Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,797
- 11,959
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemtangaza Dkt. John Magufuli, aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kuwa mshindi wa Uchaguzi uliofanyika Oktoba 28. Pia imemtangaza Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais Mteule.
Dkt. Magufuli ameshinda kwa kupata kura 12,516,252 (sawa na 84.4% ya kura halali) akifuatiwa na aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ambaye amepata kura 1,933,271 (sawa na 13.04% ya kura halali)
Dkt. Magufuli ambaye pia ni Rais wa Tanzania amepata ridhaa ya kuongoza kwa muhula wa pili kama Marais waliotangulia.
Tume imesema walikuwa na jumla ya watu 29,754,699 waliojiandikisha kupiga kura, na waliopiga kura walikuwa 15,091,950. Kura halali zilikuwa 14,830,195 huku kura 261,755 zikiwa zimeharibika.