Tume ya taifa ya uchaguzi nchini (nec) yakiri kutopingana na mawazo ya watanzan

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,280
2,000
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini (NEC) Imesema haitapingana na Mawazo ya Mabadiliko ya Kimfumo Kwenye Tume hiyo yanayotolewa na Wananchi Mbalimbali baada ya Wengi Kuonyesha Wazi Kutokuwa na Imani na Uhuru wa Tume hiyo Kiutendaji. Watanzania Wengi Wamekuwa Wakiupinga Uhuru Unaodaiwa Kwenye Tume hiyo Kwa Madai Kuwa bado Inaendeshwa na Serikali, hiyo Kushindwa Kutekeleza Majukumu yake Kwa Haki Wakati wa Chaguzi Mbalimbali. Tangu Kuanzishwa Kwa NEC 1992 Chini ya Mfumo wa Vyama vingi, Wananchi na Viongozi wa Vyama vya Siasa hususani vya Upinzani Wameonyesha Wasiwasi na Tume hiyo. Wasiwasi huu Unaoonekana Wazi Unamfanya Mwenyekiti wa NEC Taifa (Pichani) Jaji "Damian Lubuva" Kukutana na Wanahabari ili Kufafanua, Kubwa likiwa ni Mamlaka ya Rais na Mfumo wa Uteuzi wa Wajumbe wa Tume hiyo. Lakini pia Suala la Tume hiyo Kuitegemea Serikali Kifedha, nalo bado linazua Mjadala Mkubwa
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,056
2,000
Katika vikwazo vikubwa sana vya mabadiliko ya nchi hii , tume ya uchaguzi inaongoza ikifuatiwa na jeshi la polisi , hata kuboresha daftari la wapiga kura ni kwa maandamano ! Kuna watu wamepita pale nec nimejiapiza ni lazima nitawaburuza mahakamani , kama si leo basi kesho !
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom