Tume ya Taifa ya uchaguzi iwajibike kwenye vyama vyote vya siasa

songo mwene

Member
Jan 12, 2014
90
97
Nafikiri uchaguzi wa mwaka 2020 tume yetu ya uchaguzi ilishindwa kuwajibika katika kuhakikisha Nchi inapata wagombea sahihi kwa vyama vyote vya siasa.

Tume inawajibu wa kutoa elimu kwa wagombea pamoja na Wapiga kura,

Tume haikujikita katika kutoa elimu ya namna ya ujazwaji wa fomu za wagombea na kupelekea asilimia 90 ya wagombea wa upinzani kuenguliwa kwa madai ya fomu kuwa na kasoro,

Je tume bado inaweza kutoka hadharani na kujifia kuwa uchaguzi wa mwaka 2020 ulikuwa huru na haki?

Nadhani kama ambavyo baadhi ya viongozi akiwepo mheshimiwa Rais kuridhia kuwa tume huru ya uchaguzi, Sasa hoja iwe ni namna gani ya kuwapata wajumbe wa tume kwani ni rahisi kutamka kuwa tuwe na tume huru lkn tukapata wajumbe wasio huru? Tuangalie Nchi zilizo na tume huru ni jinsi gani tume zao zilipatika na sheria inasemaje kwa wajumbe wanao haribu uchaguzi kwa maslahi Yao.

Mwisho naomba wananchi nao washirikishwe kikamirifu kuhusu michakato inayoendelea na swala hili lisiachwe kwa wanasiasa pekee
 
Back
Top Bottom