Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwa uchaguzi wa ubunge wa Muhambwe utafanyika Mei 2, 2021

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwa uchaguzi wa ubunge wa Muhambwe utafanyika Mei 2, 2021.

Jimbo hilo lililopo Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma lipo wazi kuanzia Februari 12, 2021 kufuatia kifo cha Atashasta Nditiye.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na mkurugenzi wa uchaguzi NEC, Dk Wilson Mahera imeeleza kuwa tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, ameitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo.

Amesema kwa kuzingatia kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya uchaguzi, sura ya 343 ambacho kinaitaka tume kujaza nafasi ya kiti cha Ubunge katika kipindi kisichopungua siku 20 na kisichozidi siku 50 tangu kutokea kwa sababu iliyoacha nafasi wazi ya kiti hicho.

“Kutokana na matakwa hayo ya kisheria, tume inautaarifu umma kuwa Jimbo la Muhambwe liko wazi na uteuzi wa wagombea utafanyika Aprili 3, 2021 ambayo ni siku 49 tangu kutokea kwa kifo hicho,” amesema.

Amefafanua, fomu za uchaguzi zitatolewa Machi 28 hadi Aprili 3, 2021 kisha utafanyika uteuzi wa wagombea, kampeni za Uchaguzi zitakuwa Aprili 4 hadi Mei 1, 2021 na Mei 2, 2021 ndio itakuwa siku ya Uchaguzi.

Chanzo: Mwananchi
 
Natumai Mam Samia atakuwa Cman CCM tayari nataraji kuona fair play sio ule uhuni na dhuluma za kishamba.
 
Back
Top Bottom