Uchaguzi 2020 Tume ya uchaguzi na CCM wainajisi katiba, Deo Mwanyika hastahili kuteuliwa wala kugombea ubunge kwa sababu ya kesi ya kukwepa kodi

Labda tujue kwanza tafsiri na maana ya kisheria ya;

"...Ndani ya miaka mitano asiwe ametiwa hatiani kwa kosa la ukwepaji kodi...."

Sasa, sisi tunasema " amekosa sifa kwa kuwa alitiwa hatiani kwa kosa la kutolipa kodi"

Lakini, mahakama haikumtia hatiani. Kilichofanyika ni mshtakiwa na mshtaki kuelewana nje ya mahakama na kisha anayeshtaki kupeleka kusudio la "kutoendelea na kesi"...

Katika mazingira haya, hakuna hukumu ya mahakama hapa. Japo ni kweli kabisa kuwa alishtakiwa....

Lakini kabla kesi kusikilizwa hadi mwisho kisha hukumu kutolewa, ikawa imefutwa...!

Katika mazingira haya mtu atawezaje kusema alishtakiwa na kuhukumiwa na kisha amwekee pingamizi?

Kisheria, Deo Mwanyika hajawahi kuhukumiwa na mahakama kwa kosa hili...!

NEC watakuuliza swali dogo na rahisi tu, kuwa, uayo nakala ya hukumu hiyo kama ushahidi?

Hapa Deo Mwanyika kama Deo Mwanyika, hana kesi na hajawahi kuhukumiwa na mahakama kwa kosa hili...!

Shida inakuja kwa CCM kilichomteua awe mgombea wao huku kikitambua kuwa aliwahi kufanya kosa la kimaadili la kukwepa kulipa kodi na mwisho wa siku wajaelewana nje ya mahakama na akawalipa. Hili watu wote wanajua na waliona...!!

CC: Majota Cossata
 
Tuweke rekodi sawa, Deo Mwanyika alihukumiwa kwa kukwepa kodi.

Michango ya NSSF ya Deogratius Mwanyika, aliyekuwa Rais wa migodi ya Pangea, North Mara Exploration na Bulyanhulu, imelazimika kulipa sehemu ya fidia ya makubaliano maalum kwa Serikali baada ya kukiri kufanya makosa.

View attachment 1554081
Fedha kiasi cha TSh bilioni 1, kilichotwa na kuingizwa kwenye akaunti ya maalum ya fedha za serikali inayosimamiwa na Hazina iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mnamo Mei 11, 2020.

Makubaliano ya faini yaleta utata hadi Ikulu kuhusishwa
Juni 17, 2020 Mwanyika aliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, pamoja na wenzake wawili, baada ya Serikali kueleza kwamba Mwanyika amekubali kulipa fidia ya TSh bilioni 1.5. Mwanyika na wenzake wawili, Assa Mwaipopo.

KATIBA INASEMA IVI
67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-👇🏽

(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;

(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
Hiyo ya mwisho hapo chini ni uongo na upumbavu wa hali ya juu. Katiba ya JMT haisemi hivyo hata kidogo.
 
Hivi inakuwaje?Mtu anatajwa Kwenye orodha ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ..anaitwa polisi anakaa siku kadhaa akihojiwa...anaachiliwa.
Anakuja kupewa nafasi ya kugombea ubunge na serikali hiyo hiyo iliyo wahi kum arrest Kwa madawa??..umakini uko wapi?
Kama alisingiziwa je wale wengine hawakusingiziwa?
Na why serikali iwasingizie watu?
Kama hakusingiziwa why mumlete agombee ubunge?..mnaeleza wananchi kitu gani???
Sharia zipo kwa ajili ya upinzani kaka,hazimhusu kila mtu, elewa hilo
 
Hivi inakuwaje?Mtu anatajwa Kwenye orodha ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ..anaitwa polisi anakaa siku kadhaa akihojiwa...anaachiliwa.
Anakuja kupewa nafasi ya kugombea ubunge na serikali hiyo hiyo iliyo wahi kum arrest Kwa madawa??..umakini uko wapi?
Kama alisingiziwa je wale wengine hawakusingiziwa?
Na why serikali iwasingizie watu?
Kama hakusingiziwa why mumlete agombee ubunge?..mnaeleza wananchi kitu gani???
Hatari sana nchi hii
 
Back
Top Bottom