Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iachane na njama za kuvuruga uchaguzi, zitaligharimu Taifa

RAKI BIG

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
394
456
Taarifa ya Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ndg. Ado Shaibu, leo tarehe 02 Juni 2020.
Chama cha ACT Wazalendo kinasikitishwa na kupinga vikali mwenendo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendesha mchakato wa mabadiliko ya Kanuni mbalimbali za Uchaguzi bila kuwashirikisha vya kutosha wadau wa uchaguzi hasa vyama vya siasa. Hadi sasa, Tume imekwisharekebisha Maadili ya Uchaguzi na sasa kwa maelezo ya Mwenyekiti wa Tume Jaji Semistocles Kaijage, ipo mbioni kukamilisha marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi za Madiwani, Wabunge na Urais.
A. Maadili ya Uchaguzi

Tarehe 27 Mei 2020, NEC iliitisha kikao cha wadau kwa ajili ya mjadala wa Maadili ya Uchaguzi. Cha kushangaza, NEC ilipanga ratiba ya kujadiliana, kufanya marekebisho na vyama kusaini maadili yaliyopitishwa ndani ya masaa machache (saa mbili hadi saa nane mchana). Licha ya maboresho machache kufanyika, NEC ilivilazimisha vyama kusaini siku hiyohiyo bila kuwasilisha kwanza toleo la mwisho la Maadili ya Uchaguzi lililojumuisha marekebisho husika.
Chama cha ACT Wazalendo ambacho mimi nilikiwakilisha kiligomea kusaini na kuomba haki ya kusaini baada ya kuona toleo la mwisho la Maadili ya Uchaguzi lenye maboresho yaliyotokana na maoni ya wadau. Jawabu la NEC kuwa Chama ambacho hakitasaini Maadili ya Uchaguzi siku hiyo hakitashiriki kampeni, lilitulazimisha kusaini sambamba na vyama vingine vilivyosaini siku hiyo.

B. Kanuni za Uchaguzi

Kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa mjadala wa Maadili ya Uchaguzi, Mwenyekiti wa NEC Ndugu Jaji Kaijage aligusia kuwa mchakato wa kukusanya maoni kwa ajili ya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi (Madiwani, Wabunge na Urais) umefanyika na NEC ipo mbioni kuzikamilisha. NEC inakusudia kufanya hivi bila kuwepo kwa kikao cha wadau kujadili rasimu ya mwisho ya Kanuni husika. Swali la kujiuliza ni kwa nini NEC inakwepa majadiliano na wadau? Ina jambo gani inalolificha? Ina njama gani kwenye kanuni za mwaka huu?
Rasimu za Kanuni ambazo zimewasilishwa kwetu zina mapungufu mengi. Licha ya kwamba tumeiandikia NEC kutoa maoni yetu, ni dhahiri NEC inataka kuyapuuza ndio maana inakwepa kikao cha wadau. Baadhi ya mapungufu kwenye rasimu hizo yanahatarisha amani na yanaweza kuitia nchi kwenye machafuko iwapo yataachwa kama yalivyo.
Baadhi ya mapungufu hayo ni;

i). Mawakala kunyimwa hati za viapo
Rasimu ya Kanuni zote mbili, ya Uchaguzi wa Madiwani na ya Uchaguzi wa Wabunge na Rais hazina sharti kwa wasimamizi wa uchaguzi kuwapa hati za viapo mawakala wa vyama vya siasa. Kanuni zote zimeweka utaratibu wa Wasimamizi wa Uchaguzi kutuma orodha na utambulisho wa mawakala kwa wasimamizi wa vituo. Kwa uzoefu, utaratibu huu utatumika kuwahujumu mawakala wengi wa vyama vya upinzani. Wasimamizi wa Uchaguzi wasio waadilifu watatumika kutowasilisha majina ya mawakala wa vyama vya upinzani.

ii). Mawakala kutopewa nakala za matokeo
Rasimu za Kanuni za Uchaguzi hazijaweka sharti kwa mawakala wa vyama vya siasa kupewa nakala za matokeo. Kanuni hizo zinasema nakala za matokeo zitatolewa iwapo kutakuwa na nakala za kutosha! (Kanuni ya 56(2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani na kifungu cha 63(2) cha Kanuni za Uchaguzi wa Wabunge na Rais). Swali la kujiuliza ni kuwa NEC haikujiandaa kwa uchaguzi? Haina hata fedha za kuzalisha nakala za kutosha na kuepusha mizozo isiyo ya lazima?

