Tume ya Uchaguzi ifafanue kuhusu Uteuzi Viti Maalum CHADEMA

NEWSINKP

Member
Sep 26, 2016
77
92
Wasalaam,

Nmetafakari sana juu ya mambo kadhaa ya chaguzi zetu hasa hili la Viti maalumu vya CHADEMA na kuona iko haja ya NEC kutolea ufafanuzi juu ya mambo yafuatayo;

Vinginevyo naona kama kuhusishwa kwa NEC na hili swala kutaaminisha wananchi zaidi kua sio tume huru.

01. Kauli za Mahere kama ilivyorushwa na azam tv kua mpaka ile tarehe 20.11.2020 NEC haikupokea majina toka CHADEMA na hii nyingine ya kusema NEC ilipokea majina tarehe

19.11.2020. NEC angalieni hizi tarehe na kuzitolea ufafanuzi nafkiri italeta imani zaidi( Mkizingatia pia kua Ndugai alidai kupokea list toka NEC tarehe 20.11.2020 siku ambayo Mahera alisema mpaka siku hiyo hawakupokea list toka CHADEMA)

02. Tukiassume kua ni kweli List ilipelekwa NEC na KM CHADEMA, je kwa nini NEC ilipitisha jina la mtu aliekua gerezani bila hata kuhoji alijazaje form zake na ataapishwa vipi ikiwa shauri lake bado halijaisha mahakamani?

03. Kwa kua uongozi wa juu wa CHADEMA mpaka sasa umekana kupeleka majina NEC, ni wakati sasa wa NEC kumtaja aliepeleka barua ya CHADEMA yenye hayo majina, ikibidi ioneshe mpaka sehemu mtu huyo aliposaini mara baada ya kufika ofisi za NEC maana ninaamini kuna kitabu cha wageni ambapo lazima kisainiwe.

NEC ikishaweka hayo mambo 3 bayana, then tutagundua exactly where the wheel went off. La sivyo wananchi wataendelea kuamini kua tume iko one sided.

Tukimaliza hili swala la Tume tutauliza taratibu za kimahakama juu ya sakata la Nusrat, ili tuunganishe maelezo yote toka NEC na Magereza ndipo tutakapojua mchawi ni nani.

Ahsanteni,

Mwananchi asiye na Chama.
 
Huwezi amini mambo yanayofanyika nchi hii, mambo yote hayo yamefanyika kimagumashi huku mfumo inasemekana kuhusika.

Yani tumefika sehemu serikali ina Fanya jinai mchana kweupe kabisa tena bila hofu, viongozi wametuzarahu kwa kiwango cha juu sana na wananchi tunashangilia, sijui ni wapi wanalipeleka hili taifa hawa wahuni.
 
Huwezi amini mambo yanayofanyika nchi hii, mambo yote hayo yamefanyika kimagumashi huku mfumo inasemekana kuhusika.

Yani tumefika sehemu serikali ina Fanya jinai mchana kweupe kabisa tena bila hofu, viongozi wametuzarahu kwa kiwango cha juu sana na wananchi tunashangilia, sijui ni wapi wanalipeleka hili taifa hawa wahuni.
Kuna jamaa aliwahi kutuambia kwamba tumekabidhi nchi kwa wash...ba! Sasa niambie hiki kilichotokea ni nini kama sio ush...ba
 
Mleta uzi ina maana unasubiri mpaka tume itoe ufafanuzi ndio ujue kuwa sio huru? Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu anajua tume hii sio huru, haya yanayotokea ni kusaidia wale wazito wa kuamini kuwa tume sio huru.
 
NEC hawatafanya kikao chochote kile kuondoa huo mkanganyiko kwasababu wanajua wazi kabisa hii nchi imejaa wajinga ,hawana chakufanya chochote ili wadai haki zao.

Na hata ambao watakaodai haki let say mahakamani, na huko kesi itahukumiwa na NEC B,mwisho walalamikaji watashindwa kwa kishindo

Cha msingi wananchi wachache tunaojielewa tutumie akili zetu kutambua ukweli ili siku za baadae tuwasimulie vijana wetu historia ya ukweli ya nchi hii,historia ya ukweli ya utawala wa MAGUFULI.
 
Mkuu Kina Halima na Group lake la Covid19 wamewekwa na system kupitia BIASHARA YA UTUMWA.
Sasa hivi wapo chini ya Ulinzi na Utetezi wa watesi wao,wanawaalika kwenda CCM kwa kuwa ni wanawake majembe.Nisichokifahamu ni kuwa,wamefikia lini hiyo hatua ya maisha ya wanadamu!Inakuwaje watetezi wa Halima na wenzake wawe ndani ya CCM Mpya?
Jinai kwenye sakata hili ni ya kutisha na mbaya zaidi kuliko tunayoyafahamu.
 
Nec wanafanya Mambo ya hovyo Sana, kwenye nchi zingine walipaswa kufukuzwa kazi Mara moja.kitendo Cha uongozi wa chama Cha chadema kukataa kutopeleka majina Tume ni fedheha Sana, nec wanapaswa kuwasikiliza chadema wenye wabunge na kuchukua maamuzi na Sio kubishana nao
 
Ktk zama hizi kinawezekana kilichofkriwa kutowezekana,Nikikumbuka yule aliyekuwa mbunge akipatiwa matibabu na mamlaka kusema haijui alipo??? Siwezi kushangaa chochote kingne kitakachotokea
 
NDUGU YANGU NEWSINKP, UWE NA HAKIKA KUWA HUO UAFAFANUZI UNAOTAKA TOKA KWA KILE KINACHOITWA "TUME HURU YA UCHAGUZI" HAUTATOLEWA KWA SABABU ZA WAZI KABISA. WAO NI SEHEMU YA HUO MCHEZO WOTE

POLE
 
....Tukimaliza hili swala la Tume tutauliza taratibu za kimahakama juu ya sakata la Nusrat, ili tuunganishe maelezo yote toka NEC na Magereza ndipo tutakapojua mchawi ni nani.
Ha ha ha... Wewe mpaka saivi hujajua kuwa ccm inatumia NEC na mfumo wote wa serikali kufanikisha mambo yake kwa gharama yoyote?!!!
 
Back
Top Bottom