Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 2,199
- 4,670
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema inaendelea kushughulikia rufani na pingamizi ziliyowekewa na wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa.
Mkurugenzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera, alisema wanaendelea kufanya uchambuzi wa rufani na pingamizi hizo na kuwataka wananchi kuwa na subira.
“Masuala ya pingamizi na rufani yamewekwa kotekote na ndiyo tunaendelea kuyashughulikia ,haya ni mambo ya kisheria, muwe na subira,” alisema Dk. Mahera.
Hivi karibuni, baadhi ya vyama hususani vya upinzani vimewalalamikia wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo 57 na kata 600 kuwaengua wagombea wao.
Juzi NEC ilitangaza majina ya wagombea 18 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliopita bila kupingwa na wanasubiri kukabidhiwa cheti cha ushindi wa ubunge mara baada ya uchaguzi kukamilika.