iii). Waangalizi wa Uchaguzi Kuzibwa Mdomo
Rasimu za Kanuni za Uchaguzi zinatumia lugha ya hiyari kwa NEC kuwaalika waangalizi wa kimataifa. Kanuni hizo pia zinakataza waangalizi wa kimataifa na wa ndani kuripoti kwa vyombo vya habari mapungufu ya uchaguzi watakayoyaona wakati uchaguzi ukiendelea (Kifungu cha 20(2)(j) cha Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani) na Kanuni za Wabunge na Rais.

Kuwawekea masharti waangalizi wa uchaguzi kuripoti baada ya uchaguzi kukamilika ni sawa na kuwaziba mdomo.

iv). Mfumo mbovu wa kuwajibisha Wasimamizi wa Uchaguzi
Rasimu ya Kanuni za Uchaguzi wa Madiwani (Kanuni ya 66(1) na kifungu cha 74(1) cha Kanuni za Uchaguzi wa Wabunge na Rais) zinatamka kuwa iwapo Msimamizi wa Uchaguzi atakwenda kinyume na Kanuni za Uchaguzi, Mkurugenzi wa Uchaguzi atamtaka Waziri mwenye dhamana kuchukua hatua za kinidhamu. Suala la kuwawajibisha wasimamizi wa uchaguzi linapaswa kuachwa mikononi mwa NEC pekee. Waziri ambaye ni kada wa CCM hawezi kuchukua hatua stahiki dhidi ya wasimamizi wa uchaguzi.

C: Wito Wetu

Kutokana na tuliyoyaeleza, wito wetu kwa NEC ni kama ifuatavyo;
i). NEC ishirikishe wadau vya kutosha kabla ya kufanya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi. Ni muhimu kwa NEC kufanya kikao cha wadau na kujadiliana juu ya mabadiliko ya Kanuni kabla ya kufanya mabadiliko hayo. Haitoshi kuendelea kufanya mabadiliko ya Kanuni kwa kuegemea maoni ya vyama yaliyowasilishwa kimaandishi. Ni lazima vyama vione rasimu ya mwisho na kutoa maoni yao kwa kikao rasmi kabla haijawa Kanuni.

ii). NEC iiepushe nchi na machafuko yasiyo ya lazima kwa kuhakikisha inaondosha vifungu ambavyo vitahatarisha amani ya nchi. Eneo nyeti ni la mawakala kupewa nakala za viapo na nakala za matokeo. Kinyume na hapo, NEC ijue kwamba inawasha moto kwenye petroli na italipa gharama za matokeo yatakayotokea.

Ado Shaibu,
Katibu Mkuu
ACT Wazalendo.
 
Ninyi wanasiasa hasa wapinzani ni watu wa ajabu sana, kwa miaka yote hii mnasema tume sio huru, mnakaa kimya miaka yote bila kulazimisha tume huru ya uchaguzi ipatikane, then yanakuja mambo ya kuwabana mnaanza kusumbua watu, acheni mambo yenu ya ajabu ajabu mliamua kuingia kwenye uchaguzi kwa tume hii, endeleeni na sio kutupigia kelele
 
Ninyi wanasiasa hasa wapinzani ni watu wa ajabu sana, kwa miaka yote hii mnasema tume sio huru, mnakaa kimya miaka yote bila kulazimisha tume huru ya uchaguzi ipatikane, then yanakuja mambo ya kuwabana mnaanza kusumbua watu, acheni mambo yenu ya ajabu ajabu mliamua kuingia kwenye uchaguzi kwa tume hii, endeleeni na sio kutupigia kelele

Ulitakaje boss, watu wameona mapungufu na wanayaweka wazi, je unatakaje hapo?
 
Hawa Jamaa wanaandaa mazingira ya wizi wa wazi wa kura,ukitaka kuhakiki hili watapinga ushauri na kushupaza shingo zao.Refa anawezesha fouls za wazi na goli LA mkono.Hii ni aibu na ndiyo maana tunasema Tume ya Uchaguzi siyo Huru hats kidogo. Inawezekana hizi kanuni zimeandaliwa na Polepole & co.
 
Huu upuuzi wa NEC ndio nakuambia kila siku ccm chini ya Magu haiwezi ushindani wa kisiasa zaidi ya kushurutisha kutawala. Haya ndio yale yale niliyokuwa nakuambia jiwe alikuwa anashinda ubunge kwa hila miaka yote. Sasa kila kitu kiko wazi.
Haya ni maandalizi tu ya kujiongezea muda madarakani baada ya vipindi viwili kupita.hawa jamaa akili itawakaa vizuri June 2024.
 
Hawa NEC wakitaka taifa liwe salama wasithubutu kabisa kufanya kazi na yule mzee kijana wa Lumumba..atawaharibia credibility kabisa. . Maana 2020 watu wameapa kufia kwenye vituo cha kupigia kura...uhuni uhuni sasa basi.
 
Mengine yote ya taarifa yake Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa ACT Mzalendo ni ya porojo tu zao za kisiasa, kutafuta mahali pa kutokea ( kuweka mpira kwapani) kukwepa uchaguzi ambao wana uhakika wa kutoka kapa, isipokuwa hili analokiri na kuthibitisha uchanga wake kisiasa.

Ati Chama cha ACT Wazalendo ambacho mimi nilikiwakilisha kiligomea kusaini na kuomba haki ya kusaini baada ya kuona toleo la mwisho la Maadili ya Uchaguzi lenye maboresho yaliyotokana na maoni ya wadau. Jawabu la NEC kuwa Chama ambacho hakitasaini Maadili ya Uchaguzi siku hiyo hakitashiriki kampeni, lilitulazimisha kusaini sambamba na vyama vingine vilivyosaini siku hiyo.

Yaani anakiri kusaini kwa kulazimishwa kweli! Ado msomi anayejitambua! Katibu Mkuu wa aina hiyo ni FUKUZILIA MBALI.
 
Wameanza kuogopa Uchaguzi

Wasubirie October tuwakate ngembe
Chama cha mapinduzi ni waoga, tuliwaambia toka mwanzo kama kweli mtu wao anakubalika mbona figisu nyingi? Yaani wanahangaika acha, sasa wameingia time, tume bila aibu inafanya mambo ya hovyo, hapa ndipo umuhimu wa tume huru ya uchaguzi. Shit!
 
Sawa
Hawa Jamaa wanaandaa mazingira ya wizi wa wazi wa kura,ukitaka kuhakiki hili watapinga ushauri na kushupaza shingo zao.Refa anawezesha fouls za wazi na goli LA mkono.Hii ni aibu na ndiyo maana tunasema Tume ya Uchaguzi siyo Huru hats kidogo. Inawezekana hizi kanuni zimeandaliwa na Polepole & co.

Hizo kanuni ni za jiwe mwenyewe. Hao wengine wanaiga tu.
 
Miaka yote mlishiriki na mkapata ubunge kwa kanuni hizi hizi
 
Wamefunzwa kulalamika tu na kinazito wanasiasa wa upinzani bongo ni vilaza sana
Vyama vya upinzani Tanzania mnatuchosha hamna maamuzi mpo kuralamika lalamika tu

Haya mmeona kuna makosa solution ni IPI toeni solution huu si mda wa ngonjera
 
Ninyi wanasiasa hasa wapinzani ni watu wa ajabu sana, kwa miaka yote hii mnasema tume sio huru, mnakaa kimya miaka yote bila kulazimisha tume huru ya uchaguzi ipatikane, then yanakuja mambo ya kuwabana mnaanza kusumbua watu, acheni mambo yenu ya ajabu ajabu mliamua kuingia kwenye uchaguzi kwa tume hii, endeleeni na sio kutupigia kelele
Tumeiliyopo ni huru waache woga
 
Huu upuuzi wa NEC ndio nakuambia kila siku ccm chini ya Magu haiwezi ushindani wa kisiasa zaidi ya kushurutisha kutawala. Haya ndio yale yale niliyokuwa nakuambia jiwe alikuwa anashinda ubunge kwa hila miaka yote. Sasa kila kitu kiko wazi.
Mbowe alipataje bunge ?tume hii iko huru hadi wazungu wanatuheshimu
 
Back
Top Bottom