Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,578
Wanabodi,
Naafuatilia kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa live na Star TV kila Jumamosi asubuhi, kwenye kipindi cha leo, kutoka Mwanza, kinaongozwa na mkongwe, Doto Bulendu, na wageni wake waandishi wakongwe, Moses Mathew na Odero, na Dar es Salaam yuko Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena.
Mjadala unahusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Uchaguzi, (NEC), imeingizwa lawamani kwa kitendo chake cha kuwaengua wagombea mbalimbali kwa makosa madogo madogo ya ujazaji wa fomu, au kwa hoja nyepesi nyepesi, ambazo hazina mashiko ya kisheria kumfanya mgombea akose sifa na uhalali wa kugombea, mwanajopo mmoja akasema, kinachofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ni ukiukwaji wa haki za binaadamu!.
Mwana jopo huyo, amesema, kanuni za uchaguzi zimeeleza wazi kuwa kabla fumu haijapokelewa, huwa inahakikiwa. Lengo la uhakiki ni kurekebisha dosari ndogo ndogo za ujazaji fomu hiyo, na kutolea mfano, kuna mgombea ameenguliwa kwa dosari ndogo tuu ya kutumia initio ya jina lake.
Kugombea ni moja kati ya haki za msingi za binaadamu ziliziainishwa kwenye Katiba ya JMT, hivyo kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwaengua baadhi ya wagombea kwa dosari ndogo ndogo ni ukiukwaji wa haki za wagombea.
Mwendeshaji kipindi, Mkongwe Doto Bulendu, amelipongeza Jukwaa la Wahariri, kuwapatanisha TBC na Chadema, baada ya Chadema kuwafukuza TBC kwenye kampeni zao. Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri, Neville Meena, amezipokea shukrani hizo kwa shingo upande kwa kutumia msemo wa lugha ya Kilatini, kuwa "hupaswi kushukuriwa kwa kutimiza wajibu wako".
Meena amekiri waandishi wa habari na vyombo vya habari, havikutimiza wajibu wake kikamilifu kwa kunyamazia unfairness iliyofanywa na NEC kuwaengua wagombea na kukubali pingamizi zenye hoja nyepesi nyepesi. Kama media zingeliangazia suala hili kikamilifu, lingeisaidia NEC kutenda haki.
Pia NEC, imeingizwa lawamani, kwa kuelezwa kuwa uamuzi wa NEC kuengua wagombea ni uamuzi wa mwisho, final and conclusive, huu ni udikiteta. Katiba ya JMT, inaeleza wazi mahakama ndio mamlaka ya mwisho ya utoaji haki, sasa NEC isipotenda haki, kwa kumuengua mgombea kwa maonevu, mgombea kama huyu aende wapi?.
Jopo pia limeilaumu sheria yetu ya uchaguzi, ina mapungufu makubwa yanayafanya uwanja wa mapambano usiwe sawa, kwa mgombea mmoja kugombea huku akiwa ni rais wa JMT, anagombea na urais mkononi, halafu anashindana wagombea wengine with nothing!. Usawa uko wapi? Japo limenote kuna wakati mgombea mmoja anatoa ahadi za kampeni ambazo ni firm akiwa kama ni rais wa JMT na sio kama mgombea wa CCM.
My Take
Lawama hizi kwa NEC, zisiposhughulikiwa in time, zitatuharibia matokeo ya uchaguzi wetu kwa kusababisha bitterness ndani ya mioyo ya watu kuwa uchaguzi Mkuu ujao sio huru na haki. Dhulma hii itasababisha accumulation ya bad karma, ambayo itakuja kuponza watu mbele ya safari kwa wahusika na dhulma Hugo kukumbwa na majanga ya ajabu!. Na kitu kibaya kuhusu karma, huwa inawatandika wahusika na wasio husika, kwasababu wameona dhulma hiyo na walikuwa na uwezo wakuzuia but they did nothing.
Kwavile JPM na CCM watashinda kwa ushindi wa kishindo kikubwa anyway na anyhow, naiomba Tume ya Taifa Uchaguzi, iache milango wazi kwa wagombea wote wa vyama vyote hata wenye mapungufu, waruhusiwe tuu, wajaribu na washindwe wenyewe ili kuizuia bad karma ya kutumia kudhulumiwa. Watakaposhindwa kwenye sanduku la kura, hata wasipate sababu na visingizio, na hata wakiumia, hakuna karma.
Paskali