Tume ya Taifa ya uchaguzi(NEC), Magufuli katika mabango ya campaign ni mgombea wa chama gani?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Nikiwa mji mdogo wa Usa-River hapa mkoani Arusha,nimeshuhudia Bango moja kubwa kabisa likiwa na nembo ya chama kimoja kikubwa kabisa cha siasa na picha ya mgombea wa chama hicho ila kilichonishangaza katika bango hilo ni jina la mgombea wa chama hicho lililoandikwa katika bango hilo la campaign linalosomeka "Makufuli" wakati hakuna mgombea anaetambulika kwa jina hilo labda kama Tume wana mtu wa aina hiyo tofauti na hawa tunao wajua

Ujumbe katika bango hilo unasomeka: "CHAGUA MAKUFULI-2015", ujumbe huu ukiwa ndio ujumbe uliopewa uzito mkubwa kabisa sambamba na yale maneno yao mengine yakiandikwa kwa chini katika bango hilo.

Sitaki kabisa kuamini kama hii ni bahati mbaya au ni makosa ya kiuandisha tu bali hapa kuna sababu. Inawezekana wanaona jina hilo lina-sound better kuliko jina halisi la mgombea wao kwa wapiga kura.

Tuseme ni Sawa tu, lakini je ni sahihi kisheria kufanya hivi?

Hivi sheria zetu za uchaguzi ndio ziko loose kiasi hiki?

Je,mabango haya ya campaign hayasimamiwa na sheria za uchaguzi?

Kama hayasimamiwi na sheria,je kila mtu akiamua kuweka bango lake ni kuweka jina alitakalo na kisha kutumia nembo ya chama chochote kile hali itakuwaje?

Hivi kweli mabango ya uchaguzi yanaweza tu kuwa printed na kisha kusambazwa mithili ya t-shirt za msiba n.k bila kuwa na udhibiti wa kisheria?

Kama karatasi za kupigia kura zinaandaliwa kwa kuzingatia sheri, inakuwaje mabango haya rasimi ya wagombea yasiwe na udhibiti

Kama sheria ziko loose kiasi hiki,mbona kwenye karatasi ya kura hakuna mgombea wa chama cha UKAWA?

Kama mikutano ya campaign inasimamiwa na sheria pamoja na kanuni za uchaguzi,iweje uholela huu kwenye haya mabango ya uchaguzi?

NEC,Makufuli katika bango hili ni mgombea wa chama gani?!

Are we serious?
 
Salary Slip ,Hujapata bado mshahara wako???Maana mpaka sasa naona serikali karibu itakuwa mufilisi....Kimbilia bank.

Salary Slip,siku ya kupiga kura tutamtafuta MAKUFULI tusipoliona jina tutaacha tumpigie wa karibu.............USIMWAMSHE ALIYELALA..............
 
Mabango si nyaraka rasmi zinazotambulika na Tume. Hilo ni suala la CHAMA kuchukua hatua kurekebisha dosari hiyo
 
Mkuu,nimekuelewa na hata mimi niliiona hatari hiyo kwa chama chao na mgombea wao.Ila kama ndio hivyo,basi kwenye uraisi karatasi ya kura iwe na jina la mgombea uraisi wa UKAWA ili twende sambamba na uhuru huu uliotolewa.
 
We ulijuaje ni rangi za chama kikubwa??!!kukosewa jina katoka tiketi si kizuizi cha kusafiri
 
Mabango si nyaraka rasmi zinazotambulika na Tume. Hilo ni suala la CHAMA kuchukua hatua kurekebisha dosari hiyo

Kama si nyaraka rasmi ni kwa nini Tume ina kemea pale mabango yanapo banduliwa? Acha akili za kushikiwa ndugu!
 
Mkuu,nimekuelewa na hata mimi niliiona hatari hiyo kwa chama chao na mgombea wao.Ila kama ndio hivyo,basi kwenye uraisi karatasi ya kura iwe na jina la mgombea uraisi wa UKAWA ili twende sambamba na uhuru huu uliotolewa.

Kaka hawa mpaka wagombea wetu naona wanwataka maana nimeona post huko zinsema Mnyika na Sugu wafanya maamuzi magumu duh.

From Nembo tu wagombea hakika tumewashika pabaya
 
Hivi kumbe arusha imependezeshwa na mabango ya muasisi wa mahakama ya mafisadi na majizi???? taratiibu wameanza kuelewa somo
 
Back
Top Bottom