Tume ya uchaguzi na jeshi la polisi vinampa Rais kiburi

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,821
11,526
Ukiangalia sasa hivi namna rais anavyoongoza hili taifa, ni dhahiri shahiri kuwa amelewa madaraka na hajali tena wananchi wake, si wakulima wanaolima kwa shida na tabu, si wafanyabiashara wala wafanyakazi wana ahueni kwa sasa, kila wanapojaribu kuongea wanakejeliwa na kutishiwa.

Haya yote yanafanyika kwa sababu hatuna tume huru ya uchaguzi, kama hii ingelikuwa na tume huru na huru kweli kweli rais Magufuli asingelikuwa na kiburi hivi, angeonesha kuwajali wananchi na kusikiliza kile wanachokihitaji.

Rais amekuwa na kiburi kwa sababu anajua fika kuwa tume ya uchaguzi ipo chini yake, hata uchaguzi ukifanyika leo lazima ashinde pamoja na udhaifu wake wote, vile vile jeshi la polisi lipo kwa ajili yake na sio kwa ajili ya wananchi, yule ambae atahoji na kupinga chochote jeshi la polisi litamshughulikia.
Rais anatenda haya akijua kuwa mwaka 2020 hakuna uchaguzi bali kutakuwa kuidhinishwa, ndio maana hajali vilio vya wananchi baadala yake anawakejeli na kuwatisha.
 
Yoote hayo ni kwa sababu ya katiba mbovu yenye elements za kikoloni!!!! Na wa kulaumiwa hapa ni JK na unafki wa kiswahili.
 
Tatizo ni lile dubwana linalozunguka nchi nzima. Nasikia ndio uchawi mkubwa kuwaroga wadanganyika wasijielewe.
 
Ajitafakari sana kwani hakuna nguvu ya dola iliyowahi kuishinda nguvu ya umma!
 
Ametia MFUKONI,

1. Bunge

2. Wanataaluma vyuoni

3. NBS

4. Vyombo vya habari

5. PoliCCM

6. UsalamaCCM

7. JWTZCCM

8. WabungeCCM ( Hawa Misukule Kabisaaaa )

9. MahakamaCCM ( Jaji Mkuu )

10. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

11. Hazina ( Fuko la hela analo analo nyumbani kwake, anagawa kwa kila anayemfurahisha )

12. Anahonga mavyeo kwa anaemtaka wa kumfurahisha e.g KIMEI wa CRDB kaahidiwa cheo kwa kumfurahisha kujenga tawi CHATU !

- Kwa yote hayo JITU lenye roho mbaya kama hilo LITAKOSAJE Kiburi ??
 
DAAAH HATARI SANA!!!!!
DAWA YA MOTO NI MOTO.
 
Jakaya alitaka awachie Katiba Mpya yenye Tume huru ya Uchaguzi Na iliyopunguza Madaraka ya Rais mkasusa na kutoka Bungeni Na alipowabembeleza mkamwambia ilalipofikia inatosha amuachie Rais ajae ( Uncle Magu) atakuja kumalizia, Tuwe wavumilivu Magu ataimalizia
 
Jakaya nae wale wale.
 
Ana kiburi Sana
Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu Sana.
 
Ametia MFUKONI,

1. Bunge

2. Wanataaluma vyuoni

3. NBS

4. Vyombo vya habari

5. PoliCCM

6. UsalamaCCM

7. JWTZCCM

8. WabungeCCM ( Hawa Misukule Kabisaaaa )

9. MahakamaCCM ( Jaji Mkuu )

10. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

11. Hazina ( Fuko la hela analo analo nyumbani kwake, anagawa kwa kila anayemfurahisha )

12. Anahonga mavyeo kwa anaemtaka wa kumfurahisha e.g KIMEI wa CRDB kaahidiwa cheo kwa kumfurahisha kujenga tawi CHATU !

- Kwa yote hayo JITU lenye roho mbaya kama hilo LITAKOSAJE Kiburi ??
Hapo namba 11, siku hizi anatembea na kapu la pesa kama tuko kwenye ujima vile
 
Nchi za nyungi za kiafrika hakunaga uchaguzi ni viini macho tu. Burundi wanataka kupiga kura ukionekana unaunga mkono kinyume na Nkurunziza unakamatwa au kuuwawa, sasa huo ni uchaguzi gani?
 
Tena 2020 wasitupe kiini macho kuchezea kodi zetu wakati washindi tayari wanao, heri hizo hela wakatunulie Dawa hospital
 
Back
Top Bottom