Tume ya uchaguzi itoe karatasi ya mfano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya uchaguzi itoe karatasi ya mfano

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Shedafa, Oct 22, 2010.

 1. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2010
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ni busara kwa muda uliobaki tume ya uchaguzi itoe karatasi ya mfano ya kupigia kura ili wapiga kura waanze kuiona na kuizoea, pia ianze kutoa mafunzo jinsi ya kupiga kura. Hili ni jambo muhimu wala wasifanye kwa kujiamini tu kuwa watz tunaelewa, kupiga kura ni kila baada ya miaka 5 hivyo wengi watakuwa wamesahau.

  Mbali na kusahau tuna wapiga kura wapya wengi tu wanaingia ulingoni kwa mara ya kwanza, na ukichukua idadi kama walivyoitoa wapiga kura wapya wanaweza kuzidi mil 10. kwa hiyo somo la jinsi ya kupiga kura ni la muhimu mno.

  Waanze kutumia vyombo vya habari kuelimisha kuanzia sasa, tafadhali hili ni la muhimu. Na kama wao wanaona si muhimu naviomba vyama vya siasa kuwashauri hawa waheshimiwa ili waanza kutumia muda uliobaki kwa mafunzo ya jinsi ya kuitumi karatasi ya kupigia kura. Kwanza tuione inafananaje, halafu jinsi ya kupiga kura bila ya kupoteza haki ya kuchagua kwa kuharibu kura.
   
Loading...