Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi mnamuelewa Mzee Butiku?

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,264
12,561
Mzee Butiku alikuwepo kwenye awamu zote, yupo na atakuwepo Mungu akipenda. Inaelekea kuwa Mzee Butiku anafahamu mengi kuhusu mambo ya chaguzi zetu na mambo ya tume zetu hizi za uchaguzi kwa miaka 60 Sasa.

Mwaka huu Mzee Butiku kila anapopata nafasi ya kuzungumza jukwaani anasisitiza umuhimu wa mwaka huu uchaguzi kuwa huru na haki kwelikweli kuliko miaka iliyopita. Anasema uchaguzi wa aina hii ni lazima na tunao uwezo wa kuwa na uchaguzi wa aina hii mwaka huu.

Bila shaka mzee Butiku kuna ndoto ameota kuhusu taifa letu ambayo anashindwa kuisema hadharani kutokana na sababu mbalimbali. Hebu Tume yetu sikivu msikilizeni kwa karibu na kumhoji sana mzee Butiku ili mfahamu anachokimaanisha kuhusu uchaguzi wa mwaka huu kuwa huru na haki ana maanisha nini, ameona Nini, amenusa Nini tofauti na chaguzi zilizopita? Kwani tume zilizopita hazikuwa zikitenda haki kwenye chaguzi?

Kinywa cha mzee hakisemi uongo japo kinanuka ugolo, shughuli bila wazee sio shughuli na Ngoma ya watoto haikeshi
 
kavulata,
Mkuu ni vizuri ukaweka na ile video ya Mzee Butiku kwenye uzi wako au mwambie mkuu bagamoyo akuwekee ile video kwenye uzi wako, mada yako ndo italuwa imekamilika vizuri
Iweke tafadhali Kama unayo, lengo Ni kuihubiri amani yetu iendelee kuwepo. Tanzania Ni kubwa kuliko mtu au kikundi.
 
Back
Top Bottom