini huo Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine alilalamikia kuzuiwa kuendesha kampeni zake katika mji wa Hoima magharibi mwa nchi hiyo.

Katika ujumbe wake wa twitter Bobi Wine amesema kuwa polis walifunga barabara za kuelekea katika mji huo ili kumzuwia kufika katika hoteli aliyotarajia kupata malazi na kuziamuru hoteli zaote katika mji huo zisimpokee na timu yake, na hivyo kuwalazimisha kulala ndani ya magari:
 
Nami naona dalili za mzee kwenda chini, manake naona kabaki na jeshi tuu, naona tume, media, zoote zimemgeuka mzee
 
Museveni aliichukua nchi akitokea msituni, hataweza kukubali kuachia nchi kwa njia ya makaratasi.
 
Back
Top Bottom