Tume ya Uchaguzi inapaswa kujivua gamba sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tume ya Uchaguzi inapaswa kujivua gamba sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Jun 17, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  KAMA kuna wakati ambao tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatakiwa kujivua gamba ni sasa kutokana na kupoteza imani kwa wadau na umma kwa ujumla.

  Kama chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kutangaza hadharani kuwa kinajivua gamba kwa maelezo kuwa kinataka kurudisha imani yake kwa wanachama na umma kwa ujumla, basi viongozi wa NEC nao wachukue maamuzi magumu ya kujivua gamba.

  Kwa miaka 19 iliyopita tangu Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, alipounda NEC kumekuwepo na malalamiko makubwa dhidi ya chombo hicho cha kusimamia shughuli za uchaguzi nchini; kwamba kimekuwa kikipendelea chama tawala.

  NEC iliundwa mwaka 1992 baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi kwa sheria namba 5 ya Julai Mosi, 1992. NEC ilipoundwa chini ya uenyekiti wa Jaji Lewis Makame, changamoto za kwanza ilizokabiliana nazo ni kusimamia na kuratibu chaguzi ndogo zilizofanyika muda mfupi katika majimbo ya Kwahani, Tabora Kusini na Igunga.

  Vyama vya siasa vilivyoshiriki katika chaguzi hizo vililalamika kuchezewa fujo na CCM bila NEC kuchukua hatua na wakati huo huo kulalamikiwa kwamba hata makamishina wake walikuwa wanachama wa CCM.

  Uthibitisho wa madai hayo ulibainika baada ya baadhi ya waliowahi kuwa makamishna wa tume hiyo kujitokeza kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa kupitia chama tawala.

  Aidha, udhaifu wa NEC ulibainika katika kusimamia na kuratibu chaguzi za mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 pamoja na changzi ndogo zilizofanyika katika kipindi hicho.

  Pamoja na lawama kwamba NEC inaundwa na makamishna ambao ni makada wa CCM, lakini pia chombo hicho kinaonekana kukosa uhuru wa kufanya maamuzi kutokana na kasoro kubwa ya sheria ya uchaguzi.

  Lawama nyingine inazotuhumiwa nayo NEC ukiondoa kukosa uhuru wa kufanya maamuzi, ni menejimenti yake kuendesha mambo bila uwazi na kutojibu hoja zinazoelekezwa kwake na wadau mbalimbali hususan vyama vya siasa na vyombo vya habari.

  Jumatatu wiki hii, ulifanyika mkutano baina ya NEC na wadau wengine kama vyama vya siasa na wakurugenzi wa halmashauri ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo na kata.
   
Loading...